Symbion Power: Intelligence watupu

Nimetumia muda wangu mwingi kufuatilia maswala ya IPTL na Richmond/Symbion.
Kutoka kwa jamaa wa usalama wa taifa ambae anafanya kazi ikulu amenipa ukweli kuhusu mmiliki wa IPTL, Dowans, Richmond/Symbion.

Ukweli ni kwamba IPTL na Richmond ambayo kwa sasa ni Symbion zinamilikiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa serikali. Viongozi wa juu akiwemo kiongozi wa juu kabisa (jina limehifadhiwa) ndiyo wanaomiliki haya makampuni. Seth na mmiliki wa VIP ndugu Rugemalila ni kama mawakala tu lakini wala si wamiliki halali wa makampuni haya. Mtoa habari ameniambia mashine hizo zilinunuliwa kwa kodi za wananchi, kwa kupitia miradi hii viongozi wa juu wa serikali wamejivunia mabilioni ya pesa tangu miaka 90.

Ameniambia kuwa mashine hizi unufaisha takribani viongozi 72 moja kwa moja akiwemo waziri mmoja aliejiuzuru. Kuna viongozi wa ngazi za chini wenye influence au wenye kujua habari hizi wakiwemo usalama wa taifa upewa mgao kidogo ili kuwanyamazisha, pia utumiwa kwenye kampein za uchaguzi. Aidha wale wasiopewa mgao ndio vinara wa kutoa nyaraka za siri na kuwapa wapinzani.

Jamaa anasema, baada ya kugundulika kuwa Richmond haina mmiliki pale ambapo Mwakyembe alipokuta Marekani hakuna Kampuni inayoitwa Richmond , viongozi wa juu walimfuata mwanaume mwenye asili ya Asia wakampa milioni 800 ili ajifanye kuwa yeye ndie mmiliki wa Richmond, lakini huyo mmiliki alikataa kabisa kupigwa picha alipokuja nchini, alihofia sura yake ingeonekana ingekuwa ni hatari sana nchini kwake. Aliefanya mchakato mzima wa kutafuta mmiliki fake wa Richmond ambayo kwa sasa ni Symbion ni Rostam aziz. Mpaka sasa Symbion inadai deni lenye utata la zaidi ya dola milioni 100, wakati ukifika zitalipwa

Mtonyaji anasema, ili kupata njia rahisi ya kukwapua pesa za IPTL, viongozi walizua kesi fake ili kupitia wakili fake waweze kulipana hizo pesa. Wakili aliechaguliwa ni Mkono. Mkono amepewa jumla ya bilioni 60 na kitu kwa ajili ya kesi, fedha hii ni nyingi sana, lakini kutoka kwenye fedha hizo yeye alikuwa anachukua kiasi na baadhi anawapa wakubwa serikalini. Inasemekana mgao wa fedha za makampuni haya ni mkubwa sana kiasi kwamba wengi wamehamua kufungua account nje ya nchi hasa kwa kutumia majina ya watoto wao, majina yanatumika ni yale ya kikabila/kinyumbani kiasi kwamba uwezi kuwatambua kirahisi.

Kwa hiyo wadau; IPTL na Symbion, Dowans ni changa la macho, zinamilikiwa na viongozi serikalini. Kuna document nazisubiri, nitazitupia hapa

Hiki ndio M.k.were anakiita Kiherehere, sasa kilichokufanya ushindwe kusubiri ni nini?hii habari ilikuwa inakutekenya au? Yani Unatoa tuhuma lukuki kwa document unazozisubiri?seriously?

hebu tusifanyane wajinga aisee, tunauchukia ufishadi, lakini hizi ni kejeli kwa "collective inteligence" yetu hapa Jamvini.
 
Kikwete anahusika na IPTL from the scratch,since 1993 when he was minister of Muhongos' ministry.Kwa hiyo hizi deal zote kwenye energy sector anazijua kindakindaki
 
Nimetumia muda wangu mwingi kufuatilia maswala ya IPTL na Richmond/Symbion.
Kutoka kwa jamaa wa usalama wa taifa ambae anafanya kazi ikulu amenipa ukweli kuhusu mmiliki wa IPTL, Dowans, Richmond/Symbion.

Ukweli ni kwamba IPTL na Richmond ambayo kwa sasa ni Symbion zinamilikiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa serikali. Viongozi wa juu akiwemo kiongozi wa juu kabisa (jina limehifadhiwa) ndiyo wanaomiliki haya makampuni. Seth na mmiliki wa VIP ndugu Rugemalila ni kama mawakala tu lakini wala si wamiliki halali wa makampuni haya. Mtoa habari ameniambia mashine hizo zilinunuliwa kwa kodi za wananchi, kwa kupitia miradi hii viongozi wa juu wa serikali wamejivunia mabilioni ya pesa tangu miaka 90.

Ameniambia kuwa mashine hizi unufaisha takribani viongozi 72 moja kwa moja akiwemo waziri mmoja aliejiuzuru. Kuna viongozi wa ngazi za chini wenye influence au wenye kujua habari hizi wakiwemo usalama wa taifa upewa mgao kidogo ili kuwanyamazisha, pia utumiwa kwenye kampein za uchaguzi. Aidha wale wasiopewa mgao ndio vinara wa kutoa nyaraka za siri na kuwapa wapinzani.

Jamaa anasema, baada ya kugundulika kuwa Richmond haina mmiliki pale ambapo Mwakyembe alipokuta Marekani hakuna Kampuni inayoitwa Richmond , viongozi wa juu walimfuata mwanaume mwenye asili ya Asia wakampa milioni 800 ili ajifanye kuwa yeye ndie mmiliki wa Richmond, lakini huyo mmiliki alikataa kabisa kupigwa picha alipokuja nchini, alihofia sura yake ingeonekana ingekuwa ni hatari sana nchini kwake. Aliefanya mchakato mzima wa kutafuta mmiliki fake wa Richmond ambayo kwa sasa ni Symbion ni Rostam aziz. Mpaka sasa Symbion inadai deni lenye utata la zaidi ya dola milioni 100, wakati ukifika zitalipwa

Mtonyaji anasema, ili kupata njia rahisi ya kukwapua pesa za IPTL, viongozi walizua kesi fake ili kupitia wakili fake waweze kulipana hizo pesa. Wakili aliechaguliwa ni Mkono. Mkono amepewa jumla ya bilioni 60 na kitu kwa ajili ya kesi, fedha hii ni nyingi sana, lakini kutoka kwenye fedha hizo yeye alikuwa anachukua kiasi na baadhi anawapa wakubwa serikalini. Inasemekana mgao wa fedha za makampuni haya ni mkubwa sana kiasi kwamba wengi wamehamua kufungua account nje ya nchi hasa kwa kutumia majina ya watoto wao, majina yanatumika ni yale ya kikabila/kinyumbani kiasi kwamba uwezi kuwatambua kirahisi.

Kwa hiyo wadau; IPTL na Symbion, Dowans ni changa la macho, zinamilikiwa na viongozi serikalini. Kuna document nazisubiri, nitazitupia hapa

Sipendi nipuuze post yako hii.

Lakini naamini umetumia hisia zako tu kusema hayo. Umeiremba kama Liwaya.

Katika kutaka kutuaminisha,umeamua kutumia "inviting trick" ya kutumia huyo usalama wa Taifa. Post yako inawezakuwa yakichochezi au ikaleta elimu.

Umeongea uongo kadhaa humo. mfano kwa N.MKONO. Unapaswa kufahamu kuwa,yeye na kampuni yake wako independent kabisa. na mkataba wao ulipovunjwa,ndipo (inasemekana) alipenyezesha baadhi ya habari kwa kina Kafulia (just as a revenge of a contract break-down).

Naweza kuichalenji pakubwa post yako hiyo. Ila,naomba niwaachie wenzangu nao "WACHANGANYE NA ZAKWAO" tuone!

NAWASILISHA.
 
Ukweli ni kwamba IPTL na Richmond ambayo kwa sasa ni Symbion zinamilikiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa serikali.
Kwa hiyo wadau; IPTL na Symbion, Dowans ni changa la macho, zinamilikiwa na viongozi serikalini. Kuna document nazisubiri, nitazitupia hapa
Mkuu Nkobe, asante kwa hili, maadam umetuahidi documentary evidence, mimi ni miongoni mwa kina Tomaso, hivyo nasubiria hizo documents!.

Pasco
 
Hii imekaa kishakunaku haina nyama kabisa mtoto yeyote aweza tengeneza stori kama hii ya kuungaunga.
 
Mkuu Nkobe, asante kwa hili, maadam umetuahidi documentary evidence, mimi ni miongoni mwa kina Tomaso, hivyo nasubiria hizo documents!.

Pasco

Pasco kwa serikali yetu yote yawezekana.Kwa Symbion siwezi nena kitu,ila kwa IPTL kwa 100% yaweza kuwa kweli.Maana Seth aweza akawa ametumiwa tu na waheshimiwa kama kivuli lakini kuna wenywe wapo nyuma.

Jiulize utanunuaje hisa bila kutoa pesa,unapata mshiko ambao siyo wako ndiyo unanunua hisa?Hivi dukani wananunuaje kitu au vitu?

JR alilalamika Mahakamani,kuhusu kutolipwa pesa za mauziano ya HISA,HISA za JR zililipwa baada ya ESCROW A/C kupachuliwa,je hiyo siyo tu moja ya hint kwamba shares za IPTL zina hadithi ndefu zaidi ya tujuavyo.

Kwa silimiakubwa naweza nikamuaminimtoa hoja hasa upande wa IPTL na RICHMOND,siwezi kuisemea SYMBION
 
Mmmetazama shares za SYMBION last week?

Hapa kuna Ukwepaji mkubwa wa Kodi tena inashangaza Bunge hawakuwahi kulijadili hili, kuna Pesa nyingi imepotea hapa huku Serikali ikilipa Dola milion 100 nazo hazikukatwa Kodi, hata Rostam ameuza shea zake Vodacom kwa Dola milion 300 hakulipa Kodi,Mkono amekuwa akilipwa Mapesa mengi kwa miaka nenda ludi na Serikali lakini halipi Kodi na hata akilipa halipi kodi Stahiki kama ilivyo kwa mwenzake Mengi wa ipp , Nchi hii kuna Vioja vingi wale wenye kupaza sauti nao pia si watu Saafi, Mfano huyo Mengi ametuia Pesa nyingi sana kuwapa Kafulila,Sendeka , Zito na wenzao ili wamung'oe Mhongo na yeye apate mwanya wa kujipatia Vitalu vya Gesi kisha apige Udalali,hivi kwa nini Mengi hatumii hizo pesa kuboresha Masilahi ya wafanyakazi wake ambao wanalia njaa? au ni kwa nini hatumii hizo Pesa kujenga maabala na kununua Madawa hospital awasaidie wagonjwa ambapo ingempa Promo na kuwasahaulisha watu juu ya Fitana zake za kuwang'oa watu kwa Masilahi yake binafsi kisha kuwashirikisha wanachi kusaka Huruma zao.
 
Kweli nimeamini IPTL wanaonewa

kama wakumulikwa ni hawa na sio IPTL
hao jamaa walikua kwa kazi maalum na wameifanya, hinks alikua arusha. recently na kuna movement ya uwekezaji ya
kwa africa under CCA

its late kupindua, all we need ni kusimamia good governance, itawashinda hata wao... kagame keshaonyesha njia
 
Nchi hii hakuna aliye Msaafi kiasi cha kumnyooshea mwenzake Kidole, kila Kiongozi ana kasoro zake, Mapungufu yake na wengi wanamiliki Mali kinyume na Vipato vyao Harisi,hata Wafanyabiasha wakubwa wengi hawalipi Kodi hata wachache wanaolipa hawalipi Kodi Stahiki, Wakiletwa FBI hapa Tz wawachunguze Viongozi wote kuanzia vyama vya Siasa wa Taasisi za Dini Wafanyabiasha wakubwa nk hakuna ambaye atapona nina Uhakika wote watakwenda jela. Nchi hii imelaaniwa inafaa itafutwe njia ya kuondokana na Laana hii Kisha tuje na Mbinu kama za China yaani Mtu akibainika kaiba mali ya Umma ananyongwa.
 
Kuingia hawa maana yake tusubiri majungu tu dhidi ya kampuni yoyote local kuzalisha umeme.
Na tanesco nao maisha watanunua umeme kwao . Ukijaribu wapo kina zito watatumiwa kuharibu mipango.
Hao ndio mafia wa umeme hasubutu mtu kuja Tz kuzalisha umeme wa rahisi mamluki watatumiwa kuvuruga kila kitu.
 
Nimesoma kila kitu Hasira inaniwaka ndani kwa ndani,
Hebu tuwe patient kidogo tujionee, meanwhile wenye nchi tuchakarike soon tutai handle wenyewe pasipo wazawa wa neanderthals kuhusika, huenda ikawa sivyo tudhanivyo.
 
Ninajua sijajua jambo muhimu. Ninajua sijajua jambo ambalo Mwenyezi Mungu ... ameipangia Nchi yangu Tanzania kupitia utajiri Mzito wa Rasilimali zake ... Najua kuna jambo hapa. Ninajua silijui jambo hilo ..

Eee Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania Ifikie utambuzi dhahiri wa Jambo Hilo.
 
kwa maana nyingine escrow ni vita ya hawa na wale wa ndani kumbe kafulila kazi yake ndogo
 
Back
Top Bottom