Swissport (Dar & Arusha) Imejaa Rushwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swissport (Dar & Arusha) Imejaa Rushwa!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Pdidy, Nov 27, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana JF, kwanza napenda kumpongeza ndugu yangu Temu kwa jinsi anavyozidi kuliimarisha shirika la Swissport.

  Pili nina machache, nakuomba kaka kama una nia na umedhamiria kuibadilisha kampuni yako jaribu kufanya yafuatayo:

  Mosi:

  Rekebisha tabia za hawa wafanyakazi wako hapo wanapoangalia abiria kwanza ya kuondoka, nimesikitika sana jana tu imejirudia tena hali iliontokea mwezi uliopita, nikiwa nimeongeza kilo 4 tu, dada mmoja akaamua kuningangania kwa kuniomba doler 20, nilimwambia kama umeshindwa kunisaidia naomba tu nipunguze mzigo mpaka alipokuja dada mmoja wa airline husika akaamua kumwambia msamehe na ndipo alipoona aibu.

  Pili
  Wawe wasafi kimaumbile wakumbuke pale kila abiria wanapita sehemu tofauti, pia kukiwa na harufu mbaya wanashindwa kuelewa uhali halisi wa kampuni yako,najua si wote jaribu kuwafunza baadhi...wajue jinsi ya kuwa na customer service....

  TATU:
  Waache rushwa, imefika sasa kila mfanyakazi anaonekana yuko pale kwa ajili ya kuomba abiria pesa mzigo unaozidi, sidhani hilo ndilo jukumu lao ila kama unawalipa mshahara mdogo tunakuomba uwalipe mshahara unaostahili kuliko kuaibisha kampuni yako.

  NNE:
  Wawe na heshima mbele ya abiria,kumekuwa na mambo kadhaa na nikiwa kama msafiri ninaepensa kampuni hii, naomba wajitahidi kujua jinsi ya kuishi na abiria na si kuanza kushikana shikana wanaume kwa wanawake mbele ya abiria kweli ni binadamu wanahitaji mambo hayo ila nahisi kuna sehemu husika za kufanya mambo hayo.

  Tano:
  Jaribu kujali wafanyakazi wako ndugu yangu na kaka yangu,,nilijarib kumuuliza yule binti na kujua sababbu za kuishi vile alilalamika sana mshahara mdogo, maisha magumu, hakuna haja ya kuwaumiza wale watoto pale chini,okoa vizazi vichanga kwa kuwalipa sawa na pato unalopata kama umedhamiria kuijulisha dunia umuhimu wa Swissport!

  Sita:
  Hili suala wala sisemi, hata nikiwa kule Kilimanjaro ninajua mchezo wanaofanyiwa watu kupata ajira, kama ni hivyo rekebisha hilo swala maana nina uhakika wa wafanyakazi wako wengi walio na vyeo vikubwa wakiwa na div 4 ama 0 kabisa na majuzi nilisoma kijana mmoja pale Cargo alishtukiwa na div 0 yake ikawa ni aibu tupu kwa kampuni mtu amekaa miaka 6 superv..hapana rekebisha ajira zako mkuu.

  Mwisho nawatakia kila la kheri
   
  Last edited by a moderator: Nov 27, 2008
 2. 1taifa

  1taifa Member

  #2
  Jun 18, 2017
  Joined: May 31, 2013
  Messages: 74
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 15

  UNATAKA WALE WAPI ZAIDI YA WEWE MTEJA??

  KUFA KUFAANA.
   
Loading...