Mbelwa Germano
JF-Expert Member
- May 7, 2011
- 789
- 0
Mwezi septemba mwaka huu nilipata fursa ya kuzungumza na moja ya mtu maarufu ndani ya CDM kuhusu mambo mbalimbali ya kisiasa na kijamii na moja ya maneno yake yaliyonikosha sana The man is loyal na muumini mkubwa wa maneno ya Mao, No research, no right to speak akimzungumzia Dr.Slaa.
Kwa bahati nzuri maneno haya No research No right to speak yawekuwa ni ngao imara kwa CDM na mwiba mkali kwa CCM wakati wa kujibu mapigo. Japokuwa suala la ufisadi wa mabilioni ya uswisi ni suala la kitaifa, kwa upande wa pili naamini Kamanda Zitto kwa nafasi yake anapaza sauti ya upinzani katika kusimamia rasilimali za Taifa na kuongeza uwajibikaji kwa serikali iliopo madarakani (japokuwa kwa kiasi kikubwa ipo usingizini) kwa kuzingatia hoja zenye utafiti wa kutosheleza.
Binafsi naamini Zitto vilevile ni muumini mzuri wa maneno haya, No research No right to speak. Kama angetaja majina ya watu walioficha fedha Uswisi kwa kuwa alikiri kuwa na ushahidi wa kutosha kutoka wa wachunguzi wake binafsi ingekuwa jambo bora zaidi. Kutoa sababu kwamba kutaja majina ya watu hawa ni kigezo cha kuzuia uchunguzi dhidi yao ni kigezo dhaifu.
Kwa kuwa Zitto anakinga ya kibunge na sauti kubwa ya watanzania na alikuwa na ushahidi wa kutosha kuhusu suala hili, kwa mtazamo wangu ingekuwa jambo la maana kama angetaja majina ya wahusika kupitia hoja yake binafsi kwenye mkutano wa bunge uliopita. Hii ingekuwa fursa nzuri kwa wananchi kupima uwajibikaji wa serikali yao na kuipa adhabu/sifa stahili muda utakapofika.
Kutotaja majina ni njia ya watu hao kujihami kwa kutumia nyenzo za kisheria kwa ushirikiano na wale ambao tunaamini watatupa ushirikiano.
Hebu fikiri suala la Rada tumesubiri rehema za waingereza, je hili la uswiss tunasuburi ukweli wa serikali? Tusubiri tuone.
Kama nimepotoka Great Thinkers watanirekebisha.
Nawakilisha.