Swedi Mwinyi aokoa studio za TBC Taifa kuungua kwa moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swedi Mwinyi aokoa studio za TBC Taifa kuungua kwa moto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ADELADIUS, Jul 9, 2011.

 1. A

  ADELADIUS Member

  #1
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Swedi Mwinyi aokoa studio za TBC Taifa kuungua kwa moto
  ADELADIUS MAKWENGATBC!
  1338 EAT

  Kama ilivyo kawaida ya siku ya jumamosi ni siku ya mapumziko huku baadhi ya taasisi kama vile hospitali, polisi, Jeshi , Vituo vya redio, Magazeti na Televisheni ni jambo la kawaida kwa watendaji wake kufika kazini na kutekeleza majukumu yao ndivyo ilivyokuwa siku ya Jumamosi ya Julai 9, 2011majira ya mchana hapa TBC 1.Nilifika ofisini saa 3 na dakika 19 na nilifanya shughuli zangu za hapa na pale na nilipoingia chumba kimoja ambacho ni ofisi ya makarani nilikutana na Swedi Mwinyi akifuatalia Shughuli za Uhuru wa Sudani ya Kusini huku akipitia magazeti ya siku husika na Makarani hao .Nilimsalimu kaka huyo ambaye ni miongoni mwa Watangazaji wenye mvuto na wa muda mrefu nchini petu na kuendelea na kazi. Huku kila mmoja akifanya majukumu yake. Ghafla nilisikia ukelele wa moshi mkubwa ukiwa angani.Ah nini tena ! moto moto moto!(Kelele za watu), nilitoka nje na kwenda kwenye kiwambaza na kuangalia chini nikaona gari dogo aina ya TOYOTA ikiteketea kwa moto ambao kwa hakika ulikuwa unakaribia kuingia kwenye ofisi za Redio ya Taifa amabapo ndani yake alikuwa Mtangazaji vipindi Emmanuel Pajera huku akiwa hajui kipi kinaendelea pale nje.Watu walishuka toka kwa mwendo kasi bila ya kujali mlinzi,polisi au Mtangazaji wa tulielekea kwenye moto huo.Swedi Mwinyi akiwa nyuma yetu alitoka na mitungi wa kuzimia moto mkononi akieelekea huko ambapo alifika kwenye eneo la tukio na kuanza kuzima moto huo huku watu wakianza kujaa kuja kuokoa jahazi kwa ushirikiano wa Polisi ."Njoo na mchanga! Leta maji, aha maji siyo wewe.. ah huyu vipi leta mchanga(kelele zilisikia huku na kule) ah leta maji Swedi…" Wadau walikuwapo ndani ya nyumba hilo walipiga kelele.Kwa hakika moto huo ulizimwa huku Emamanuel Pajera nayeye aliyekuwa jirani na tukio hilo kutoka salama. Nayeye alianza kushiriki kazi hiyo ya kuokoa uhai wa watu na mali za Shirika letu la Utangazaji.Walikuja wengi na wengi walisaidia hilo lakini kubwa zidi ambalo nililiona ni umuhimu wa wadau wote kujifunza kutumia vifaa vya zima moto kwani kinyume chake vifaa hivyo vinaweza kuwa mzigo tu kama watu walijirani na vifaa hivyo hawajui kutumia vifaaa vya zima mto.Gari hilo dogo aina ya TOYOTA liliweza kushika moto na kuungua lakini hakuna madhara kwa binadamu yeyote aliyekuwapo hapo. Kwa bahati njema Mkurugenzi Mkuu wa TBC 1 Clement Mshana nayeye alifika kwenye eneo la tukio na kuweza kushirika kazi hiyo ambayo chanzo chake ni moto ambao uliwashwa pembeni ya eneo hilo na Vijana wa kampuni ya usafi."Swedi nimevipenda viatu vyako (alikuwa pekupeku akizima moto huo) hongera " alisema Mkurugenzi Mkuu wa TBC 1 Clemence Mshana.(akimtania Swedi Mwinyi)Ah jamani moto ni hatari.
  Kwangu mimi nilikuwa sijui kutumia vifaa hivyo vya zima moto na wezangu wengi , japokuwa mafunzo yake utolewa kila mara. Siku nyingine yakitolewa nitajifunza kwa umakini ili niweze kujiokoa na kuwaokoa wengine punde moto unapotokea.Kwani moto ni hatari, tena hatari sana. Kwa ukweli eneo ambalo TBC 1 ipo pana idhaa zote za TBC 1yaani TBC AM, TBC FM na TBC 1, huku bila kusahau kuwa hapa ndipo makao makuu ya Taasisi hii.

  adeladiusmakwenga@yahoo.com
   
 2. papaa masikini

  papaa masikini Senior Member

  #2
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hata ingeungua,ingekuwa sawa tu,haina faida kwa wananchi bali ccm!!
  Anyway lets me say...poleni sana TBCCM!!
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Jul 9, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Nasikitika kwakua mliwahi kuzima moto huo. . . Sioni faida ya Tbc, TSN,ni matawi ya Ccm na vitengo vya propaganda vya chama cha magamba.. .NAOMBA kwa muumba Tbc na Tsn WAUNGUE NA MOTO WOTE wawe majivu.
   
 4. D

  Derimto JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna kazi gani ya maana mnayofanya na hiyo studio yenu ambayo siku zote mmekuwa mnawapofusha watanzania wasio na elimu huku tukiwalipa kwa kodi zetu na bado kama haitaungua basi iko siku itapigwa hata na radi au tetemeko almradi tu mungu atawalipa kwa ukandamizaji wenu tumewachoka
   
 5. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 4,000
  Trophy Points: 280
  Tatizo inaweza kuungua na kutoa mwanya wa bajeti mpya kutengwa kujenga studio mupya! Sasa usiombe ukaskia makadirio yake mbele ya mafisadi! Lazma wakutandike penalt ewe mlipa kodi!
   
 6. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kumbuka kuna ndugu zako pale sio mitambo ya ccm peke yake kama unavyodhani.
   
 7. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  mamayangu!kwa nini aijaungua kabisa.siipendi namna ilivyo bias
   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Na supose "MAMAYAKO" ni mwajiriwa wa hili li taasis!!!!!
   
 9. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Inaitwa TBC au Redio Tanzania??
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,525
  Trophy Points: 280
  Asante, namkubali sana huyu mtangazaji Swedi Mwinyi. Namfahamu ni Jah people na karateker sikujua kuwa pia ni shujaa wa fire drill.
   
 11. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  aaargh nilidhani story itaishia na majivu, IUNGUE TUU kodi zetu zinanufaisha CCM bila sie kupenda.
   
 12. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Nimepita tu mara baada ya kusoma jina swedi mwinyi otherwise story hii mimi hainihusu
   
 13. Paul Kijoka

  Paul Kijoka JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  • Angalau Tido alikuwa mzuri 30% wasliobakia ni 0%. Hii TBC ningefurahi kama ingeungua na watangzaji wake ila tu Comedy original ambayo niko naburudika nayo sasa hivi
   
 14. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lakini ingeungua tungekosa Zilipendwa maana pale pana maktaba yenye nyimbo za zamani.
   
 15. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,204
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Big up swedi mwinyi.lakn jueni kua mnafanya mauaji ya halaiki kwa kuviza na kuwapofusha watanzania.mnasema ni chombo cha umma,umma upi huo?umma wa wana CCM?Ukweli na uhakika upi huo mnao uhubiri?kwenu nyeupe ni nyeusi na nyekundu ni njano.kodi za watanzania mnazokula ztawalaani milele na milele.
   
 16. Officer2009

  Officer2009 JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  TBC - Another Magamba propaganda tool for deceiving the masses. Let it burn to ashes!
   
 17. MAYOO

  MAYOO JF-Expert Member

  #17
  Jul 9, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Nadhani ujumbe mmeuona enyi Tbc watz wamewachoka, hadi wanawaombea muungue?! Shame on you people, angalieni kuna siku mtapigwa na radi.
   
 18. A

  Alakara Armamasitai Verified User

  #18
  Jul 9, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 415
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli huwa sipendi kushabikiya mauaji ya binadamu wenzangu ila kwa hali hii ya TBC kufanya nyeusi kuwa nyekundu na nyekundu kuwa nyeusi hivyo imefika wakati tuwachane laif kuwa hatuoni faida ya hiyo mnayoita tbc mtaendeleya kuwa didimiza watanzaniya mpaka lini? nasema bora ingeunguwa kwani imebaki mtaji kwa ccm na kuendeleya kuwapofusha watanzania nasema ipo siku mtaungua tumewachoka msipojirekebisha mtaona ipo siku tu
   
 19. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ahaaaaa ndugu hata kama ni vitu vya vyenyewe vinaendeshwa kimagamba kaa ukijua hivyo ni mali ya umma sawa mkuu..hongera zako s mwinyi.....
   
 20. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #20
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kweli nimeamini wa bongo hatupendani baada ya kupeana pole si tunaona bora watu wafe..
  Praaaaaaaaaaaaaaah..
   
Loading...