beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa Sh196 bilioni kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa awamu ya Pili ya Mpango wa Elimu kwa Matokeo unaohusu elimu ya Msingi (EP4R II).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 5,2021 na kitengo cha mawasiliano cha Wizara ya Fedha na Mipango, Maktaba huo umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Emmanuel Tutuba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Anders Sjoberg kwa niaba ya Serikali ya Sweden.
Tutuba amesema msaada huo utasaidia utekelezaji wa mpango huo wa kuboresha elimu ya msingi kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Julai, 2021 hadi Juni mwaka 2026.
Katika kutekeleza Mpango wa Elimu kwa Matokeo wa EP4R uliohusisha pia kuendeleza elimu ya msingi Awamu ya Kwanza, ulioanza mwaka 2014 hadi 2020, Sweden kupitia Shirika lake la Maendeleo SIDA, ilitoa kiasi cha sh208 bilioni.
Tutuba ametaja baadhi ya mafanikio ya utekelezaji wa Awamu ya Kwanza ya Mpango huo kuwa ni ujenzi wa madarasa, 10,409, mabweni 646, nyumba za walimu 91, majengo ya utawala 37, maktaba 49, maabara 29, uzio 3 na visima vya maji katika shule za msingi 16.
Mengine ni ujenzi wa ofisi 155 za udhibiti wa ubora wa shule, ujenzi wa shule mpya 44, ukarabati wa shule kongwe 86, ununuzi wa magari 347 kwa ajili ya halmashauri zote za wilaya, ofisi za wilaya za udhibiti wa ubora wa shule, maafisa elimu wa mikoa, Baraza la Mitihani la Taifa na vyuo.
Kwa upande wake, Balozi wa Sweden nchini Anders Sjoberg amesema kuwa nchi yake inafadhili kwa mara nyingine uboreshaji wa elimu ya msingi ambapo mpango huo umelenga kuwanufaisha wanafunzi milioni 16.
Amebainusha mpango wa awali ulilenga zaidi kuwanufaisha Watoto wa kike lakini mpango huu mpya utawanufaisha wanafunzi wote wakiwemo wenye mahitaji maalum na kuwawezesha kuhitimu masomo yao kwa ajili ya manufaa yao na Taifa kwa ujumla.
Sjoberg amesema kuwa EP4R Awamu ya Kwanza imefanikisha kujenga mifumo imara ya elimu ya msingi kwa kuweka miundombinu mahsusi na maendeleo ya kimkakati itakayoisaidia nchi kuboresha elimu kwa miongo mingi ijayo.
Chanzo: Mwananchi