Swaum yako itapokewa kwa kutekeleza Dhakat Ul fitri

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
15,825
2,000
Tunakaribia kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhwaan na mambo matatu yafuatayo ya muhimu yanayotukabili yanapasa kuzingatiwa ili tukamilishe Swawm zetu ipasavyo na tupate fadhila zake.

1. Zakaatul-Fitwr:

Inaitwa Zakaatul-Fitwr (Zakaah ya Kufuturu au Kufutari) kutokana na kumalizika Swiyaam za Ramadhwaan. Imefaridhiwa mwaka wa pili wa Hijrah katika mwezi wa Ramadhwaan.

i. Hikmah Ya Zakaatul-Fitwr:

Zakaatul-Fitwr ni kwa ajili ya kutakasa Swiyaam za Muislamu kutokana na maneno machafu na ya upuuzi wakati alipokuwa katika Swawm kwa kulisha maskini chakula ili nao wapate chakula kizuri siku ya ‘Iyd. Ndio maana kutolewa kwake kunakuwa kabla ya kuswali Swalaah ya ‘Iydul-Fitwr kwa dalili:

عَنْ ابْنِ عَبَّاس قَالَ فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الْفِطْرِ طُهْرَةً لِلصَّائِمِ مِنْ اللَّغْوِ وَالرَّفَثِ وَطُعْمَةً لِلْمَسَاكِينِ مَنْ أَدَّاهَا قَبْلَ الصَّلاةِ فَهِيَ زَكَاةٌ مَقْبُولَةٌ وَمَنْ أَدَّاهَا بَعْدَ الصَّلاةِ فَهِيَ صَدَقَةٌ مِنْ الصَّدَقَاتِ . " رواه أبو داود بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ .

Kutoka Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefaridhisha Zakaatul-Fitwr kuwa ni takaso kwa mwenye kufunga kutokana na maneno ya upuuzi na machafu, na kulisha masikini. Atakayeitoa kabla ya Swalaah basi hiyo ni Zakaah iliyotakabaliwa, na atakayeitoa baada ya Swalaah basi hiyo ni miongoni mwa swadaqag” [Abuu Daawuwd kwa isnaad iliyo nzuri].

Na ndio kusudio ya kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ ﴿١٤﴾

Hakika amefaulu ambaye amejitakasa.

وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّىٰ ﴿١٥﴾

Na akadhukuru Jina la Rabb wake na akaswali. [Al-A’laa: 14-15]

‘Umar bin ‘Abdil-Aziyz alikuwa akiamrisha watu kutoa Zakatul-Fitwr na huku akisoma Aayah hizo tukufu.ii. Wakati Unaowajibika Kutoa Zakaatul-Fitwr:

Kuanzia Magharibi ya siku ya mwisho ya Ramadhwaan hadi asubuhi kabla ya Swalaah ya ‘Iydul-Fitwr. Inaweza pia kutolewa siku mbili tatu kabla. Mtoto atakayezaliwa siku hiyo kabla ya kuzama jua imewajibika kumtolea Zakaatul-Fitwr.
iii. Anayewajibika Kutoa Zakaatul-Fitwr Na Kitu Gani Cha Kutoa:

عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَال فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الْفِطْرِ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ عَلَى الْعَبْدِ وَالْحُرِّ وَالذَّكَرِ وَالأُنْثَى وَالصَّغِيرِ وَالْكَبِيرِ مِنْ الْمُسْلِمِينَ وَأَمَرَ بِهَا أَنْ تُؤَدَّى قَبْلَ خُرُوجِ النَّاسِ إِلَى الصَّلاةِ . صحيح البخاري

Kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameifanya Zakaatul-Fitwr ni fardhi kwa mtumwa na aliye huru, mwanamume na mwanamke, mdogo na mkubwa miongoni mwa Waislamu kwa kutoa swaa'aa moja ya tende kavu au swaa’aa moja ya shayiri, na akaamrisha kwamba itolewe kabla ya watu kwenda kuswali (Swalaatul-'Iyd)" [Al-Bukhaariy]

Swaa’aa moja = Kilo mbili na robo hadi tatu au (mteko) viganja viwili vya mkono vya mtu wa wastani vilivyojaa mara nne.

iv. Kinachotolewa Ni Chakula Kinachotumika Na Watu Katika Nchi:

عن أبي سَعِيدٍ الْخُدْرِيَّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ "ُكُنَّا نُعْطِيهَا فِي زَمَانِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَاعًا مِنْ طَعَامٍ أو صَاعاً من الشعير أو صاعاً من تَمر أو صاعاً من زَبيب، أو صاعاً من أقِط البخاري

Abuu Sa'iydil-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Tulikuwa tukitoa zama za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) swaa’ moja ya chakula, au swaa’aa ya shayiri au swaa’aa ya tende au swaa’aa ya zabibu au swaa’ ya aqitw" (mtindi mkavu) (ambacho ndicho kilichokuwa chakula chao zama za hizo) [Al-Bukhaariy Na Muslim]

Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,532

Shukrani, kwa ukumbusho mwema.
Mwenyezi Mungu akulipe mema.
 
MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
15,825
2,000
Shukrani, kwa ukumbusho mwema.
Mwenyezi Mungu akulipe mema.
inshallah jazzakal lah kheir
ila maalim ni jambo la muhim sana kulitekeleza kwa maana ndio linaloweza kusaidia swaum yako kupokelewa na mwenyeezi mungu bila kikwazo. na usipotoa zakatlfitr basi utambue kuwa swaum yako itaishia inaelea angani tu haitafika.
inshaallah mola akujaze nguvu na kukupa nia ya kutenda tendo hili tukufu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom