Swali

Masiko W. M.

Member
Mar 9, 2010
41
3
Naomba wana JF mnisaidie, neno sahihi ni lipi?
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA au JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA?
Naomba nipate ufafanuzi wa kila moja
 
Naomba wana JF mnisaidie, neno sahihi ni lipi?
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA au JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA?
Naomba nipate ufafanuzi wa kila moja
Inatamkwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa sababu Tanzania ni Jamhuri mbili au nchi mbili zilizo ungana, ingekuwa ni nchi moja tu peke yake ingetambuliwa kwa kuandikwa hivi: Jamhuri ya Tanzania (Tanganyika).
 
tukisema Jamhuri ya Muungano 'wa' ni lazima tuongeze kiunganishi ''na'' ili twende sawa na kile cha ''wa''
Mfano: Jamhuri ya Muungano 'wa' Tanganyika na Zanzibar

na tukeisema Jamhuri ya Muungano 'ya'
tayari tunakuwa tumetaja neno la nchi mbili zilizoungana yaani Tanzania
mimi naona ''ya'' ndo ingekuwa sahihi kwa vile tunatamka
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
Habari WanaJF?
Napenda kuchukua fursa hii kwa mara ya kwanza katika safu hii ya wanaJF kumuunga mkono Bwana Anyisile Obheli kwa majibu yake mazuri kwa swali la Bwana Masiko W. M.
Unaposema 'Muungano wa' unahitaji kutaja zaidi ya kitu kimoja yaani Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (hivyo huwezi kusema wa Tanzania).
Unaposema 'Jamhuri ya' unazungumza kuhusu umoja na si wingi wa nomino 'Jamhuri' katika ngeli ya N/N (na hapa umoja huo unaletwa na Muungano wa [TAN]ganyk[A] na [ZAN]zb[A]r).
 
Wana JF, nashukuru kwa majibu mazurina yanayotoa changamoto. Kutokana na majibu yaliyotolewa kwa swalilangu, nami nimepata cha kusema baada yakusikia hojazenu. Tukumbuke Tanzania ni zao la nchi mbili, ambazo ziliungana na kuzaa jamhuri YA Tanzania. Pia nchi hizo zilizoungana haziitwi Tanzania bali zilikuwa na majina yake.

Hivyo basi, Tukisema ni JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Tunamaanisha kuwa kuna nchi zilizoungana na kutengeneza Tanzania, lakini pia nchi hizo zilikuwa zikiitwa Tanzania [ MUUNGANO WA TANZANIA] na;

Tukisema jamhuri ya muungano ya Tanzania, tunamaanisha kuwa iko nchi ambayo ni JAMHURI, NCHI HIYO IMETOKANA NA MUUNGANO WA NCHI FURANI, NA NCHI HIYO AMBAYO NI JAMHURI INAITWA TANZANIA [JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA ]
 
Back
Top Bottom