Swali: Walinzi wa wanaovaa sare za SUMA JKT walipe nauli?

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
727
500
Jana nilishuhudia malumbambano kati ya Kondakta na Mlinzi alievaa sare yenye nembo ya SUMA JKT, kuhusu kulipa nauli kwenye Basi, wapo baadhi ya abiria walikuwa wanaunga mkono hoja ya Kondakta kwamba wanapaswa kulipa na wengine wakisema wao wapo chini ya JWTZ.

Kwa wenye kufahamu utaratibu na kanuni zinazotumika kutowatoza nauli Polisi, Magereza, Mwanajeshi, nk atufahamishe kuhusu SUMA JKT!!!
 
chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
13,495
2,000
Ni utaratibu wa wapi huo kwamba hao walioko jeshini wasilipe nauli kwenye public transport?

Kwani huwa wanafanya kazi bure bila mshahara? Yani mfanyabiashara amewekeza analipa kodi ambayo inamlipa mshahara alafu bado akipanda gari la mlipa kodi anataka kupanda bure?

Upumbavu huu nausikiaga tu Tanzania.

Tupo katika mfumo wa ki capitalist, hakuna kula kwa mgongo wa wengine huo ni unyonyaji wa kukemewa kama pepo mchafu.
 
Mnyenz

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
1,154
2,000
Malumbano na zogo kubwa katika basi lileeee,
Kati ya kondakta na bwana mgambo yuleeee,
Kondaktaa anadai nauli yakee eeeeee katika basi lileeee
Mgambo anadai yeye chombo cha dolaaa,
Kondakta kaja juuuuuu, anasema haiwezekaniiiii,
Kupanda bureeee limeruhusiwa jeshi la polisiiiiii.
HAYO NI MASHAIRI KATIKA WIMBO MZURI SANA KUTOKA KWA JAGUAR (MCHIRIKU)

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
busha

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
1,647

Jaguar taifa kubwa..Anaitwa Jacki simela(marehemu)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dogo G

JF-Expert Member
Jul 6, 2018
1,052
1,500
Analipa tuu kwani ye ni askari rasmi?,asiyelipa ni police,mwanajeshi na askari magereza hao wengine walipe tuu hamna tofauti na walinzi wa vilabuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Black BackUp

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
599
500
Suma JKT wanapaswa walipe nauli maana hao si Askali kamili hawajapoga depo za kutosha za kuwafanya wasilipe nauli.
 
EvilSpirit

JF-Expert Member
Jun 15, 2017
4,342
2,000
Inchi hii ya ajabu sana,mtoto analipa nauli,mtu mzima na mshahara wake wa jeshini halipi nauli kisa askari,
 
KOLOKOLONI

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,779
2,000
Jana nilishuhudia malumbambano kati ya Kondakta na Mlinzi alievaa sare yenye nembo ya SUMA JKT, kuhusu kulipa nauli kwenye Basi, wapo baadhi ya abiria walikuwa wanaunga mkono hoja ya Kondakta kwamba wanapaswa kulipa na wengine wakisema wao wapo chini ya JWTZ.

Kwa wenye kufahamu utaratibu na kanuni zinazotumika kutowatoza nauli Polisi, Magereza, Mwanajeshi, nk atufahamishe kuhusu SUMA JKT!!!
Ili ulipwe lazima umfikishe polisi na ukifika hapo unaulizwa tu kuwa huyo ni askari gani .bila shaka utasema suma jkt nini maana yake .Shirika la uzalishaji mali jeshi la kujenga Taifa .Swali nani mkuu wa jkt bila shaka utataja jina lake huyo ni askari au mlinzi wa vilabuni? Jibu utasema wanajeshi .je suma jkt ipo chini ya nani? Chini ya mkuu wa jkt .Sasa unafikiri wanaofanya kazi huko ni maraia? hapana askari .Je wewe umeambiwa uwadai nauli askari hapana.Je unataka nini? Nauli.Nenda kachukue kwa Mabeyo. Nakukumbusha tu kuwa wale wanakuja kuwakagua wale askari malindoni ni macoplo, sargent, na na kwenye malindo nyeti ni maluteni. Sasa wewe dai tu nauli mimi simo huko kitakachomukuta.
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
37,314
2,000
Wale jamaa wanajikutaga wakati wao ni walinzi kama wengine
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
13,988
2,000
Kama watumishi wengine wa serikali wanalipa nauli wao kina Nani wasilipe.. Kazi kuharibu biashara za watu serikali iseme juu ya hili..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom