Swali: Walimu wanahamishiwa shule za msingi watakuwa chini ya afisa elimu wa msingi au sekondari?

othuman dan fodio

JF-Expert Member
Jan 2, 2018
5,578
8,913
Habari wanamember wenzangu, kwa siku za hivi karibuni katika sekta ya elimu kumekuwa na utekelezaji wa agizo la wizara ya elimu/Tamisemi kama sikosei la kuhamisha baadhi ya walimu wa sekondari hasa wale wa masomo ya sanaa (arts) kwenda kufundisha shule ya msingi. sasa swali langu ni hili: hawa walimu watakuwa chini ya nani kati ya hawa, afisaelimu sekondari au afisa elimu msingi? kwawale wenye uelewa tu wasuala hili karibuni tujuzane wewe ambae unajijua hujui chochote kuhusiana na hiki nilichokiandika pita mbali kabisa. Karibuni.
 
Maneno yako makali umebagua watu
Haya jadilini mnaojua zaidi
Ila jifunze kutoa swali
Ww unajua chagua majibu yako ya kweli ambayo hayafai weka kosa
 
Chini ya afisa elimu msingi kwa kuwa utakuwa unatekeleza sera ya elimu msingi na Cyo secondary.ni kawaida mkuu mbona bashite anaongoza mkoa na ndani yake wapo watu wenye elimu kubwa kuliko yeye? (Katibu mkuu mkoa ana elimu kubwa hata afisa elimu mkoa)
 
Wanaopelekwa shule za msingi watakuwa chini ya Afisa Elimu wa Wilaya wa idara ya elimu msingi.
Ingawa katika hili,bado kuna changamoto ipo hasa kama hakutakuwa na ajira ya walimu karibuni.
Hili linatokana na maelekezo ya Sera ya Elimu ya mwaka 2014 ambayo inatuondoa kutoka darasa la saba( miaka saba yaani darasa la I-VII) na kuelekea darasa la sita(miaka sita yaani darasa la I-VI). Hii itasababisha kuwa na makundi mawili ya wahitimu mwaka 2020 ambao ni darasa la sita na saba ambao watajiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021.Hili litasababisha upungufu wa walimu unless ajira ziwe zimetolewa.
 
Na vp kuhusu malipo ya hamisha hamishi hii, je watalipwa stahili zao au ndio nitolee maana naskia wapo walio hamishiwa nje ya kata zao
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom