SWALI; Vijana wengi wa Tanzania wako Chama gani, CCM au CHADEMA?

JF Salaam,
Naomba tujiulize, hivi vijana wengi wa Tanzania wako chama gani kati ya CCM na Chadema??

Unajua mtu wa kiwango chako na unavyopenda kujipambanua hustahili kuuliza maswali hapa kama vile uko baa.

Unauliza vijana wengi ndani ya vyama hivi based of quantitave au qualitative analysis?
 
Unajua mtu wa kiwango chako na ilunavyopenda kujipambanua hustahili kuuliza maswali hapa kama vile uko baa.

Unauliza vijana wengi ndani ya vyama hivi based of quantitave au qualitative analysis?

Ben,
Kuna vigezo vingi sana tunatumia kufanya tafiti ndogo, ikiwa ni pamoja na kuuliza maswali.

Hivi unavijua vigezo vya mtu kuitwa mwanachama wa chama fulani??
 
Vijana wenye fikra pevu, kwa sasa tunaendelea kutafakari chama gani ni sahihi na chenye utashi wa kusimamia masilahi ya watanzania; kwa sasa CDM imepwaya na vijana tumegundua kuwa ni Saccos ya ukoo!
 
weng ni cdm mkuu! Mbona hilo liko waz

Nakupinga.
hakika Vijana wengi wanapenda madiliko na kwa sasa wanasupport CHADEMA kwa kuwa ndio walio jipambanaua na kufanana nawao Vijana.

lakini kikitokea chama kingine kipya kikajipambanua na Vijana, hakika CHADEMA watapoteza japo kama kwa kila chama kinawatu wake.

nacho amini CHADEMA kwa kilipo fikia hata kiki poromoka,hakiwezi fikia level ya CUF au NCCR ilipo sasa kwani CHADEMA inawenyewe.
 
Mkuu una kadi na unashiriki katika shughuli za chama??

ninayo Mkuu, tangu mwaka 2010.

huku Kimanga kumejaa vizimba vya CHADEMA na mimi ndo mmoja wa Makamanda Watiifu waliofanikisha hilo. Juzi tu tumekizinduwa kimoja pale Mtaa wa The Place. sasa tunataka kuzinduwa chengine Mtaa wa Tembomgwaza karibu na Shule ya Msingi Kisukuru.

Karibu tujenge chama, Mkuu.
 
Mi nazani wengi ni ushabiki ukitaka kuamini Tafuta wenye kadi. Bahati mbaya wengi hatuna uelewa mpana wa siasa. Mi nimeshashindwa kuchagua chama bora kwa mtazamo na upeo wangu. Sababu vyote vinafanana na tofauti ni majina na nguvu mwingine ana Dora mwingine mpinzani mkuu mwengine mpinzani mdogo. Ila yanayofanyika kwenye yanapishana ukubwa ila ni yale yale. Nimebaki katika imani ya kuchagua mtu na si chama.
 
Back
Top Bottom