Swali: Tozo mpya za miamala zimeshavuna kiasi gani cha pesa hadi sasa?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,044
40,705
Ikiwa ni Takriban wiki 3 sasa tangu serikali ianze kuvuna kodi mpya iliyopewa jina ya ‘Tozo ya kizalendo’, nimepata shauku ya kujua walau kwa makadirio, serikali imashavuna kiasi gani cha kodi toka kwenye tozo hii mpya?

===============================
Update: Waziri Mwigulu Nchemba kupitia TBC 1 (19/08/2021) amesema kwamba mapatao ya mwezi uliopita yamezidi makusanyo ya miezi mingine yote toka 2017. Swali linabaki, katika hayo makusanyo, Tozo mpya ni trillion ngapi na kodi zingine za siku zote ni kiasi gani? Tunasubiri majibu

================================
Update: 20/08/2021
AD84720D-E66E-4E9D-BF16-C446C3F20CF8.jpeg

==================================
Update: 20/08/2021
Hatimae wamekubali kutoa takwimu
 
Huu si uyoga, upande asubuhi, uvune jioni.

Suburi riport ya TRA ya mwezi August alafu linganisha na ya mwezi uliopita. Ile difference ndio itareflect mavuno ya kodi ya uzalendo.😎
 
Hii tozo kwa mtazamo wangu itavuna trillion moja na ushehe per month.

Hii tunaiita unkwepabo tozo.

Miamala malaki kwa malaki inafanyika Tanzania kila siku, na kila muamala serikali inachukua pesa kotekote bila kuacha VAT toka kwa wamiliki wa mitandao.
 
Huu si uyoga, upande asubuhi, uvune jioni.
Suburi riport ya TRA ya mwezi August alafu linganisha na ya mwezi uliopita. Ile difference ndio itareflect mavuno ya kodi ya uzalendo.😎
Sawa, lakini specific data si zipo kwenye system kiasi inaweza tukaambiwa exactly ni kiasi gani cha kodi kimetokana na tozo mpya, down to the last shilling
 
Hii tozo kwa mtazamo wangu itavuna trillion moja na ushehe per month.
Hii tunaiita unkwepabo tozo.
Miamala malaki kwa malaki inafanyika Tanzania kila siku, na kila muamala serikali inachukua pesa kotekote bila kuacha VAT toka kwa wamiliki wa mitandao.
Daah, tusije tukasikia masuala ya Escrow tu, nchi haitakalika hii. Kwahiyo kwa mwaka inaweza kuwa Trillion 12??! Nusu ya bajeti ya nchi inapatikana sehemu moja tu, hii inakuaje hii
 
Mi hazijavuna hata 100. Nashukuru Mungu tangu zianze sijapata shida ya kutuma hela kwa simu, natumia zaidi bank. Simu nanunulia umeme tu.
 
Jamani tulieni muone Barabara mpya za lami, zahanati na vituo vipya vya afya, madarasa na madawati mapya ya watoto wenu, na maboresho kadhaa wa kadha ya upatikanaji wa huduma nyingi za kijamii kutoka serikalini, hayo ndiyo tuliyotolea ufafanuzi wakati mfumo huu tunauanzisha!
 
Sawa, binafsi pengine na wengine, tunataka kujua, kupitia mfumo huu mpya wa tozo, ni trillion ngapi zimeshakusanywa? Kwani ni siri?!!
 
Wengi wenu hamtuamini na hata tukisema hamtosadiki, waswahili wanasema hata kimya ni jibu! Hii inatuhusu sisi wazalendo tu!
 
Wengi wenu hamtuamini na hata tukisema hamtosadiki, waswahili wanasema hata kimya ni jibu! Hii inatuhusu sisi wazalendo tu!
Kwani Kujibu ni hiari au wajibu? hakuna uhuru wa kukaa kimya kwenye pesa za umma, labda kwa kiburi, ila ni haki ya waliokatwa kujua!
 
Kijana tulia, kuwa mzalendo kwa kusubiri utekelezaji wa tulichofafanua, wapi tuliahidi kutoa hesabu ya kiasi tunachokipata kutokana na tozo hizo za kizalendo?
 
Back
Top Bottom