herzegovina
JF-Expert Member
- Oct 28, 2015
- 3,129
- 4,712
Salaam,
Juzi usiku, wafanyakazi wa TANESCO wakijitambulisha kama maafisa wa jeshi la polisi, walifika nyumbani kwa mwandishi wa habari, Emmanuel Kibiki na kumpekua nje ya muda uliowekwa kisheria na kisha kuondoka naye halafu wakamkabishi polisi baada ya zaidi ya masaa kumi na mbili.
Hapa Mkurugenzi wa TANESCO amevuka mipaka. Amepata wapi mamlaka ya kuwatuma vijana wake kupekua na kukamata bila kulishirikisha jeshi la polisi?
Kama TANESCO wana malalamiko, vyombo vya kutoa haki si vinajulikana? Kwanini hawakwenda kama wamechafuliwa??
Kwa waandishi wa habari, wanaharakati na wadau wa demokrasia, je hakuna haja ya kumfikisha mahakamani huyu Mkurugenzi wa TANESCO ? Jeshi la polisi nalo, je wameridhia TANESCO kuwasaidia kupekua na kukamata??
Kwanini Jeshi la Polisi halijalaani kitendo cha wafanyakazi wa TANESCO kujitambulisha kama maafisa wa polisi?.
Wito kwa wanahabari, ukifuatwa na TANESCO kabla hujafungua ita wenzako. Kama TANESCO watataka kuondoka na wewe basi wenzako wakusindikize hadi kituoni..haya mambo ya TANESCO kukupeleka wanapojua kwanza bila hata polisi kujua ni hatari.
Ni vizuri kuanza na huyu Mkurugenzi
Nawasilisha
Mods nisaidieni kuweka alama ya kuuliza kwenye title