Swali shirikishi: Je ni kwanini Serikali sikivu ya CCM ipo kimya juu ya vitendo vya utekaji na mauaji ya raia?

Kanguyeyejr

Senior Member
Jan 27, 2018
105
91
Amani iwe nanyi, inasikitisha kuona serikali ya awamu ya tano chini ya rais magufuli kunyamazia vitendo vya utekaji na mauaji ya wanasiasa wa upinzani.

Serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ilipaswa kukemea na kuchukua hatua dhidi ya vitendo hivyo. Kinyume chake serikali imekaa kimya huku watu wasio na hatia wakitekwa, kutoweka na wakati mwengine kuuawa kikatili.

Sote in mashahidi kwamba baada ya jaribio la mauaji dhidi ya tundu lissu, ilifuata kutekwa na kupotea kwa mwandishi wa gazeti la mwananchi ndugu Azory mpaka Leo hatujui yuko hai au ameshaliwa na samaki: juzi wametekwa viongozi wa chadema na mmoja wao kauawa kikatili lakini serikali imeamua kuwa kimya.

Nashangaa kiongozi wa wanyonge hajatoka hadharani na kukemea uonevu dhidi ya RAIA wema. Kama MTU anauwezo wa kutumbua majipu ya kila aina anashindwa VP kukomemesha vitendo vya kigaidi vinavyoendelea nchini mwetu na kuchafua taswira ya Tanzania kimataifa.

Najiuliza hivi ni kweli watekaji na wauaji wana nguvu kuliko rais magufuli na serikali sikivu ya ccm? Je ni kweli watu hawa wasiojulikana wana nguvu kuliko waziri mwigulu nchemba? Kiukweli inashangaza sana watu wasiojulikana wanaendelea kutojulikana.

Mwisho namwomba amiri jeshi wetu aingilie kati na atamke neno juu ya unyama huu unaostawi kwa kasi ya 4G.

Mungu tunusuru.
 
Back
Top Bottom