SWALI RAHISI.... labda....

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,398
8,883
Mimi nina swali ambalo nimekuwa nikitaka kuuliza watu humu ktk hii foramu, nalo ni kwamba, hivi ni kwanini ktk kila habari ninyosoma watu wanalalamika tuu kuhusu nchi yetu na watu wetu? Hakuna kitu ambacho mtu wa serikali atafanya bila kutukanwa na kukosolewa sasa mimi ninauliza swali rahisi tuu.. sisi sote ni watz na tz ni nchi yetu sote, na uchungu wa tz ni wa kwetu sote.. sasa ni kwanini hamuelekezei nguvu zenu ktk kubadilisha mambo kule tz kwa maana mnaonekana kuwa mnajua mengi sana badala ya kukaa hapa na kuandika kuhusu mabaya tuu?
sisemi kwamba hakuna mabaya nchini mwetu nafahamu kuwa kuna mambo mengi ambayo hayaendi sawa sasa kama na ninyi mnafahamu hivyo na kweli mnataka kuisaidia nchi yetu kwanini hamfanyi lelote? kwani hakuna kazi rahisi kama kukosoa... kila siku nasoma hivi nasikia vile sasa ni kwa nini hamuendi kubadilisha mambo? Je hamuoni kwamba labda mambo yote mabaya yanayotokea nchini kwa kiwango kikubwa yanasabishwa na kutokuelewa kwa mambo mengi sasa kama ninyi mnafahamu mengi kwa nini hamji kutusaidia na kutuongoza badala ya kulalamika tuu? kwani hivyo ni rahisi kila mtu anaweza kulalamika, lkn mtu mwenye akili hawezi kulamika kama hatoi suluhisho kwani ni kupoteza muda na ndio maana wengi huwa tunapendekeza tuu na sio kulalamika... kama wabunge ni wala rushwa basi njooni mgombee ubunge ili mbadilishe mambo na sisi tutawachagua... msikae tuu kulalamika bila KUTOA SULUHISHO LOLOTE...
kwa kifupi swali langu ndio hilo kama mna uwezo wakuona hayo yote maovu yanafanywa na nchi yetu ambayo siyatetei kwa nini basi msitusaidie? ni kwa nini mnakimbilia kwenda kuishi nchi za watu na kula JASHO LA WATU WENGINE?
kwani hizo nchi zinawapa jeuri ya kututukana sisi huku zimejengwa na wenyewe ambao sio ninyi, kwa maana nyingine ninyi ni maruba kwani mnapenda njia rahisi, mmeona wenzenu wametoa jasho kujenga vya kwao na ndio mnakimbilia huko hamuoni kama huko kula jasho la hao waliojenga hizo nchi.? wamewajengea watu wao na sio ninyi kwa hiyo kama mnajua hivyo njooni basi huku mtueleweshe na sisi tutawasilikiza na kuwakabidhi nchi.....
 
Pole sana kama nawe ni mmoja wapo katika serikali hii ya .......

Mnataka mpewe ushauri na msaidiwe mawazo kivipi?

Kumbuka mshapewa kila aina ya ushauri, mawazo na mbinu mbalimbali, lakini vichwa vyenu vigumu na ubinafsi ndo vinavyofanya mambo kuwa magumu, mnajifikilia nyie na familia zetu

Sio watu wote wanaweza kuja moja kwa moja, wanawakilishwa kila kukicha, Mliambiwa nini na Dr Slaah, mmetekeleza?? Tume ya Mwakyembe imewambia nini? mmetekeleza??
mwanakiji kawashauli vizuri kabisa leo, mtatekeleza ushauri wake?

sasa mnataka nini? tatizo lenu mnapenda sana kujilimbilizia na wizi umewajaa kila mahali.
wewe sasa unatoka nje ya kile ninchokiongolea mimi sijatetea maovu hapa, umemuongelea Slaa sasa huoni kama kuna tofauti kubwa kati ya Slaa na ninyi humu? Slaa ndio watu wanaotakiwa kwamba hakai tuu kulalamika bali anatoa suluhisho na amejitahidi ktk hilo... kuhusu kama amefanikwa au laa hicho nikitu kingine na kipo nje ya kile mimi ninachokiongolea...
ninachoongea mimi ni kwamba badala ya kuona malalamiko tuu kutoka kwenu tunataka matendo kama vile Slaa na Kabwe wana/livyofanya na hii ndio inavyotakiwa, na kila mmoja wenu akiacha tuu kulalamka na kuanza kufanya kile anachotakiwa kufanya kama vile Slaa na Kabwe basi nchi yetu itaweza kwenda mwenendo ambao upo sawa.... kwa hiyo ninachosema mimi hapa ni hivyo nafasi zinatangazwa kila siku za uongozi njooni mpiganie kama Slaa na Kabwe walivyofanya sio lazima muwe wabunge hata kama ni benki au posta au popote pale wizarani serikalini halafu muonyeshe kile mnachoweza manake vinginevyo hapa tunasikia maneno tuu... mara serikali ingefanya hivi mara vile mara hivi njooni basi... na kama msitoe sababu za kusema kwamba hamuwezi kupata nafasi kutokana na upendeleo.. upendeleo upo lkni kama kweli wewe ni mginaji kama Slaa au Kabwe basi utaweza kupata nafasi na kuonyesha umahiri wako... na sio maneno tuu
 
Katiba Katiba KAtiba ,maana ukiangalia KATIBA haimruhusu Mtz anaeishi mauraya kurudi na manjonjo ya ugaibuni .jamaa watamuita fisadi ,na katiba hairuhusu kwa yeye kusikilizwa ,sera zinazokubaliwa ambazo hazitekelezeki ni chama tawala. Sasa hata watu wakirudi kuja kugombea ubunge hawaruhusiki maana wataingia katika kundi la mgombea binafsi ,katiba hairuhusu hilo.
Na kwa kuwa fimbo ya mbali haiuwi nyoka lakini siku hizi mambo yameendelea kuna misaili abazo ndio zinazotumika hakuna haja ya kupeleka jeshi mstari wa mbele hukuhuku tuliko bila ya shaka yeyote misaili zikitumwa huko Tanzania basi zitafika tu ila CCM nao wameweka Patriotic missile kibao ,mara nyingi wanafanikiwa kuzidungua hizi zinazotumwa kutoka majuu ,ila inayofanikiwa kutua inaweza kuwachengua CCM na mara unasikia mmoja ameanguka na wengine wamejiua.
 
Kijakazi, swali lako ni muhimu sana na ambalo limeulizwa hapa kabla. Kwa upande wangu naweza kukujibu ifuatavyo.

a. Suluhisho siyo wote kurundikana nyumbani.
Kutakuwa na Rais Mmoja, kutakuwa na Waziri Mkuu mmoja n.k n.k Hivyo hata wote turudi nyumbani bado katika kufanya maamuzi atakuwepo anayetakiwa kufanya maamuzi kwani si wote tunaweza kufanya maamuzi. Hivyo kurudi kwa watu au kutoa mapendekezo ya nini kifanyike haijalishi mtu yuko wapi kwa kadiri ya kwamba wenye kufanya maamuzi hawataki kufanya maamuzi.

b. Hatukosoi tu bali pia tunatoa mapendekezo ya nini kifanyike; hatusikilizwi.
Sasa ukiangalia humu utaona kuna mapendekezo ya 1001 ya mambo mbalimbali ya nini kifanyike lakini hatusikilizwi. Hivi majuzi katika mada ya "Picha ya maendeleleo) tulionesha jinsi shimo moja la barabarani lilivyozidi kukua. Picha ile niliiweka kwa karibu wiki mbili zilizopita sasa. Na lengo siyo kukosoa tu bali pia kumulika nini kinahitajika. Sasa angalia shimo hilo lilipofikia sasa na hatua zilizochukuliwa kutatua tatizo hilo:

3603.jpg
Sasa hapa tutoe pongezi au pendekezo la namna gani? Hivi turudi kutatua tatizo hili la shimo lililowashinda Watanzania walioko nyumbani?

Hebu angalia na tatizo hili; hivi ni nani atakayerudi nyumbani kutoa pendekezo ya jinsi ya kulitatua, pendekezo ambalo watanzania walioko nyumbani hawakulifikiria?

3623.jpg

c. Hata watumwe Musa na Manabii hawatasikia.
Kama wameshindwa kuwasikia kina Dr. Slaa, Marando, Mvungi, wachungaji na mashehe kibao; kama wameshindwa kusikilizana wenyewe kwa wenyewe ni kitu gani kinakufanya uamini kuwa wakija watu kutoka nje ya nchi watasikilizwa? Hivi unajua ni wangapi kati yao tulikuwa nao huku huku, wamesoma huku, wameishi huku na wameviona vile vile tunavyoviona sisi, lakini waliporudi wakageuka baada ya wimbi la ufisadi kuwapitia au kupigwa ganzi na madaraka?
 
Ndugu yangu kama ndivyo unavyofikri basi hakuna utakachofanikiwa kwani kama kweli wewe ni raia wa tz hakuna kinachokuzuia kurudi nymbni na kutoa mchango ktk nyanja yeyote ile.. kwa hiyo kusema katiba ni kutafuta visingizio ambavyo ndio kitu ninachoongelea kwamba ni rRAHISI KUTOA MAKOSA NA KULALAMIKA lkni ikija ija kwenye utekerezaji ni kitu tofauti kabisa...
naweza nikakupa mfano watu wanalalamika kuhusu mikataba ya madini kwamba hakuna wataalamu wa hilo na wanaandika vizuri kabisa sasa Je ni kitu gani kinachowashinda kurudi nymbani kama kweli wameliona tatizo lilipo na kuja kupigania na kutafuta suluhisho? kwa nini wanakaa kulalamika tuu? njoo uonyeshe ujuzi wako kama kweli unao nafasi utapewa kama ukiipigania... mbona huko ulaya hamtakiwi lkni mnapigania kuishi? sasa kama mnaweza kupigania huko kwa nini pia nguvu hizo msije kuziweka huku na kujaribu kubadilisha mambo? sisi tunawasubiri tupo njia PANDA HATUJUI WAPI TUENDE sasa sio mnaandika tuu kila siku na kutuelezea ni jinsi gani mifumo ya huko mlipo ilivyokuwa mizuri.. sisi hatutaki kujua hilo... kama ni mizuri wameijenga kwa hiyo inawastahili wao pamoja na watoto wao na sio ninyi...kama nilivyosema NJOONI NYUMBANI tuungane woote tubadileshe nchi yetu
 
Mimi nina swali ambalo nimekuwa nikitaka kuuliza watu humu ktk hii foramu, nalo ni kwamba, hivi ni kwanini ktk kila habari ninyosoma watu wanalalamika tuu kuhusu nchi yetu na watu wetu? Hakuna kitu ambacho mtu wa serikali atafanya bila kutukanwa na kukosolewa sasa mimi ninauliza swali rahisi tuu.. sisi sote ni watz na tz ni nchi yetu sote, na uchungu wa tz ni wa kwetu sote.. sasa ni kwanini hamuelekezei nguvu zenu ktk kubadilisha mambo kule tz kwa maana mnaonekana kuwa mnajua mengi sana badala ya kukaa hapa na kuandika kuhusu mabaya tuu?

Swali zuri sana kijakazi,

Sio kweli kwamba watu "wanalalamika" tu kuhusu serikali. Katika forum iliyo diverse kama hii yetu ni vigumu kwa watu wote kuwa na msimamo mmoja. Kama alivyosema General Patton -na tunaye mwanachama mmoja hapa ambaye amekunwa na msemo huu mpaka kuufanya signature yake- ukiona watu wote wanafikiri sawa ujue kuna wengine hawafikiri or something to that effect.

Forum ina watu tofauti wa mitizamo tofauti walio katika sehemu tofauti kuanzia kijiografia mpaka katika phases za maisha. Mathalani kuna wengi tu walio ughaibuni ambao kwao hao njia nyepesi kabisa ya kuchangia vuguvugu la maendeleo nyumbani ni kwa kuja hapa na kutoa mchango wao. Sitaki tujisifu sana na pengine kulitia tembo maji, lakini tumeona hata magazeti yetu ya nyumbani yanakuja hapa kupata muelekeo katika baadhi ya mambo. Kwa hiyo kwa kuchangia hapa mtu anaweza kabisa kuwa anaandikia magazeti nyumbani by proxy na hivyo kuchangia maendeleo.

Siku chache zilizopita nilimsikia Rais Kikwete akitoa wito kama wako kwa kurudia mbiu ya "Afrika haiandikwi vizuri". Yaonekana rais Kikwete ama haelewi vizuri priorities ya "wanahabari" katika ulimwengu wetu au anataka kubadilisha saikolojia ya habari. Saikolojia ya habari inatuambia kuwa mazuri ni ya kawaida, unless yawe distinguished kwa uzuri wake yaani yawe mazuri sana kupita mengine, kwa hiyo Tanzania kama itakuwa nchi yenye inflation ndogo kuliko zote Afrika halafu tusipolisema hilo kama kitu kizuri (depending which economic school of thought you are from and how does it view inflation in a developing nation) hapo unaweza kuwa na case.Hii ni issue ya "mbwa akimng'ata mtu si habari, mtu akimng'ata mbwa ni habari". Vitu vilivyo commonplace kama "Tanzania kuwa nchi salama" haviwezi kufanya habari kubwa, kwa sababu every other country can claim that, and that is how we should be anyway. La kama unataka kuandika kuhusu usalama wa Tanzania basi ni bora usalama huo uwe ule wa watu kulala milango wazi, kitu ambacho hatuwezi kukisema kwa sababu hakipo.

Kwa hiyo kutokana na uzalendo wetu na kusikia tunachomwa na kila senti inayoibiwa, kila appointment mbovu, kila safari isiyo lazima, kila kupindishwa kwa ethics, kila kampuni inayouzwa kiholela na mengine mengi zaidi, tunajisikia ni lazima "tulalamike". Hii haina maana kwamba hakuna mazuri yanayofanyika.

Ukiwa ndani nyumbani kwako halafu una watoto wawili, mmoja anawasha moto na petroli na mwingine anafagia chumba chake, unataka kuniambia utaenda kumpongeza anayefagia chumbani kwake na kumuacha anayewasha moto? Hasha, utamuwahi anayewasha moto ili kuzuia madhara kwanza, yule anayefagia anaweza kusifiwa baada ya moto kuzuiwa, lakini ukitaka kumsifia anayetimiza wajibu wake kwanza (anayefagia) halafu ndiyo uende kumzuia na kumkemea anayewasha moto unaweza kujikuta umekosa kila kitu kutokana na moto.

Sisemi kwamba ili kusifia chochote ni lazima tuumalize ufisadi wote, na ndiyo maana nikasisitiza kuwa tunasifia yanayopaswa kusifiwa hata kama mara nyingine tunafanya hivyo kwa kupingana (mpaka leo hii sikubaliani na GAME THEORY katika criticism yake ya utawala wa Kikwete kuhusu uvamizi wa Anjouan, mimi namuunga mkono Kikwete in principle kwa kutetea charter ya AU kuhusu territorial integrity na ku stand up against that fool Mbeki, GAME THEORY anamlaumu Kikwete kwa kuingiza wanajeshi wa Tanzania katika vita, madai makuu yakiwa kwamba Tanzania imetumia pesa zake -kitu ambacho mimi nasema at best hatuna ushahidi either way-).Kwa hiyo kinachogomba hapa naona ni degree, ni kwa degree gani watu wanalalamika na kwa degree gani watu wanapiga makofi.

Tunatakiwa tuwe na balance somewhere na binafsi nafikiri kuna watu wa kutosha ambao ni watetezi adilifu wa serikali, na kuna wengine ambao hawana msimamo kamili ila hutegemea issue (ambao serikali yenyewe inaelekea kuwakosa zaidi kwa sababu inaboronga kila siku) kwa hiyo kama watu hawaitetei serikali au kuiimbia sifa kama unavyotaka katika forum iliyokuwa balanced kama hii kitu muhimu kabisa cha kujiuliza ni "kwa nini hawa watu wanakuwa hivi?". Huenda serikali haiteteeki!

sisemi kwamba hakuna mabaya nchini mwetu nafahamu kuwa kuna mambo mengi ambayo hayaendi sawa sasa kama na ninyi mnafahamu hivyo na kweli mnataka kuisaidia nchi yetu kwanini hamfanyi lelote? kwani hakuna kazi rahisi kama kukosoa... kila siku nasoma hivi nasikia vile sasa ni kwa nini hamuendi kubadilisha mambo? Je hamuoni kwamba labda mambo yote mabaya yanayotokea nchini kwa kiwango kikubwa yanasabishwa na kutokuelewa kwa mambo mengi sasa kama ninyi mnafahamu mengi kwa nini hamji kutusaidia na kutuongoza badala ya kulalamika tuu?

Kuhusu "kufanya lolote" kama nilivyoeleza hapo juu inawezekana wengine kutokana na ratiba za maisha yao kuandika hapa ndiyo kufanya kwenyewe. Nishaanza kuona pages za jamboforum zinapata high rank katika google searches ukiseach mambo fulani, labda huo ndio mchango wao. Ingawa najua kuna mengi tunaweza kufanya zaidi (kuna maandamano yamesemwa, kuna vijarida vimesemwa, kuna petitions zimesemwa) lakini inabidi kwanza tuelewane tunaendaje, ni bora tuelewane hapa hapa kwenye forum misimamo yetu kabla ya kurukia mambo makubwa na kujikuta kuna nyufa kubwa.Lakini pia kuna watu wanaanzisha network nyumbani, watu wanaandikia magazeti, watu wameanzisha radio za mtandaoni zenye reputation kiasi cha kuweza kuwaita watu wazito tu katika serikali, ukweli tu kwamba hii forum inazungumziwa na kufuatiliwa katika "corridors of power" ni kilelelezo kikubwa kwamba "hatutwangi maji kwenye kinu". Baada ya kusema hayo nataka kusema pia kuwa naelewa challenge uliyotupa na ni challenge nzuri tu, kwamba inabidi tufanye mambo mengi zaidi yaliyo tangible.

kwani hivyo ni rahisi kila mtu anaweza kulalamika, lkn mtu mwenye akili hawezi kulamika kama hatoi suluhisho kwani ni kupoteza muda na ndio maana wengi huwa tunapendekeza tuu na sio kulalamika

Kuhusu kutoa usuluhisho kwa matatizo "tunayolalamikia" naomba nikufunge kwa kamba yako mwenyewe, umetulaumu kwamba tunasema mabaya tu na hatusemi mazuri ya serikali. Na mimi naweza kusema wewe unaona mabaya tu ya forum hii lakini huoni mazuri,not to be defensive lakini inaonekana kama unaona malalamiko tu lakini huoni kina Augustine Moshi, Kithuku, Fundi Mchundo na wengine wengi wanavyokuja hapa na kutoa maada za nguvu. Usiegamie sana kuwasoma watu fulani fulani tu ambao inawezekamna kabisa criticism hii inawafaa, watu ambao ni rahisi sana kuwa "armchair critics" bila kutoa solutions.Angalia forum kiujumla.

... kama wabunge ni wala rushwa basi njooni mgombee ubunge ili mbadilishe mambo na sisi tutawachagua... msikae tuu kulalamika bila KUTOA SULUHISHO LOLOTE...

Sio lazima kila mtu awe mbunge, kila mtu ana "talent" yake.Wengine wafanyabiashara, wengine waandishi wazuri, wengine hata walimu tu wa kuelimisha watu.Kama ningekuwa napata thumni kwa kila suluhisho linalotolewa hapa mbona ningekuwa milionea sasa!

kwa kifupi swali langu ndio hilo kama mna uwezo wakuona hayo yote maovu yanafanywa na nchi yetu ambayo siyatetei kwa nini basi msitusaidie? ni kwa nini mnakimbilia kwenda kuishi nchi za watu na kula JASHO LA WATU WENGINE?

Inaonekana umeamua kuwabagua watu walio nje bila hata ya kuonyesha kuwa watu wote wanaosema bila kufanya wako nje, au mtu kuwa Tanzania tu tayari kashafanya jambo la maana katika vita hii?

Ondoa wazo kwamba mtu mwingine anaweza kukusaidia na labda utaweza kufanya kitu. Hii mentality ya "mtusaidie" ndiyo imeifanya nchi yetu kuwa ya kwanza kwa kupewa misaada Afrika tangu Uhuru lakini hatujaendelea mpaka leo. Hii notion ya kijamaa-jamaa kuwa Watanzania wote wana agenda moja ni sumu kubwa sana, kuna watu wako nje washaonja ubepari wanaona njia pekee ya Tanzania kuendele ni kwa nchi yetu kukubali kuwa na classes na kila mtu ajitete kivyake katika mfumo wa soko huria, sasa ukisema watu hawa "wakusaidie" sielewi una maana gani, naweza kuelewa kama unaongelea vita dhidi ya ufisadi lakini pengine unaongelea habari za kusaidiwa kusoma shule bure au matibabu bure ambao baadhi ya hao unaosema wakusaidie washaona kuwa hazilipi na ndiyo sababu ya nchi yetu kushindwa kuendelea.

Kuhusu watu kuishi kwa jasho la wengine viwanjani nakuhakikishia ni rahisi kwa mtu kufanya hivyo Tanzania kuliko viwanja.Labda kama unaongelea wapuuzi waliojilipua katika systems za welfare ambao mimi sioni kama watu wenye mchango anyway.

kwani hizo nchi zinawapa jeuri ya kututukana sisi huku zimejengwa na wenyewe ambao sio ninyi, kwa maana nyingine ninyi ni maruba kwani mnapenda njia rahisi, mmeona wenzenu wametoa jasho kujenga vya kwao na ndio mnakimbilia huko hamuoni kama huko kula jasho la hao waliojenga hizo nchi.? wamewajengea watu wao na sio ninyi kwa hiyo kama mnajua hivyo njooni basi huku mtueleweshe na sisi tutawasilikiza na kuwakabidhi nchi.....

Sasa hapa unaonyesha diatribe yako inatokea wapi.kwa taarifa tu ni kwamba globalism inayokuja sasa hivi itafanya mambo ya nationalism kuwa irrelevant kichizi, concept nzima ya utaifa kwa vizazi vijavyo itakuwa as parochial as ukabila ulivyo leo.Kama wewe umeshindwa kujichanganya katika the global economy usiwe na kijiba, kubali kuwa kuyatekenya mawingu si zako (huwezi/hutaki etc) na play your part in bongo na waachie wenye kuweza/kutaka wafanye wanachoweza na kutaka, ilmuradi hawavunji sheria tu.Ukiwaandama Watanzania wanaouza madawa ya kulevya nitakuelewa, lakini kuna watu wanafanya kazi zao halali na kufanya mambo ya maana nyumbani kama kusaidia familia, kusomesha watu, kujenga halafu wewe unaleta mambo ya idealism zilizotulostisha miaka yote hii tangu uhuru?

Huyo mchina mwenyewe mwenye mighty power na dynastic lineage za millennia kafungua mipaka yake na raia wake wanaanza kuja west, huyo muhindi mwenye pride na civilization iliyozaa culture zote za Indo-Europian languages anatafuta H1 Visa.

Sembuse sie kina kabwela wa Mkuranga, Ngosha wa Malampaka na Chinga wa Masasi?
 
Kijakazi, swali lako ni muhimu sana na ambalo limeulizwa hapa kabla. Kwa upande wangu naweza kukujibu ifuatavyo.

a. Suluhisho siyo wote kurundikana nyumbani.
Kutakuwa na Rais Mmoja, kutakuwa na Waziri Mkuu mmoja n.k n.k Hivyo hata wote turudi nyumbani bado katika kufanya maamuzi atakuwepo anayetakiwa kufanya maamuzi kwani si wote tunaweza kufanya maamuzi. Hivyo kurudi kwa watu au kutoa mapendekezo ya nini kifanyike haijalishi mtu yuko wapi kwa kadiri ya kwamba wenye kufanya maamuzi hawataki kufanya maamuzi.

b. Hatukosoi tu bali pia tunatoa mapendekezo ya nini kifanyike; hatusikilizwi.
Sasa ukiangalia humu utaona kuna mapendekezo ya 1001 ya mambo mbalimbali ya nini kifanyike lakini hatusikilizwi. Hivi majuzi katika mada ya "Picha ya maendeleleo) tulionesha jinsi shimo moja la barabarani lilivyozidi kukua. Picha ile niliiweka kwa karibu wiki mbili zilizopita sasa. Na lengo siyo kukosoa tu bali pia kumulika nini kinahitajika. Sasa angalia shimo hilo lilipofikia sasa na hatua zilizochukuliwa kutatua tatizo hilo:

3603.jpg
Sasa hapa tutoe pongezi au pendekezo la namna gani? Hivi turudi kutatua tatizo hili la shimo lililowashinda Watanzania walioko nyumbani?

Hebu angalia na tatizo hili; hivi ni nani atakayerudi nyumbani kutoa pendekezo ya jinsi ya kulitatua, pendekezo ambalo watanzania walioko nyumbani hawakulifikiria?

3623.jpg

c. Hata watumwe Musa na Manabii hawatasikia.
Kama wameshindwa kuwasikia kina Dr. Slaa, Marando, Mvungi, wachungaji na mashehe kibao; kama wameshindwa kusikilizana wenyewe kwa wenyewe ni kitu gani kinakufanya uamini kuwa wakija watu kutoka nje ya nchi watasikilizwa? Hivi unajua ni wangapi kati yao tulikuwa nao huku huku, wamesoma huku, wameishi huku na wameviona vile vile tunavyoviona sisi, lakini waliporudi wakageuka baada ya wimbi la ufisadi kuwapitia au kupigwa ganzi na madaraka?

sasa mimi napenda nikuulize swali kama unaona kama hausikilzwi kama ulivyosema, na hawabadiliki Je ni sahihi kusema kwamba umekata tamaa? na kama ni hivyo Je kuna ulazima wa hata kuandika hoja kama unajua kabisa kwamba hausikilizwi?
Pili mimi napenda kupingana na wewe ktk kitu kingine kusema kwamba hakuna mabadiliko SI kweli kwani waliyoyafanikisha akina Bw Slaa na Kabwe ni makubwa sana kama unaelewa ni wapi tunatoka ktk nchi yetu....
ni hivi majuzi tuu Mkapa alizomewa kuwa fisadi, mbunge wa kahama alifungiwa na wananchi Je kama kweli wewe umekulia Tz kuna mtz yeyote ambaye angethubutu kufanya hata tuu kufikiria vitendo kama hivyo.....

kuna viongozi wameshutumiwa na uhalifu na matokeo yake tumeyaona wamejiuzulu nyadhifa.. sasa unaweza kuuliza Je hiii inatosha kwa mtu ambaye ameiba mabilioni? La hasha! lkni ni mwanzo narudia tena nagalia tunapotoka
miaka 20 iliyopita ni nani angweza kwenda bungeni na kumshtumu kiongozi wa serikali kwa uahalifu na kusababisha huyo kiongozi kujiuzulu? lkni sasa hivi kimetokea kwa kusema kwamba hakuna kitu ambacho Kabwe au Slaa wamefanikisha ni DHAMBI kubwa kwani unakuwa hautendei haki hawa watu waliojitolea ktk kulikomboa taifa letu na tunahitaji wengi zaidi....

Kuhusu hizo picha za mashimo ya barabarani ni kweli na kitu ambacho mimi ninachokiongelea kama mnaona kuna huo upungufu sasa Je ni kwa nini msije kupambana na kujaribu kuudhibiti, kama ni uongozi wa jiji basi njooni mombe kazi halmshauri ya jiji au wizarani halafu mjaribu kulitatua hilo?
kwani mimi naamini hivyo ndi jinsi nchi zinavyoendelea... huko ulaya mliko MSIFIKIRI KUWA WAO HAWANA MATATIZO wanayomengi lkni hawayakimbiii bali wanayakabili kwa hiyo narudia tena kama mnaweza kupambana huko ktk nchi za kigeni ambazo hamjashiriki ktk lolote ktk kuzijenga kwa nini msiwekeze nguvu hizo huku nymbani kam vile Bw Slaa na Kabwe badala ya kukosoa kila siku.....
 
Kijakazi,
Mkuu sasa umekuwa wewe mwenye kulalamika tuuuuu!..
Maelezo aliyolkupa Pundit kama ningekuwa wewe ningeshiba kabisa kwani ulouliza lilikuwa swali na umepatiwa jibu lakini ajabu baada ya jibu sasa wewe ndio umekuwa mlalamikaji kutafuta Mwanakijiji kaandika kitu gani ambacho hukubaliani nacho...
Sababu zozote utakazo nipa sasa hivi ndizo sababu zinazojenga hoja zetu humu ndani kwa serikali yetu ambayo kwa bahati mbaya hakuna watu kama Pundit wenye majibu yanayoridhisha..
Hivyo sifa zote ulizozitoa kuhusiana na kina Zitto na Dr. Slaa nadhani ungeanza kwa kuishuru JF na malalamiko yake kwa sababu ndiyo chimbuko la hoja za hawa waheshimiwa zilipotoka.

Hapa JF kuna mazuri ambayo yamesifiwa kwa kuleta mageuzi baada ya malalamiko unayoyasema, na mengine pia yana sifa zake pamoja na kwamba hayakuleta/hayaleti mageuzi haraka lakini yameweza kuonyesha upeo mkubwa wa wananchi ktk kutazama wigo zima la maendeleo kwa taifa letu. hakluna malalamiko yoyote humu ndani ambayo hayaendani na sheria ama tumaduini zetu isipokuwa tunakemea upotoshaji wowote wa sheria na tamaduni hizo, jambo ambali nadhani linajenga zaidi ya kubomoa tatizo ni kwamba walioko upande wa pili wanachokiona na USIKU mtupu, haya malalamiko yanawakera zaidi kwa sababu yanaingiliana na Ufisadi wao.
Hiki ni KIJIWE, uwanja wa mapambano ambapo hapendwi mtu isipokuwa NCHI YETU, hivyo hakuna mtu anayerusha madongo kuhusu nchi yetu, tunaelekeza mapambano kwa hao wanaotaka kuharibu jina la MAMA yetu Tanzania.
 
kijakazi inaonyesha hujui impact ya kuandika na kulalama hapa JF!
hapa unapopaita watu wamekaa tu na kulalama, hutembelewa na wasiasa, waandishi wa habari na hata viongozi wa serikalini.
hapa ni sehemu ambayo imejaa mawazo ya matatizo yetu watanzania, na nini cha kufanya kutatua matatizo hayo. kwa mwenye akili, huja hapa na kujichotea mapendekezo ayapendayo na kwenda kuyafanyia kazi, na wengi wa wale unaowatetea (serikali) hukosa akili ya kuyachukua mapendekezo na kuyafanyia kazi na kusema JF ni sehemu ya upinzani na watu wanalalama bure
 
Back
Top Bottom