Swali Pagawishi: Lowassa Angemuunga Mkono 2015 Tungekuwa Tunazungumzia Serikali ya CHADEMA/UKAWA?

kati ya CHADEMA na CCM nani alikuwa wakwanza kumuita Lowassa fisadi kama sio ccm wenyewe Chadema walikuwa wanafanya lobbying wakati huo kuigawanya nguvu yenu ccm na muda wote huo mbona hakufukuzwa chamani mpaka alioamua kujiunga na Chadema
Unauliza au unaeleza? Mbona hueleweki?
 
Jifunze kwanza kuandika kwa Kiswahili rahisi tu. Kwa jinsi ulivyoandika ovyo unadhihirisha elimu yako ndogo sana na una kila dalili za ulofa!
Nyani haoni kundule...!!sijakataa kuwa na elimu ndogo lakini lilokubwa hapa ni hoja ilioko mezani wala sio kejeli na hasira unazoonyesha hakuna mahali umejibu nilicho kuuliza,sasa basi tujipime mimi na wewe katika kiwango cha ulofa nani zaidi
 
Ndio maana CHADEMA hawaaminiki na hawataaminika tena. Ni hao hao walisema LOWASSA fisadi kwa miaka 8. Mara wanageuka kusema ni malaika! Ebo! Nani atawapa Nchi ndumakuwili wasio na msimamo?
Just thinking aloud,vipi yule aliyegawa nyumba za serikali kwa watu hata wasiohusika,aliyevunja kituo cha mafuta na tukalipa,aliyekuwemo kwenye awamu mbili ndani ya cabinet huku akishuhudia madudu na leo ndiye Masiah wetu????
 
Eti "THE BIGGEST POLITICAL CON IN OUR HISTORY " hahahaha, mwanakijiji hii kiboko!
 
Joseph Stalin say, “…the people who cast the votes decide nothing. The people who count the votes decide everything.”
 
Asiye mwaminifu kwa machache awezi kuwa mwaminifu katika mengi. Mtu viapo viwili vimemshinda(cha upadri na cha ndoa) tena akishindwa hata cha kuwa mwaminifu kwa chama chake, angewezaje kuwa mwaminifu kwa kiapo cha urais? Uwezekano mkubwa angesaliti taifa kutokana na historia yake ya kukosa uaminifu kwa kila afanyacho.
 
Asiye mwaminifu kwa machache awezi kuwa mwaminifu katika mengi. Mtu viapo viwili vimemshinda(cha upadri na cha ndoa) tena akishindwa hata cha kuwa mwaminifu kwa chama chake, angewezaje kuwa mwaminifu kwa kiapo cha urais? Uwezekano mkubwa angesaliti taifa kutokana na historia yake ya kukosa uaminifu kwa kila afanyacho.
Huko shuleni siku hizi Kiswahili naona hakifundishwi vizuri siyo? "ata" ndio nini?
 
Kitu kingine ambacho ndio ukweli ni kuwa Lowassa alipata kura Nyingi sana kuliko kura za wabunge wa upinzani. Hii ina maana kuwa sehemu Nyingi watu walikua tayari kumpa kura ya uraisi Lowassa na ubunge wakampa CCM.

Angalia kura za Lowassa na Magufuri. Lowassa kura zake zilivuka nusu ya kura za Magufuri yaani kura zaidi ya 6m lkn ukichukua kura za wabunge wote wa upinzani hazivuki 4m wakati kura za Magufuli ni zaidi ya 8m lkn pia kura za wabunge wa CCM zilifika 8m.

Kwa hiyo picha tunayopata ni kuwa Lowassa alikua na mvuto mkubwa zaidi kuliko ukawa kwa ujumla, na ndio tunahitimisha kwa kusema kuwa Lowassa aliibeba ukawa kuliko ukawa ilivyombeba Lowassa
 
Ahaaa! Kuna hoja gani uligusia wewe? Unajihesabu kama unachangia chochote? Ridiculous!!
mchezo huu hautaki hasira,ukija JF relax usichokijua utakijua,ujinga ujinga na utoto kama wako huo pia huwa unaisha jifunze kuongea kwa heshima unapokuwa kuwa mbele ya wanaume
 
Tatizo ni tume huru ya uchaguzi...!! Hata chadema wamulete malaika agombee ni ngumu kushinda Wala haiwezekani kabisa.. lakn ccm hata waweke jiwe litapita tu
Tatizo Mwanakijiji anataka kutuaminisha kuwa CCM huwa wanashinda kuhalali!!

Ila nakubaliana naye kuwa CDM walibugu sana kukubali kumsimamisha Lowasa. Pamoja na kuwa wangeshindwa chini ya Silaa (zengwe la CCM) lakini naamini nguvu yao ya kisiasa ingekuwa bado kubwa kuliko ilivyo sasa!!
 
Ndugu zangu, nawahakikishia kama Lowassa angekuja alivyokuja lakini angesema amekuja kumuunga mkono Dr. Slaa katika kugombea Urais leo tungekuwa tunazungumzia mambo mengine kabisa... combination ya Lowassa, Slaa, Mbowe na inawezekana hata Zitto angemuunga mkono Slaa.. CCM wangetegemea zaidi kura zao wenyewe kuliko za wasio wana CCM

Wacha hizo CCM wangeshinda tu uchaguzi kwani wamebobea katika wizi wa kura na kulazimisha ushindi.(Zanzibar).

Hebu jikite kwenye kuileta katiba ya Warioba, Ikishindikana basi pigania japo tume huru ya uchaguzi. Sasa hivi naona na wewe umeanza kulia lia sijui umekata tamaa na unayemuunga mkono?
 
Back
Top Bottom