Swali Pagawishi: Lowassa Angemuunga Mkono 2015 Tungekuwa Tunazungumzia Serikali ya CHADEMA/UKAWA?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,944
2,000
CHADEMA walitapelewa sana 2015 - unaweza kuita ni utapeli wa juu kabisa wa kisiasa kuwahi kutokea nchini (the biggest political con in our history); hesabu zao ilikuwa ni kwamba Lowassa angekuja na watu wengi sana na hivyo itawapa uwezo wa kushinda hata mbinu chafu. Jinsi ya watetezi wa ujio wa Lowassa walivyoona wakati ule ni kuwa "Dr. Slaa hachaguliki" lakini Lowassa "anakubalika sana". Hawakuwahi kujiliza Lowassa anakubalika na nani na kwanini.

Na ushahidi unaonesha ni kweli Lowassa alikuja na "kura" nyingi zake kuliko kuja na watu wengi kumfuata hadharani. Walichosahau ni kuwa hawakutegemea kuwa baadhi ya watu wao wenyewe wangewakimbia hasa baada ya move ya Slaa kuondoka.

Ni rahisi kuona kuwa kuna uwezekano mkubwa sana watu waliokuwa wamfuata Lowassa "aliko waweko" wengi hawakutegemea kuwa angeenda CHADEMA. Wakati makundi ya vijana yalikuwa tayari kumfuata huko kuna ushahidi mkubwa makundi ya watu wazima na wazee wenye hekima hawakuwa tayari kufanya hivyo hata kama walikuwa tayari "kumpigia kura". Kitendo cha kukosekana watu wengi mashuhuri walioimba "tuna imani na Lowassa" kwenda kumfuata CHADEMA lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa matumaini ya Lowassa ndani ya CHADEMA.

Ndugu zangu, nawahakikishia kama Lowassa angekuja alivyokuja lakini angesema amekuja kumuunga mkono Dr. Slaa katika kugombea Urais leo tungekuwa tunazungumzia mambo mengine kabisa... combination ya Lowassa, Slaa, Mbowe na inawezekana hata Zitto angemuunga mkono Slaa.. CCM wangetegemea zaidi kura zao wenyewe kuliko za wasio wana CCM.

Badala yake, kura za CCM zilimeguka kwenda na Lowassa CHADEMA na wakati huo huo kura za CHADEMA zikamegekuka kwa watu waliomkimbia Lowassa. Hili unaweza kuona kwenye baadhi ya matokeo ya Ubunge ambapo watu walikuwa tayari kumpa kura Mbunge wa CHADEMA lakini kwenye Urais wakampa Magufuli!

Alichofanya Magufuli kiukweli kabisa ni kujiuza yeye mwenyewe na siyo chama chake. Matokeo yake alivuta kura nyingi kwake yeye binafsi na hakuvuta kura nyingi kwa chama chake. Takwimu za uchaguzi zinaonesha wazi trend hii.

Kuelekea 2020 Zitto atakuwa eligible to run. CUF maskini ndio sijui tena maana sioni kupitia CUF nani mwingine baada ya Lipumba na Maalim kuvurugana. Lowassa hata akiamua kugombea tena sidhani kama itakuwa rahisi kivile tena na hasa katika mahali ambapo lile dubwasha a.k.a UKAWA limegeuka UKIWA wa IKAWA halipo tena.

Kwenye uchaguzi ambapo ndani atakuwepo Lowassa, Magufuli, Zitto (je Zitto anaweza kuungana na Lowassa kama Lowassa na Juma Duni Haji?) au mgombea wa chama chake kuna uwezekano kweli wa kuwa na matokeo tofauti?

Ni katika mazingira ya kumsimamisha nani katika upinzani kusimama dhidi ya Magufuli kutokea upinzani?

Lowassa
Lissu
Zitto
Nape (wakitoka/tolewa CCM)
Muhongo (akitoka/tolewa CCM)
Januari (akitoka CCM)

Au tuanze kuzungumzia siasa za 2025? na hii 2020 watu wasalimu amri bila hata kunyanyua mikono kujaribu?
 
Mbalinga

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
1,665
2,000
Mzee hata kama Lowasa angemuunga mkono Dr Slaa wasingeweza "maarifa" ya ccm ya Ushindi. Tungerudi kuendelea kulaumiana tu. Kwa Tanzania ilivyo sasa ni upuuzi kwenda kwenye uchaguzi chini ya tume hii ya uchaguzi halafu ukategemea upinzani kushinda, hilo halitakuja litokee.

Kama kuna tume huru kweli kweli hata mimi nikigombea chini ya upinzani naweza kushika nchi. Ukweli ni kuwa watu walishachoka na wanataka mabadiliko, lakini hayatakuja kutokea kama katiba na tume huru ya uchaguzi havijawa in place.

Jamani ili tuiponye nchi hii tusikubali kuingia uchaguzi mkuu bila tume huru. Mimi kama hilo halitafanyika sitakubali kusimama mstari kupiga kura.
 
TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,667
2,000
Hili linchi ni kubwa sana. Kuna sehemu ambazo hazifikiki ccm huwa wanapandikiza vituo hewa. Mfano, kuna vijiji kama nyingwa kata ya kibungo juu, huwezi amini wana diwani wa CHADEMA. Sasa maeneo kama lumba, kienzema, lukenge, dimilo, ng'ooni, kiunza, mrono, na mengineyo yanayofanana utaambiwa kulikuwa na vituo 300 kila kijiji. Sasa ndo utajiuliza hivyo vijiji vina wastani wa watu 700 mpaka 1000 hivyo vituo 300 mpaka kuku walipiga kura!?
 
MAHORO

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
7,598
2,000
Tatizo ni tume huru ya uchaguzi...!! Hata chadema wamulete malaika agombee ni ngumu kushinda Wala haiwezekani kabisa.. lakn ccm hata waweke jiwe litapita tu
 
Msungu inv

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
260
250
Nilimaanisha "angemuunga mkono Dr. Slaa" naomba Mods wanisahihishie hapo juu...

CHADEMA walitapelewa sana 2015 - unaweza kuita ni utapeli wa juu kabisa wa kisiasa kuwahi kutokea nchini (the biggest political con in our history); hesabu zao ilikuwa ni kwamba Lowassa angekuja na watu wengi sana na hivyo itawapa uwezo wa kushinda hata mbinu chafu. Jinsi ya watetezi wa ujio wa Lowassa walivyoona wakati ule ni kuwa "Dr. Slaa hachaguliki" lakini Lowassa "anakubalika sana". Hawakuwahi kujiliza Lowassa anakubalika na nani na kwanini.

Na ushahidi unaonesha ni kweli Lowassa alikuja na "kura" nyingi zake kuliko kuja na watu wengi kumfuata hadharani. Walichosahau ni kuwa hawakutegemea kuwa baadhi ya watu wao wenyewe wangewakimbia hasa baada ya move ya Slaa kuondoka.

Ni rahisi kuona kuwa kuna uwezekano mkubwa sana watu waliokuwa wamfuata Lowassa "aliko waweko" wengi hawakutegemea kuwa angeenda CHADEMA. Wakati makundi ya vijana yalikuwa tayari kumfuata huko kuna ushahidi mkubwa makundi ya watu wazima na wazee wenye hekima hawakuwa tayari kufanya hivyo hata kama walikuwa tayari "kumpigia kura". Kitendo cha kukosekana watu wengi mashuhuri walioimba "tuna imani na Lowassa" kwenda kumfuata CHADEMA lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa matumaini ya Lowassa ndani ya CHADEMA.

Ndugu zangu, nawahakikishia kama Lowassa angekuja alivyokuja lakini angesema amekuja kumuunga mkono Dr. Slaa katika kugombea Urais leo tungekuwa tunazungumzia mambo mengine kabisa... combination ya Lowassa, Slaa, Mbowe na inawezekana hata Zitto angemuunga mkono Slaa.. CCM wangetegemea zaidi kura zao wenyewe kuliko za wasio wana CCM.

Badala yake, kura za CCM zilimeguka kwenda na Lowassa CHADEMA na wakati huo huo kura za CHADEMA zikamegekuka kwa watu waliomkimbia Lowassa. Hili unaweza kuona kwenye baadhi ya matokeo ya Ubunge ambapo watu walikuwa tayari kumpa kura Mbunge wa CHADEMA lakini kwenye Urais wakampa Magufuli!

Alichofanya Magufuli kiukweli kabisa ni kujiuza yeye mwenyewe na siyo chama chake. Matokeo yake alivuta kura nyingi kwake yeye binafsi na hakuvuta kura nyingi kwa chama chake. Takwimu za uchaguzi zinaonesha wazi trend hii.

Kuelekea 2020 Zitto atakuwa eligible to run. CUF maskini ndio sijui tena maana sioni kupitia CUF nani mwingine baada ya Lipumba na Maalim kuvurugana. Lowassa hata akiamua kugombea tena sidhani kama itakuwa rahisi kivile tena na hasa katika mahali ambapo lile dubwasha a.k.a UKAWA limegeuka UKIWA wa IKAWA halipo tena.

Kwenye uchaguzi ambapo ndani atakuwepo Lowassa, Magufuli, Zitto (je Zitto anaweza kuungana na Lowassa kama Lowassa na Juma Duni Haji?) au mgombea wa chama chake kuna uwezekano kweli wa kuwa na matokeo tofauti?

Ni katika mazingira ya kumsimamisha nani katika upinzani kusimama dhidi ya Magufuli kutokea upinzani?

Lowassa
Lissu
Zitto
Nape (wakitoka/tolewa CCM)
Muhongo (akitoka/tolewa CCM)
Januari (akitoka CCM)

Au tuanze kuzungumzia siasa za 2025? na hii 2020 watu wasalimu amri bila hata kunyanyua mikono kujaribu?
Lakini usisahau kuwa dr slaa kuungwa mkono na lowasa kungemnyima slaa agenda mama.
 
Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
13,891
2,000
Najua watakuja kwa jazba.. Na yule mtia hofu mkuu wa Taifa Tundu Lisu yeye pekee ndio anajiona mpinzani
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,520
2,000
Ya ngoswe mpe Ngoswe, ya CDM waachie CDM.

EL alipata kura 6mil, na MAGU alipata 8mil... unafikiri Slaa angeweza kupata hata 3mil?..

Ukweli lazima usemwe labda uwe huishi Tanzania, upepo wa EL ulikuwa hatari sana kwa CCM na hili analijua JK... EL alikuja na nguvu yake ambayo Slaa hakuwa nayo hapa tusidanganyane hata kidogo, Slaa hakuwa na nguvu yeye kama yeye zaidi yakutegemea nguvu ya chama na kuchoka kwa watanzania.

El pamoja na mambo yake au kashfa zake siasa zake zilitaka kubadirisha upepo wa nchi hii na tushukuru sana upole, uoga na busara za watanzania na hapa vyombo vya usalama visijisifie hata kidogo maana tanzania ingekuwa inafanana watu wake kama wakenya walivyo nafikiri tungezungumza suala lingine leo hapa.
 
Gangongine

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
3,857
2,000
Mzee hata kama Lowasa angemuunga mkono Dr Slaa wasingeweza "maarifa" ya ccm ya Ushindi. Tungerudi kuendelea kulaumiana tu. Kwa Tanzania ilivyo sasa ni upuuzi kwenda kwenye uchaguzi chini ya tume hii ya uchaguzi halafu ukategemea upinzani kushinda, hilo halitakuja litokee. Kama kuna tume huru kweli kweli hata mimi nikigombea chini ya upinzani naweza kushika nchi. Ukweli ni kuwa watu walishachoka na wanataka mabadiliko, lakini hayatakuja kutokea kama katiba na tume huru ya uchaguzi havijawa in place.
Jamani ili tuiponye nchi hii tusikubali kuingia uchaguzi mkuu bila tume huru. Mimi kama hilo halitafanyika sitakubali kusimama mstari kupiga kura.
Nashindwa kuwaelewa BAVICHA kabisa. Kila siku Tume huru ya Uchaguzi. Hizo 40% na hao wabunge kibao walishindaje wakati Uchaguzi haukuwa Huru? Halafu unadai Chama Tawala kikupe Tume Huru ili iweje? Eti mtu anataka kukunyang'anya mkeo na anajigamba kuwa anaweza kumtunza vizuri kuliko wewe! Anakuja kumshawishi mkeo na ugomvi unapoanza unataka mume akupe silaha ili mapigano yawe sawa!! EBO? ilitokea wapi na Nchi gani?
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
9,990
2,000
Ndugu zangu, nawahakikishia kama Lowassa angekuja alivyokuja lakini angesema amekuja kumuunga mkono Dr. Slaa katika kugombea Urais leo tungekuwa tunazungumzia mambo mengine kabisa... combination ya Lowassa, Slaa, Mbowe na inawezekana hata Zitto angemuunga mkono Slaa.. CCM wangetegemea zaidi kura zao wenyewe kuliko za wasio wana CCM.
Nakuunga mkono kwa 101%!! CCM ingekuwa ndo wao hivi sasa wanaotoka bungeni.
 
Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,401
2,000
chadema walifanya kosa kubwa kumsimamisha lowasa kugombea urais, walitumia garama kubwa sana kujijenga lakini ndani ya sekunde chache wakaharibu taswira yao kwa kubadili gia angani. Anayepinga kuwa Slaa alikuwa kipenzi cha watu apimwe akili, Dr. Slaa alikuwa mtetezi wa kweli wa wnyonge, alipigwa na polisi ktk harakati za kutetea haki na utu wa wanyonge. Kazi aliyofanya Slaa itabaki alama na mhuri ndani ya chadema, leo wanamwita msaliti badala ya kumlaumu Mwenyekiti wao... SHAME TO MBOWE
 
MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,165
2,000
Nilimaanisha "angemuunga mkono Dr. Slaa" naomba Mods wanisahihishie hapo juu...

CHADEMA walitapelewa sana 2015 - unaweza kuita ni utapeli wa juu kabisa wa kisiasa kuwahi kutokea nchini (the biggest political con in our history); hesabu zao ilikuwa ni kwamba Lowassa angekuja na watu wengi sana na hivyo itawapa uwezo wa kushinda hata mbinu chafu. Jinsi ya watetezi wa ujio wa Lowassa walivyoona wakati ule ni kuwa "Dr. Slaa hachaguliki" lakini Lowassa "anakubalika sana". Hawakuwahi kujiliza Lowassa anakubalika na nani na kwanini.

Na ushahidi unaonesha ni kweli Lowassa alikuja na "kura" nyingi zake kuliko kuja na watu wengi kumfuata hadharani. Walichosahau ni kuwa hawakutegemea kuwa baadhi ya watu wao wenyewe wangewakimbia hasa baada ya move ya Slaa kuondoka.

Ni rahisi kuona kuwa kuna uwezekano mkubwa sana watu waliokuwa wamfuata Lowassa "aliko waweko" wengi hawakutegemea kuwa angeenda CHADEMA. Wakati makundi ya vijana yalikuwa tayari kumfuata huko kuna ushahidi mkubwa makundi ya watu wazima na wazee wenye hekima hawakuwa tayari kufanya hivyo hata kama walikuwa tayari "kumpigia kura". Kitendo cha kukosekana watu wengi mashuhuri walioimba "tuna imani na Lowassa" kwenda kumfuata CHADEMA lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa matumaini ya Lowassa ndani ya CHADEMA.

Ndugu zangu, nawahakikishia kama Lowassa angekuja alivyokuja lakini angesema amekuja kumuunga mkono Dr. Slaa katika kugombea Urais leo tungekuwa tunazungumzia mambo mengine kabisa... combination ya Lowassa, Slaa, Mbowe na inawezekana hata Zitto angemuunga mkono Slaa.. CCM wangetegemea zaidi kura zao wenyewe kuliko za wasio wana CCM.

Badala yake, kura za CCM zilimeguka kwenda na Lowassa CHADEMA na wakati huo huo kura za CHADEMA zikamegekuka kwa watu waliomkimbia Lowassa. Hili unaweza kuona kwenye baadhi ya matokeo ya Ubunge ambapo watu walikuwa tayari kumpa kura Mbunge wa CHADEMA lakini kwenye Urais wakampa Magufuli!

Alichofanya Magufuli kiukweli kabisa ni kujiuza yeye mwenyewe na siyo chama chake. Matokeo yake alivuta kura nyingi kwake yeye binafsi na hakuvuta kura nyingi kwa chama chake. Takwimu za uchaguzi zinaonesha wazi trend hii.

Kuelekea 2020 Zitto atakuwa eligible to run. CUF maskini ndio sijui tena maana sioni kupitia CUF nani mwingine baada ya Lipumba na Maalim kuvurugana. Lowassa hata akiamua kugombea tena sidhani kama itakuwa rahisi kivile tena na hasa katika mahali ambapo lile dubwasha a.k.a UKAWA limegeuka UKIWA wa IKAWA halipo tena.

Kwenye uchaguzi ambapo ndani atakuwepo Lowassa, Magufuli, Zitto (je Zitto anaweza kuungana na Lowassa kama Lowassa na Juma Duni Haji?) au mgombea wa chama chake kuna uwezekano kweli wa kuwa na matokeo tofauti?

Ni katika mazingira ya kumsimamisha nani katika upinzani kusimama dhidi ya Magufuli kutokea upinzani?

Lowassa
Lissu
Zitto
Nape (wakitoka/tolewa CCM)
Muhongo (akitoka/tolewa CCM)
Januari (akitoka CCM)

Au tuanze kuzungumzia siasa za 2025? na hii 2020 watu wasalimu amri bila hata kunyanyua mikono kujaribu?
Post mortem, naam!!
Heshima kuu!!
Assumption zako zina uhalisia fulani lakini kuna mahali unapakwepa aidha kwa maksudi au kutokujua.

Umeangalia ujio wa Lowasa ndani ya CDM na kuacha kujishughulisha na taratibu za uchaguzi na mikakati ndani ya CDM.

Tumefahamishwa mara nyingi kuwa katika kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi CM iliajiri consultant tena wa kutoka nje ambao waliwaeleza wazi kuhusu nafasi ya kushinda uchaguzi na wakati wakiwa wamemu earmark Slaa.

Walipewa na ushauri ambao ungeweza kuwasaidia na ambao ndio waliotumia na wa kumpokea Lowasa,kujenga umoja wa vyama (UKAWA) na matokeo yake yalionekana,kura nyingi za U rais na wabunge wengi zaidi kuliko wakati mwingine wowote bila kusahau ongezeko la ruzuku.Kwangu mimi haya ni mafanikio makubwa kwa chama cha upinzani Tanzania.

Wangekubali kuendelea na Slaa ilikuwa kukubali kutangaziwa kushindwa hata kabla ya uchaguzi hasa kisaikolojia.

Kwa sisi tuliopo Tanzania na hasa vijijini ukweli unabaki kuwa CCM itaendelea kushinda kwa miaka mingi ijayo si kwa kuwa ni watekelezaji wazuri wa sera wa sera ila kwa sababu............
 
Gangongine

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
3,857
2,000
chadema walifanya kosa kubwa kumsimamisha lowasa kugombea urais, walitumia garama kubwa sana kujijenga lakini ndani ya sekunde chache wakaharibu taswira yao kwa kubadili gia angani. Anayepinga kuwa Slaa alikuwa kipenzi cha watu apimwe akili, Dr. Slaa alikuwa mtetezi wa kweli wa wnyonge, alipigwa na polisi ktk harakati za kutetea haki na utu wa wanyonge. Kazi aliyofanya Slaa itabaki alama na mhuri ndani ya chadema, leo wanamwita msaliti badala ya kumlaumu Mwenyekiti wao... SHAME TO MBOWE
Huyo Lowassa aliwahi kuandamana lini akapigwa virungu na Polisi? Anaujua uchunguwa CHADEMA yeye? Watu mnakuwa wajinga kuwa kilichompa Lowassa kura nyingi ni mnyukano ndani ya CCM. Subirini 2020 kama atapata angalau 3,000,000!
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
9,990
2,000
Ni katika mazingira ya kumsimamisha nani katika upinzani kusimama dhidi ya Magufuli kutokea upinzani?

Lowassa
Lissu
Zitto
Nape (wakitoka/tolewa CCM)
Muhongo (akitoka/tolewa CCM)
Januari (akitoka CCM)

Au tuanze kuzungumzia siasa za 2025? na hii 2020 watu wasalimu amri bila hata kunyanyua mikono kujaribu?
Kama kuna kosa kubwa watakalofanya CHADEMA hivi sasa ni kuwekeza nguvu nyingi kwa Lowassa!!!! Njia nyepesi ya kumuondoa JPM 2020 ni moja tu! Reconciliation among top opposition leaders hususani Dr. Slaa!

Bado naamini ni Dr. Slaa ndie pekee anayeweza kuwa tishio zaidi kwa JPM kuliko Lowassa... hususani Lowassa huyu wa sasa!!! Hata Mrema wa 1995 (Lowassa wa 2015) hakuwa Mrema yule wa 2000 (Lowassa wa 2020).

Vile vile ni muhimu sana Zitto nae kuwa sehemu ya big opposition block na sio ACT opposition leader.

Unless kama CHADEMA wanaota kuirudisha Tanganyika kwahiyo ni muhimu ku-team up na Seif anayeota kuirejesha Zanzibar yenye mamlaka kamili; kinyume chake, kwa upande wa Tanganyika Zitto ni potential kuliko Maalim Seif!!!

Umuhimu wa Maalim Seif kwa CHADEMA ni mmoja tu!!! Akiweza kushinda Zanzibar basi kuna uwezekano mkubwa ama ikazaliwa Tanganyika ndani ya Muungano baada ya Seif kuijenga Zanzibar yenye mamlaka kamili au si ajabu hata muungano wenyewe ukafilia mbali!!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom