Swali: Ni kwanini urefu wa milima unapimwa kutoka usawa wa Bahari?

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,373
Wakuu,
Tangu tukiwa tunasoma ngazi mbalimbali za elimu kuanzia shule ya msingi,sekondari na kuendelea tumekuwa tukisika urefu wa milima mfano Kilimanjaro ina urefu wa mita 5,895 kutoka usawa wa bahari(above sea level),ndege inapaa futi 30,00 kutoka usawa wa bahari nk.

1.Je ni kwanini urefu huu upimwe kutoka usawa wa bahari na sio usawa wa ardhi tunayoikanyaga?

2.Je huu usawa wa bahari haubadiliki?(constant)miaka yote hata katika kipindi hiki cha global warming ambapo mabarafu huyeyuka na kuongeza kina cha bahari?

3.Kama Kina cha bahari kimebadilika kuna haja ya kupitia upya urefu wa milima kwakua utakua pia umeathirika?

Karibuni kwa ufafanuzi.

sunset-192980__480.jpeg
 
Bahari ni the lowest point , arbitrarily we make it zero level (and this makes sense) and start counting from here. Imagine kama bahari ingelikuwa juu ya mlima Kilimanjaro, nini kingelitokea? Ina maana nchi yote ingelikuwa chini ya bahari na hivyo kufunikwa. Nchi zote ziko juu ya bahari hivyo ni logical bahari kuwa reference point .. (I stand to be corrected)
 
Asante kwa maelezo,vp kuhusu namba 2 na 3
 
Bahari ni the lowest point , arbitrarily we make it zero level (and this makes sense) and start counting from here. Imagine kama bahari ingelikuwa juu ya mlima Kilimanjaro, nini kingelitokea? Ina maana nchi yote ingelikuwa chini ya bahari na hivyo kufunikwa. Nchi zote ziko juu ya bahari hivyo ni logical bahari kuwa reference point .. (I stand to be corrected)
Asante mkuu nimepata shule
 
Asante nimeelewa, na Je sea level ya Pwani ya Hindi iko sawasawa na sea level ya Pwani ya Miami ambayo ni Atlantic Ocean? zote zipo level moja?
No.2 ans 3 together: Urefu Haubadiliki maana kipimo kinaanzia kwenye ufukwe na siyo chini ya bahari ambayo kina may be kinaweza kutofautiana with time. Sidhani kama pwani ya Dar imewahi ku-sink na hivyo kuathiri urefu wa mlima!
 
Swali zuri
Swali la msingi sea level haibadiliki? Maji ya mvua ya msimu mzima hayawezi kubadilisha sea level? Kama inabadilika ni sea level ipi ilitumika kati ya wakati wa mvua na ya kiangazi? Na je bahari nzima ya hindi kwa upande wa Tanzania ina level moja?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom