Swali Ngumu Kwa Vyombo Vya Usalama na Kwa wizara ya Mambo ya Ndani

Tule Mihogo

Member
Dec 15, 2016
34
125
Tangu mwanzoni mwa mwezi September Ndugu Ben Saanane alikomalia sana kuhusu uhalali wa shahada ya uzamivu ya Mhe Mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Ndugu Ben alikoleza madai yake kuhusu elimu ya mkuu kipindi cha uhakiki wa elimu za watumishi wa Umma.
Kwa bahati mbaya sana hakuna kiongozi wa nchi, chama au mwanazuoni yeyote aloweza kuzijibu hoja za Ndg Ben (sitaki kuzitaja hapa yasije yakanikuta)
Dr. Chalali na wenzake wote walishindwa kujibu na wasomi wote walibaki kuporomosha matusi na kutoka nje ya mada.

Kila mtu anakumbuka hoja za Ben kwamba mkuu awe wa kwanza kuhakiki elimu yake kama alivyokuwa wa kwanza kuhakiki silaha yake. Cha kushangaza zoezi la uhakiki liliendelezwa kimya kimya kama vile kuna woga fulani.

Tofauti na mkuu huyo kusemwa na ndg Ben kuhusiana na elimu yake, waziri wa mambo ya ndani nae aliingia kwenye headlines kwamba anatumia jina la mtu na yeye alifeli kabisa STD VII lakini waziri huyu haraka alitoa clarification na kila mtu akaelewa japo kulikuwa na makando kando.

Baada ya Ndg Ben kuendelea na kuisakama elimu ya mkuu, alipokea ujumbe wa vitisho na pengine alipokea jumbe nyingi sana lakini aloiweka hadharani ni hiyo moja tuu.

Tangu kupotea kwa Ben Saanane katika mazingira yasoeleweka zaid ya mwezi sasa, tulishuhudia jambo la ajabu kwenye Facebook page yake pale ambapo maandiko yake yote ya mwezi October yanayohusu elimu ya mkubwa yamefutwa yote. Yote kabisa.

Waliofuta post za ndg Ben katika page yake walisahau kwamba sisi tuliokuwa tunamsubiri sana Ben tulikuwa muda wote tunaingia katika page yake kuangalia kama amepost chochote ili tujue kama yupo hai. Usiku wa manane wakafuta post zote za October. Zote kabisa.

Maswali yangu:
1. Kwa scenario hiyo hapo juu, je kuna uhusiano wowote wa kupotea kwa Ben na kuhoji kwake uhalali wa elimu ya mku?

2. Serikali imefwatilia walioingia kwenye page ya Saanane na kudelete post zake zote za October kuhusu elimu ya mkuu?

3. Serikali imechukua hatua gani kwa namba iliyoandika ujumbe wa vitisho kwa ndugu Ben na leo ujumbe umetimia kweli na Ben hayupo tena?

4. Kuna watu wanawahusisha viongozi wakuu wa CHADEMA especially Mwenyekiti kuhusu kupotea kwa Ben. Je, serikali imechukua hatua yoyote kuwahoji na kuwashikilia wasaidie police katika uchunguzi?
Hapa siongelei kukamatwa kwa Lissu kwa kuwa Lissu alihojiwa kwa sababu ya ujumbe alounukuu kutoka facebook page ya Ben

5. Kwa maana hiyo, hii serikali haipendi kukosolewa na haipendi kama kuna ukakasi katika elimu ya kiongozi usemwe?
Kwa mtizamo wangu kama kiongozi anasingiziwa, anaweza akatokea na kufanya clarification kama Mwigulu na watu tukaridhika sio kuchukua uhai wa mtu.

Nina huzuni. Nina mashaka. Mungu tuepushe na hila za shetani tudumishe undugu wetu na tuijenge Tanzania yetu.

Nawatakiwa mapumziko mema katika msimu huu wa sikukuu.
 

JFK wabongo

JF-Expert Member
Aug 11, 2015
3,755
2,000
Chadema wajibu pia hoja za Dr Slaa. Dr Slaa juzi katoa hoja kadhaa zinazo wa-implicate Chadema kwenye hilo suala. Mbowe alipotakiwa kuzijibu akadai achwe kwanza akale Christmas. Wenye akili tukaongeza kitufe hiki '??'!
 

Batale

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
1,113
2,000
Nakubaliana na wewe mtoa mada. Wakati mwingine nashinda najiuliza hivi mtu akikutuhumu hoja ya elimu kwnn uthithibitishe tu au kukiri tuhuma?, badala ya kuvimba na kumwandama aliyetoa tuhuma.

Ushauri wangu kwa viongozi muwe makini sana na maamzi mazito na magumu myatoapo make yakiwarudi yanachoma wenyewe na hasa wapambe wenu ndio wako tayari hata kutoa roho.

Mh. raisi tuhuma ya mwisho ya Sanane ilikuwa dhidi yako na tokea hapo akapata vitisho na hatimaye kupotea kabisa. Tafadhali nakuomba sana ingilia kati uamru apatikane akiwa hai au la na hatimaye ukweli ujulikane.

Aidha sitaki kuamini tuhuma dhidi yake dhidi yako ndio sababu ya kupotea kwake kwani yaweza kuwa juhudi za wapinzani wako kukuchafua kisiasa.

Lakini pia kwenye mambo yanayokuhusu siku zote uko mwepesi kujibu mfn la mshahara wako ulipiga moja kwa moja simu radioni. Nakuomba sana mkuu amru vikosi vimsake Sanane na wahusika wote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom