Swali: Mwiko kuvunjika chunguni

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
1564971933128.png
Salamu nawasalimu, Amani nawatakia,
Niishikapo kalamu, swali nawaulizia,
Si fumbo la kitalaamu, ni hoja nawapangia,
Umevunjika chunguni, mwiko wangu, mwiko wangu!

Kupika ninavyopika, nikipika vinalika,
Vinalika na kulika, na vidole kulambika,
Mwiko ninaposhika, Vitu vinakorogeka,

Viungo nikiongeza, chumvi na mdalasini,
Na ndimu nikinyunyiza, kolienda na komuni,
Utamu nikikoleza, harufu tamu chunguni,

Sasa nashindwa kupika, mwiko umevunjikia,
Nilipokuwa napika, chunguni kumegukia,
Mwiko wangu wa hakika, mwingine sitamania,

Maana yake ni nini, mwiko kunivunjikia,
Niambieni asilani, mizimu imechukia?
Nichinje mnyama gani, mkosi kufukuzia,

Nawauliza watani, na watani wa watani,
Hili jambo ni la nini, kuvunjikia chunguni,
Kama ni zuri ni nini, niambieni jamani,

Swali nimewauliza, beti zangu nazifunga,
Msiseme nawakwaza, imenibidi kulonga,
Mwenzenu naona kiza, nashindwa tena kusonga,

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Mzee Mwanakijiji fasihi iliyobeba vina hii na kusheheni ufundi wa lugha yenye ladha imeangushwa na kitu kimoja tu.. Picha ya mwiko...
Picha ambayo kimsingi ndio kiambishi cha muktadha wa mada yote ingenoga kama mwiko uliovunjika ungekuwa chunguni... BTW kazi ni nzuri na hongera sana
 
Msogezee chungu cha yale mambo yetu ya drone ya kale kule kwa Majaliwa ili aweze kukiweka kilete uhalisia unaousema
 
Back
Top Bottom