Swali: Mwakyembe anajua zaidi ya Takururu?

wapo ila si waadilifu.kwani unadhani madudu yanayofahamika maeneo mbalimbali hayafahamiki?yanafahamika suala nani msafi na anayeguswa aanze kutupa jiwe?
 
Huyu mwakyembe hajasomea u Takururu.. Ila kaenda bandarini na kukamata watu.. Ina maana wenye professional zao wako wapi?
Mwanangu mtakatifu Ivuga kwa Bongo wizi ni nje nje hapahitajiki ujuzi wa ndani zaidi. Kwanza wengi wasiofaidika na huo wizi wanawajua wezi wote na wako tayari kukutajia. Hivyo ni suala la uzalendo zaidi. Hukusikia eti kesi ya Dowans imekula pesa nyingi kuliko inayodaiwa. Hiki ndicho marehemu Remmy Ongala aliita wizi ndani ya wizi.
 
Saint Ivuga siku hizi profession sio mali kitu, siku ikulu ikiwa mahali patakatifu hutauliza hili swali.

Imeandikwa "kichwa kikioza, huoza mwili mzima"....
 
Last edited by a moderator:

huo ni wizi skwea root
 
Saint Ivuga siku hizi profession sio mali kitu, siku ikulu ikiwa mahali patakatifu hutauliza hili swali.

Imeandikwa "kichwa kikioza, huoza mwili mzima"....

Raisi wangu mpeleke Mwakembe Takukuru badala ya Hosea. Pengine nchi itanusurika.
 
Last edited by a moderator:
Huyu mwakyembe hajasomea u Takururu.. Ila kaenda bandarini na kukamata watu.. Ina maana wenye professional zao wako wapi?
Huitaji kusomea ili kuweza kumkamata mwizi,kama kawakamata mwache awakamate wakajibu mashtaka Polisi,haki ya kukamata si ya Takukuru pekee hata mwananchi wa kawaida unaweza kumkamata mtu ambaye katenda kosa na kumpeleka Polisi.
 
Japokuwa yeye ni mwanasheria hivyo anajua zaidi...lakini sikumwelewe alipoagiza kesi ipelekwe mahakamani haraka ndani ya siku 2...hii ndio zinapelekwa kesi kwa kukurupuka zisizo na ushahidi wa kutosha halafu watuhumiwa wanashinda kirahisi!
 
Bongo hakuna professionalism tumekuwa mavuvuzela wote kuanzia kileleni. Ghorofa zinota ovyo jijini kama uyoga wataalamu wako wapi? Barabara zinajengwa chini ya kiwango wataalamu wako wapi? Mtu anafanyiwa operesheni ya kichwa badala ya mguu! Vigogo wanajenga ufukweni bila woga. Viwanja vya wazi vimeuzwa vyote. Vigogo wanabeba mizigo kwa malori yao reli imekufa! Vitalu vinauzwa kifisadi! MSD na madawa feki! Vifaa feki mitaani! Hukumu zinatolewa kiajabu ajabu! Wizi wa kura! Jamani tukisema uongozi dhaifu tumekosea? Vyuo vikuu vinatoa wataalam feki au? Inauma na inasikitisha mno. Onyesha nji Dr. Mwakyembe wengine bado tunalalia magoro ya Comfy hatujui tutaamka lini.
 
Huyu mwakyembe hajasomea u Takururu.. Ila kaenda bandarini na kukamata watu.. Ina maana wenye professional zao wako wapi?
Hapo kwenye maandishi mekundu unamaanisha Dokta Eddy Hosea ama mwingine?
 
Huyu mwakyembe hajasomea u Takururu.. Ila kaenda bandarini na kukamata watu.. Ina maana wenye professional zao wako wapi?

Hata mimi nimemkamata Police alitaka nimpe rushwa na wala mimi siyo takukuru! Saint umeandika hoja nyepesi sana,hukupaswa kushangaa yeye kufanya hivyo ukizingatia Serikali yetu ilivyo na hao Takukuru unao wasema,sijui labda wamesomea kufumbia macho wahalifu wakubwa! si umesikia habari za Dowans? Rushwa ndani ya rushwa! au Rushwa kipeo cha pili aka rushwa squired
 
Nakuunga mkono Saint Ivuga !
Ni kweli ubadhirifu umefanyika, lakini suala la kujua nani anahusika linahitaji utaalamu wa fani husika, na sio kukurupuka.
Ni mbaya sana inapotokea asiyehusika anaingia kwenye mkumbo kutokana na maamuzi ya kisiasa.
Mwakyembe amekurupuka !!!!!
 
Kweli kakurupuka? this is not about cheap popularity.. hapa kawa spin watu vilivyo. Japo the issue is not small ..still kuna ma papa ambayo hataweza kuyakamata kirahisi kama hivyo vidagaa hapo.
 
napita naenda kunywa chai na mihogo. ila kwakukurupuka Mwakyembe anaongoza subilini.
 
Kuwa na proffessional yako si issue na usidhani kwa kuwa na hiyo proffessional yako unawazidi ambao hawajaisomea. Wapo watu wanawezakuwa wanayajua uliyoyasomea kuliko wewe uliyeyasoma!
 
takukuru wamesha jichokea kama wenzao wa tiss hamna kitu.Taifa linateketea kwa kwenda mbele.wakereketwa wa nchi yao kama Mwakyembe wamebaki wachache sana.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom