Swali: Mliofanikiwa kutumia mifuko mipya, inafaa kwa kubebea mboga yenye majimaji?(nyama au samaki) au unga wa kula?

Kuna mifuko ya nylon ambayo ina kidhi vigezo na masharti ya kisheria na siyo harmful kwa mazingira, itazalishwa mingi kwa sasa
 
IMG_6885.JPG


Biashara in politics
 
Siku zote mabadiliko hayapokelewi positively, ndio maana hata kukubali kuwa bila ccm inawezekana watu wanaona sio kweli.
 
Haya ni mawazo yangu tu. Isije ikawa inatengenezwa kiki special for jiwe, baada ya watu kunyanyasika kwa kufungwa, faini, vipigo vya hapa na pale basi mpenda sifa jiwe ajitokeza na kuondoa marufuku hiyo na kubeba kura za uchaguzi ujao 2020.
Binafsi sijaitumia ila nimefanikiwa kuiona sehemu mbalimbali ikiuzwa kwa wingi sana.
Nilipojaribu kuichunguza kwa makini nilipata walakini kama inaweza kuhifadhi mboga kwa usalama na isiwe na matokeo mabaya kwa mbebaji. Niliona pia kutakuwa kuna tatizo kwa wale wanapima unga wa kula kwa kilo, sioni kama mifuko ile ni rafiki kwa kuhifadhi ili utoke nao dukani hadi nyumbani (mliofanikiwa kuiona nadhani mlijiuliza swali hilo pia) lakini nikajiuliza wamama wanaobeba mchele toka sokoni hadi nyumbani pia kutakuwa kuna hitilafu kidogo kwenye chakula chao.

Mifuko ile ni ya nyuzinyuzi na sio karatasi (japo sijui kama imethibitiswa au ni watu wanatumia fursa).

Kwa haraka haraka nimeona ile inafaa kubebea nguo ukitoka dukani ila si mboga ama chakula cha kupima.(mliotumia nisahihisheni kama nipo tofauti).


Hili swala lisichuliwe kirahisi, linahitaji umakini sana kuendelea kulinda afya za watu na mazingira kiujumla.

Tusijekuwa tunamwita Dulla badala ya Abdalah.
 
Unanaje ule nfuko ukiubebea nyama ama samaki?
Beba sufuria mkuu ukienda kuchukua nyama....

By the way (jokes aside) nyama au samaki zitawekwa kwenye karatasi ngumu then wewe unatia kwa mfuko yako..... Au watakua wanaweka nyama mbichi kwenye foil paper
 
Wale wasafiri wa route ya njombe songea hadi songea masasi wajiandae tu kutapikiwa kwasababu hakuna namna
Ipo mifuko Mbadala Ambayo ni ya paper na ndan yake inatengenezwa na plastics nyepes. Wale wanaosafir kwenda Zanzibar kwa bot za azam wanajuwa
 
Mfuko wowote wa nailoni unaweza kutumika kama kifungashio, hivyo inaweza ikatengenezwa na kuwekwa nembo maalum ya kuashiria kwamba hii ni kwa ajili ya kutapikia tu, hivyo ukikutwa umebebea bidhaa au ipo dukani au gengeni utashikwa na kuchukuliwa hatua, ila ikikutwa ndani ya basi au boti hakuna shida.
Moja ya point kubwa sana kwenye Uzi huu, pia ni fursa.
 
Pia kwabla 1990 Smartphone hazikuwepo, je ndio imaanishe unaweza kuishi tu bila smart kwasababu hiyo.
Mkuu ukipoteza hivyo vitendea kazi vilivyobuniwa kurahisisha maisha ya mwanadamu unaweza kuishi bila shaka. Kama ni mawasiliano utatembea kwa miguu kupeleka habari.
 
Mkuu ukipoteza hivyo vitendea kazi vilivyobuniwa kurahisisha maisha ya mwanadamu unaweza kuishi bila shaka. Kama ni mawasiliano utatembea kwa miguu kupeleka habari.
Nawaajiri watakuja kwako kukupa habari za ajira | unapozungumzia mawasiliano ni broad area don't think small.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom