Mzee Mapenzi
Senior Member
- Jan 9, 2019
- 122
- 439
Binafsi sijaitumia ila nimefanikiwa kuiona sehemu mbalimbali ikiuzwa kwa wingi sana.
Nilipojaribu kuichunguza kwa makini nilipata walakini kama inaweza kuhifadhi mboga kwa usalama na isiwe na matokeo mabaya kwa mbebaji. Niliona pia kutakuwa kuna tatizo kwa wale wanapima unga wa kula kwa kilo, sioni kama mifuko ile ni rafiki kwa kuhifadhi ili utoke nao dukani hadi nyumbani (mliofanikiwa kuiona nadhani mlijiuliza swali hilo pia) lakini nikajiuliza wamama wanaobeba mchele toka sokoni hadi nyumbani pia kutakuwa kuna hitilafu kidogo kwenye chakula chao.
Mifuko ile ni ya nyuzinyuzi na sio karatasi (japo sijui kama imethibitiswa au ni watu wanatumia fursa).
Kwa haraka haraka nimeona ile inafaa kubebea nguo ukitoka dukani ila si mboga ama chakula cha kupima.(mliotumia nisahihisheni kama nipo tofauti).
Hili swala lisichuliwe kirahisi, linahitaji umakini sana kuendelea kulinda afya za watu na mazingira kiujumla.
Tusijekuwa tunamwita Dulla badala ya Abdalah.