SWALI: Mkoa gani Tanzania ni mzuri kwa kuishi?

Karibu Pemba mkuu ni pazuri kuliko unavyofkiria, amani + utuluvu 100%, hewa nzuri kutoka kwenye miti iliyojaa iukijani, hakuna stress za wizi, majambazi, wala wanawake wanaojiuza

Mmmhh, Pemba tena mkuu! Hali ya usafiri ikoje huko?
 
Mkoa wa dodoma
wilaya ya dodoma mjini
kata ya mnadani
eneo la maili mbili

JIJI LA KITOVU CHA ELIMU TANZANIA

KUNA
1. CHUO CHA UDOM
2. ST.JOHN
3. CHUO MIPANGO
4. CBE
5. CHUO CHA MADINI
6. ASSEKI CHUO CHA BIASHARA
7. VETA KANDA YA KATI
9. CAPITAL CHUO CHA UALIMU
10. CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MAKUTUPORA

KUNA
¡ú BUNGE
¡ú KIWANDA CHA NYAMA CHA TAIFA TMC

KUNA
CHAKO NI CHAKO
MNADA MSALATO
MASTER PUB

LOL
KARIBU DODOMA
HOME OF THE BRAVE

Chako ni chako.. Umenikumbusha mbali kweli mkuu!
 
Mkuu sumbawanga,mbeya na katavi iwapo unataka kulima na kufuga uzeeni. Arusha NO, Dar NO,Dom NO, Pemba muungano ukifa umekwisha NO,
 
Ukweli mie naona mkao mzuri kuishi ni morogoro!! Kwanza sio mbali na dar ambako Ndio Tz ilipo pili Hali ya hewa si ya joto Kama dar, bei ya chakula sio ghali Sana na ardhi unaweza kununua kwa bei poa pia!! Sijazaliwa hapo wala kusoma ila nimefanya upembuzi yakinifu! Moro ze best

Mji bora kuishi nami pia ni Morogoro kwa sababu ya flexibility yake kwa kuwa unaweza kuopt uelekee mkoa gani wowote nchini Tanzania. Ama mkoa gani ni bora kuishi dah, mkoa unakua na mji mkuu wa Mkoa na Wilaya n.k. Sasa kwa vigezo vya maeneo na rutuba kaishi popote Mbeya
 
Back
Top Bottom