Swali lolote kuhusu mambo ya upande wa pili (kiroho)

Tembelea thread hii utajifunza kidogo

Rakims
habari yako kiongozi asante kwa kuendela kutupa elimu tusizozijua....
mm naomba niulize kitu kuhusu mimi, zamani nilipokuwa mdogo nilikuwa naokota fedha eneo lile lile kila siku pia nilikuwa na uwezo wa kuchimba shimo na kuweka mawe kisha fukia zen baada ya muda yale mawe yanageuka pesa ( sarafu) but as i grow up nilipoteza kila kitu.
2. pia nilikuwa nauwezo wakuona future event japo sio full event yaani inatokea event afu unahisi kama lilishatokea before
je haya yanaelezeka kwa ufahamu wako??
 
Shikamo wakuu,jaman naomba msaada, know yu nawatu wamejifanyia mke wangu wa Ndoa kuwa mke wao, kilasiku wamfanya na wamemtia mimba,Bado nampenda mkewangu.Naomba msaada jinsi ya kuwavimbisha matumbo hawa watu.. Nimechoka kuvumilia,.
 
Je Majini maruhani mkuu wao ni Lucifer?
Majini ni mjumuisho wa viumbe hivi visivyoonekana na wanyama wao pia, sasa maruhani ni baadhi ya majini tu ambao hujisema wao ni wema na hata ukiwahoji maswali hujisema wao ni wazuri na kama ni waislamu utaskia wanasema mafundisho ya kiislamu na kama ni wakiristo utasikia wanasema mazungumzo ya kikristo,
Unapokuja kwa Lucifer huyu ndio huitwa Ibilis na hujulikana pia kama Dajjal huyu ni mmoja kati ya majini ambaye aliomba kwa Mungu kuwa lau kama akiachwa hadi siku ya hukumu basi atakuwa kapotosha watu wengi lakini Mwenyezi Mungu alimwambia utawapotosha wale wasiokuwa wangu tu,

Huyu ndiye chanzo cha dhambi, sasa kielimu huyu ukisema majini wote wapo kama huyu unakosea

Rakims
 
habari yako kiongozi asante kwa kuendela kutupa elimu tusizozijua....
mm naomba niulize kitu kuhusu mimi, zamani nilipokuwa mdogo nilikuwa naokota fedha eneo lile lile kila siku pia nilikuwa na uwezo wa kuchimba shimo na kuweka mawe kisha fukia zen baada ya muda yale mawe yanageuka pesa ( sarafu) but as i grow up nilipoteza kila kitu.
2. pia nilikuwa nauwezo wakuona future event japo sio full event yaani inatokea event afu unahisi kama lilishatokea before
je haya yanaelezeka kwa ufahamu wako??
Habari mkuu, Ndio haya yalikuwepo yapo na yataendelea kuwepo kwa watu wengine waliojaliwa pia, hapo kuna jambo moja au mawili
Kwanza Mwenyezi Mungu pili majini,

Ikiwa tu ulikuwa karibu na Mungu sana kipindi hicho basi Riziki hii alikuwa akikuruzuku yeye kupitia malaika wake,
Lakini kama ulikuwa kawaida tu basi uliwahi kuwa na Jini wa mali ambaye alikuwa anataka akuzoeshe kidogo kidogo baadae ukikuwa akupe zaidi watu wengi sana walishatokewa na hizi mambo za mfano huu lakini leo wamepoteza sababu ya kupoteza huwa ni mazingira na kuhadithia hovyo hovyo pia kwenye kuota future ni hivyo hivyo, Moja kati ya uwezo nilionao hadi leo ni huo. Kwa nini bado ninao na sijapoteza kama member wengine humu, kwa sababu niliwahi kuhadithia tukio moja tu na likatokea hivyo hivyo niliemuhadithia ndio alinipa Onyo la kutosema hovyo nilikuwa around 9-12yrs old mkuu

Njia pekee ya kurudisha uwezo ulionao ni kila siku ukiamka hesabu 100-0 na ukilala hivyo hivyo bila kuwaza kingine chochote zitaanza kuja kama flashes baadae utakuwa ukilala unaota possibilities na baada ya hapo hali inarudi awali, pia jiweke karibu na imani ya dini yako, zungumza na unayemuabudu akurejeshee uwezo uliokuwa nao awali

Rakims

Rakims
 
Shikamo wakuu,jaman naomba msaada, know yu nawatu wamejifanyia mke wangu wa Ndoa kuwa mke wao, kilasiku wamfanya na wamemtia mimba,Bado nampenda mkewangu.Naomba msaada jinsi ya kuwavimbisha matumbo hawa watu.. Nimechoka kuvumilia,.
Habari mkuu,
Kwanza kabisa pole na tatizo lililokukuta lakini pili fahamu ya kuwa hakuna linalotokea isipokuwa mwenyezi Mungu kakupangia sasa pale ambapo linatokea la kishetani either wewe haukupangiwa na Mungu ukawa umelileta mwenyewe au ulishafanya hivyo sasa umelipwa,
Yote kwa yote linalokuepuka lina heri na wewe, wanawake wapo wengi wazuri kumzidi yeye, kapenda hadi kubeba mimba nje, achana nae muombe mwenyezi Mungu samahani na subiri pamoja na wenye Kusubiri uje kupata wa maana aliyekurudhuku mwenyezi Mungu,

Naweza kukusaidia na kukuelekeza jinsi na kuwatoa vishipa lakini la kheri zaidi kwako ni kukusaidia kuondoa pingu za mapenzi yako kwake,
Ili ukinai

Nb:
Kisasi ni haki lakini kusamehe ni bora zaidi

Rakims
 
Swali;
Meno ya chini mara nyingi ndiyo huanza kuchomoza kwa watoto wachanga walio wengi wanapo kuwa ;
wachache wengine huanza kuchomoza meno ya juu ;

@Je kuna ukweli wowote kiroho au ki-imani kwa wale wanao anza chomoza na meno ya juu ,?

@ Je kuna uhusiana wa ukweli na jambo lolote LA kiroho ,kimaumbile,kinyota au ki-imani ?

Msaada wako tafadhari.
 
salute...
 
Inaaminika kuwa meno ya juu mtoto akianza kuota meno ya juu mtoto huyo hata kaa na mke au mume kwa muda mrefu, ni mkosi na pia humdhohofisha mtoto wengine huamini kuwa yanasababisha mzazi kuto kuzaa kwa muda mrefu,

Hapa kuna scientifical information zinasema kuhusu kuharibu kizazi lakini hayo mengine yapo kimila zaidi na kiimani zaidi ukiamini hivyo itakuwa hivyo

Rakims
 
Mimi pia huota ndoto za shule. Tena secondary Na nilishapita huko miaka karibu kumi. Hua ninaota tumekaribia kufanya mitihani imebaki wiki moja au Mbili lakini Mimi somo LA hesabu Sifaham chochote. Nashikwa Na waswas nakuanza kutafuta namna ya kufundishwa Na wenzangu.

Ni mara moja nilishaota imefika hadi siku ya mtihani nikafanya bila kusoma hio hesabu.paper 1 nikapata 100 nikawa wakwanza paper 2 nikapata 0 nikawa wa mwisho.

Haipiti wiki ninaota tena ni miaka karibu miwili sasa.
 
Sijawai amini ivi vitu, hata ivyo havipo kabisaa na wote wanaoamini Ukiwangalia ni watu ambao wanafanana, ni watu ambao wanaakili moja ambayo ni wepesi sana kukata tamaa katika kila jambo,

Napata shida sana wasomi wanaoamini haya mambo, unakuta mtu anavyeti vyake tena vizuri kabisa lakini haamini kama vinaweza vikampa ajira hadi aende kwa ao watu napenda kuwaita ni mapunguani

Ndugu na jamaa zangu wenye imani izo wananifahamu kabisa, hakuna ulimwengu wa kiroho ni hadhithi tu za rejea

Inaonyesha wewe hujawahi kwenda kwa mganga wa kienyeji,kitu ambacho kinakuweka kwenye nafasi nzuri sana kuja kuelewa mambo huko mebel ya safari kwa sababu hujawahi ku-pollute sana maisha yako ya kiroho. Ila inaonyesha hata Kanisani pia nako huwa hauendi. Kwa maelezo yako mafupi tu nimepata picha kuwa una ulinzi wa Mungu wa hali ya juu sana, kiasi kwamba ukianza kwenda Kanisani, mambo utakayokuja kuyashuhudia utashangaa sana, utajua ya nyuma, yaliyopo na yajayo. Kwa yale ya nyuma, namaanisha kuwa kuna mengi tu tena makubwa yameshawahi kukupita huko nyuma ukayachukulia poa, kumbe hayakuwa hivyo hata kidogo. Hata mimi mwenyewe nilikuwa kama wewe, na mara ya kwanza ku-detect pattern ya kunifanya nishtuke kwamba huwa kuna nguvu nyingine ya ziada inayo-operate katika maisha yetu pasipo mimi mwenyewe kujua, ilikuwa ni juzi tu mwaka 2010. Mwaka uliofuata 2011, nilianza kwenda Kanisani na sasa hivi niko at an advanced stage ya ushirika wangu na Mungu. Ukitaka kujibu maswali yako uliyomuuliza huyu jamaa, anza kwenda Kanisani. Anachojaribu kukueleza yeye kwa kiasi fulani kiko sahihi, halafu wewe ndiye uko completely wrong. Angalau yeye ana usahihi fulani kukuzidi wewe, wewe una sifuri. Nenda Kanisani
 
Mimi pia huota ndoto za shule. Tena secondary Na nilishapita huko miaka karibu kumi. Hua ninaota tumekaribia kufanya mitihani imebaki wiki moja au Mbili lakini Mimi somo LA hesabu Sifaham chochote. Nashikwa Na waswas nakuanza kutafuta namna ya kufundishwa Na wenzangu.

Ni mara moja nilishaota imefika hadi siku ya mtihani nikafanya bila kusoma hio hesabu.paper 1 nikapata 100 nikawa wakwanza paper 2 nikapata 0 nikawa wa mwisho.

Haipiti wiki ninaota tena ni miaka karibu miwili sasa.
Una roho ya kukwama.yaani Mambo yako yanakuwa hayaendi kabisa au yanaenda slow sana
 
Mimi pia huota ndoto za shule. Tena secondary Na nilishapita huko miaka karibu kumi. Hua ninaota tumekaribia kufanya mitihani imebaki wiki moja au Mbili lakini Mimi somo LA hesabu Sifaham chochote. Nashikwa Na waswas nakuanza kutafuta namna ya kufundishwa Na wenzangu.

Ni mara moja nilishaota imefika hadi siku ya mtihani nikafanya bila kusoma hio hesabu.paper 1 nikapata 100 nikawa wakwanza paper 2 nikapata 0 nikawa wa mwisho.

Haipiti wiki ninaota tena ni miaka karibu miwili sasa.
Habari mkuu hilo tukio liligusa sana roho yako jaribu kufuatilia vema kwa karibu utafahamu sababu

Rakims
 
Back
Top Bottom