Swali lolote kuhusu mambo ya upande wa pili (kiroho)

Eleza hapa ksbb na wengine wafaidike,waliobahatika kuiona hii thread. Ile nyingine kujiponya hawakuiona
Mkuu fungua link hii utaziona zote

Mkuu fungua link hii utaziona zote

Asante mkuu. Nifundishe ile kutumai kitu unachokihitaji
 
Mkuu watu kama wewe walikuwepo katika zama na waliuliza swali kama lako sasa ukizungumzia mitume, wote hakuna aliyekuwa tajiri kwa sababu utajili wao wengi waliuteketeza na kuutenga kwa kuhofia kuwa ni mapambo ya dunia ambayo yangeweza kuwateteresha hata nguvu walizopewa hawakutaka kuzitumia kupitiliza kwa kuhofia utiifu wao kwa Mwenyezi mungu aliowapa utume lakini aliyeamua Mwenyezi Mungu kumpa ilisalia kidogo tu amkosee vibaya ambaye ni Mfalme Suleiman Ibn Daud (King Solomon Son Of David)
Ambapo na haya mambo mengi ya interference baina ya wanadamu na viumbe vya kiroho yalizidi,

Mkuu kwenye sinema za watoto (Spiderman) hii pia ilitajwa "with great power comes great responsibility" ukiwa na power hizi utajiri ni kitu cha mwisho kabisa kitakuwa kikigonga kichwa chako

Rakims
Nimekuelewa mkuu.
 
mie nauliza tu mizimu.. kwanini ikutese usipoifuatisha masharti yao. mfano matambiko? na kuna tofauti gani kati ya kutambika mizimu ya upande wa babaa na mama? utajuaje tambiko limeisha? je kuku anatumikaje kutambika? na je ni lazima urudi ulipozaliwa au unaweza kutambika popote pale?
 
Sijawai amini ivi vitu, hata ivyo havipo kabisaa na wote wanaoamini Ukiwangalia ni watu ambao wanafanana, ni watu ambao wanaakili moja ambayo ni wepesi sana kukata tamaa katika kila jambo,

Napata shida sana wasomi wanaoamini haya mambo, unakuta mtu anavyeti vyake tena vizuri kabisa lakini haamini kama vinaweza vikampa ajira hadi aende kwa ao watu napenda kuwaita ni mapunguani

Ndugu na jamaa zangu wenye imani izo wananifahamu kabisa, hakuna ulimwengu wa kiroho ni hadhithi tu za rejea
 
Eleza jinsi ya kushinda katika michezo ya kubahatisha kwa kutumia roho.
Mkuu nilishaeleza hili bonyeza hapa

Rakims
 
mie nauliza tu mizimu.. kwanini ikutese usipoifuatisha masharti yao. mfano matambiko? na kuna tofauti gani kati ya kutambika mizimu ya upande wa babaa na mama? utajuaje tambiko limeisha? je kuku anatumikaje kutambika? na je ni lazima urudi ulipozaliwa au unaweza kutambika popote pale?
Tofauti ya kutambika mizimu ya pande hizo mbili ni makabila ikiwa wote wanakabila moja basi utatakiwa utambike mara moja tu inatosha, na ikiwa una makabila tofauti utabidi utambikie kila moja kivyake na kwa taratibu zake,
Mizimu kumtesa mtu huja pale anapoipa kipaumbele na kutegemea msaada kutoka kwao tu, hapa mtu mwenyezi Mungu anakuwa kamkasirikia kwa maana kategemea mwingine asiyekuwa yeye,
Na ukiogopa hii mizimu ndio inakushurutisha lakini ukiweka hofu kwa mwenyezi Mungu pekee na roho yako ikatakatia kwake basi hautaona usumbufu wowote wa majini haya ya kienyeje(mizimu)

Rakims
 
Sijawai amini ivi vitu, hata ivyo havipo kabisaa na wote wanaoamini Ukiwangalia ni watu ambao wanafanana, ni watu ambao wanaakili moja ambayo ni wepesi sana kukata tamaa katika kila jambo,

Napata shida sana wasomi wanaoamini haya mambo, unakuta mtu anavyeti vyake tena vizuri kabisa lakini haamini kama vinaweza vikampa ajira hadi aende kwa ao watu napenda kuwaita ni mapunguani

Ndugu na jamaa zangu wenye imani izo wananifahamu kabisa, hakuna ulimwengu wa kiroho ni hadhithi tu za rejea
Wazee wenye hekima na umri kukuzidi wewe waliwahi kusema hivi:

Usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Neno liliumba

Ukiona mwenzio ananyolewa zako tia maji

Na misemo mingine zaidi ya hiyo ambapo generation iliyofuata ambayo haina adabu ikasema ni maneno ya kiswahili swahili kutoa maana chanzo chake kilikuwa wapi,

Kitu ninachohitaji kukutaarifu mkuu ni kwamba ukiona mtu anamtihani na unamuona ana tatizo la hivi muombee mwenyezi Mungu amuokoe na aachane na mambo hayo, lakini siyo kumuona hana akili wengi kama wewe waliwahi kusema hivi na wasomi kuliko wewe na ni matajiri kuliko wewe lakini walipokuja kukumbwa na yale waliyoyaona ni upuuzi basi walitafuta msaada kwa kumulika tochi mchana. Jambo lililokuepuka shukuru na waombee msamaha na salama yaliyowakuta usijione unaakili sana kwa kuwa mwenyezi Mungu hajakupa mitihani ya hivyo lakini akikupa ndio utafahamu yapo au hayapo,

Mwisho ninachotaka kukwambia ni kwamba, siku umejikuta kwenye situation kama hizo na unatafuta salama kwa tochi kanisani au misikitini ukumbuke ya kwamba lakini mimi si niliwahi kusema hivi na nafsi yako ikusute

Rakims
 
Sijawai amini ivi vitu, hata ivyo havipo kabisaa na wote wanaoamini Ukiwangalia ni watu ambao wanafanana, ni watu ambao wanaakili moja ambayo ni wepesi sana kukata tamaa katika kila jambo,

Napata shida sana wasomi wanaoamini haya mambo, unakuta mtu anavyeti vyake tena vizuri kabisa lakini haamini kama vinaweza vikampa ajira hadi aende kwa ao watu napenda kuwaita ni mapunguani

Ndugu na jamaa zangu wenye imani izo wananifahamu kabisa, hakuna ulimwengu wa kiroho ni hadhithi tu za rejea
Hahahaah.!! Hahaahaha...hahah..pole sana.sana
 
hebu niambie... kuna watu hawakuwahi kuamini hivi vitu ila kwa maisha wamepata changamoto nyingi sana kurudi kwa wazazi wakawaambia kwamba ni mizimu yao inawasumbua.. kbl ya hapo hawakuwahi kujua kuhusu hbr za majini wala mapepo ya kienyeji..!!

na wengi wa wanaokataa kutambika hiyo mizimu wanaishi kwa tabu maisha yao yote wakilia na kuombewa kila uchao na watu waitwao watumishi wa Mungu. kuna shida gani hapa?? rakims hebu ongea kitu!!!...!
 
Mkuu, kushinda na kushindwa zoteni amri zake mwenyezi mungu na matakwa yake hasa tukirejea katika mafundisho tunayofundishwa ni kwamba,mwenyezi mungu anamjalia na kumpa amtakae vile atakavyo ikiwa kakuumba wewe ili uwe mwema utakuwa mwema hata ufanye uasi kiasi gani lakini pia ikiwa kakuandikia kubaya basi hata ufanye nini ni kazi bure, lakini siri hiyo anayo mwenyewe ya kumuelekeza mtu wapi aende kwa maana yeye anajua alivyo muumba na atakavyo mlipa, yote hayo ni yake kwa amri yake ndio maana tumekaa kusubiri hukumu zetu katika jela hii tuliomo na mwisho wetu basi
KWA HIYO tangu kuzaliwa kwetu,kabla hata ya kuja duniani tukiwa ndani ya mtumbo ya mama zetu Huwa Mungu anakua ameshajua huyu ni wa PEPONI na huyu wa JEHANAMU si ndio maana yake?
 
Je ni kweli.kuwa kuna majini mema na mabaya kama tunavyo aminishwa..
Je ni kweli kuna majini wanaomwabudu MUNGU
 
Je ni kweli kwamba kuna Evil spirit na Good Spirit ? Nipe darasa kidogo Rakim.
Tembelea thread hii mkuu,

Je ni kweli.kuwa kuna majini mema na mabaya kama tunavyo aminishwa..
Je ni kweli kuna majini wanaomwabudu MUNGU
Ndio mkuu wapo kwa dini yako yoyote na vyovyote naweza nikakuprove na ukawaona wazuri na wabaya pia kama utahitaji lakini kiukweli ni kuwa wapo na wapo kama sisi,

Tembelea hapa pia

Rakims
 
hebu niambie... kuna watu hawakuwahi kuamini hivi vitu ila kwa maisha wamepata changamoto nyingi sana kurudi kwa wazazi wakawaambia kwamba ni mizimu yao inawasumbua.. kbl ya hapo hawakuwahi kujua kuhusu hbr za majini wala mapepo ya kienyeji..!!

na wengi wa wanaokataa kutambika hiyo mizimu wanaishi kwa tabu maisha yao yote wakilia na kuombewa kila uchao na watu waitwao watumishi wa Mungu. kuna shida gani hapa?? rakims hebu ongea kitu!!!...!
Shida ilipo ni pale ambapo mtu anachemsha maji kwa barafu yaani unaenda kuomba msaada kwa mtu mwenye matatizo kuliko hata ulivyo wewe mfano wewe unamizimu dhaifu ambayo haikutokei live na kukuongoza kutenda mabaya wapo waliojificha kwenye utumishi wa Mungu hali ya kuwa vivuli vyao ni hayo mamizimu n.k kitu kinachosababisha mtu kuteswa hadi wengine kuharibiwa na hii mizimu ni kukosa power za kucontrol hivi viumbe na kusahau kwamba mwanadamu kapewa mamlaka ya kutawala hii dunia hata humu kwenye social network wapo wengi tu wanapakua habari za watu na kupeleka kwenye sources ningesema kitu hapa lakini nitazua mjadala mkubwa zaidi, elewa ya kwamba hakuna kitu mtu anadhindwa kusolve unless yeye mwenyewe kataka kimshinde au Mungu katika amri yake, pia Mungu anaombwa na kujibu hivyo mengi ni mambo ya kujitakia,
Hujamaliza tiba mkuu lakini,

Rakims
 
Back
Top Bottom