Swali lolote kuhusu mambo ya upande wa pili (kiroho)

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
4,982
4,481
Thread hii nimeandaa mahususi kwa ajili ya kujibu na kutoa maelekezo vile nilivyo jaaliwa kuhusu maisha upande wa pili yaani ulimwengu wa kijini kichawi na kimiujiza, ikiwa una swali lolote kuhusu upande huo basi niulize na wanaofahamu zaidi wataweza kuelekeza kupitia Thread hii ikiwa kuna jambo litakuwa gumu basi tutalijadili kwa pamoja,

images%20(1).jpeg

Kwa haya na mengineyo:
Tembelea:

Rakims
 
Habari wanabodi,

Thread hii nimeandaa mahususi kwa ajili ya kujibu na kutoa maelekezo vile nilivyo jaaliwa kuhusu maisha upande wa pili yaani ulimwengu wa kijini kichawi na kimiujiza, ikiwa una swali lolote kuhusu upande huo basi niulize na wanaofahamu zaidi wataweza kuelekeza kupitia Thread hii ikiwa kuna jambo litakuwa gumu basi tutalijadili kwa pamoja,

View attachment 1080884

Rakims
are demons real? or myth
 
Hesabu ( somo la hesabu ) na somo la Biology... katika ulimwengu wa roho yana maana gani ?
Mkuu swali lako linahitaji maelezo na maelekezo mapana lakini nitalijibu hivi:

Hesabu kwa ulimwengu wa pande ya pili ni kila kitu na jambo linalofanyika na hesabu ni njia ya kupata au kubashiri matukio yaliyopita yaliyopo na yajayo, maana nyingine hayana tofauti na maana za kawaida na vile vile biology.
Jaribu kutanua swali mkuu naweza kulijibu vema zaidi

Rakims
 
Unafikiri ni nini kinamsukuma Mungu kumwacha shetani nyakati zote aendelee na madhara kwa wanae ilihali ana mamlaka hayo?
Katika maandiko matakatifu tuna wito wa kumpinga sheitwan nae atawakimbia.
 
Anamuacha kwa maana kaisha zungumzia kwenye vitabu vyake kuwa huyo kamuumba kama mtihani kwetu ambao anatupima kwake mkuu, kutokana na kuasi kwake
 
Sasa ikatokea jamaa akatushinda nguvu tutawajibika kutumikia adhabu?
Maana kama ni maandalizi ni yeye Mungu aliyetuandaa kushinda. Na je kushindwa ni nani katuandalia?
 
Mkuu swali lako linahitaji maelezo na maelekezo mapana lakini nitalijibu hivi:

Hesabu kwa ulimwengu wa pande ya pili ni kila kitu na jambo linalofanyika na hesabu ni njia ya kupata au kubashiri matukio yaliyopita yaliyopo na yajayo, maana nyingine hayana tofauti na maana za kawaida na vile vile biology.
Jaribu kutanua swali mkuu naweza kulijibu vema zaidi

Rakims

Mtu ameota yupo darasani ana mtihani wa hesabu, na mwingine akaota anajiandaa kufanya mtihani wa biology.. Sio mwanafunzi ni mtu mzima na maisha yake na familia yake, alishaga maliza mambo ya elimu zamani sana
 
Back
Top Bottom