Swali langu kwenu waendesha private car kwenda Mikoani

Ni simple sana Mkuu ukikuwa utajua wala huitaji kuonyeshwa wala kuuliza barabara huwa zinajiongoza ....kwanza kasomee driving utajifunza kila kitu... kwanza ukiona kibao cha 30speed inamaanisha nini ama uko eneo gani na 80speed Ina maana gani
Mkuu yule binti binti bado yupo au alishaolewa?
 
Unakuta mtu anaishi Arusha au anaishi Dodoma then anataka atoke alipo aende mkoa tofauti

Labda tuseme unataka kwenda kigoma,swali langu ni:

Unajuaje njia ya kupita hadi kufika kigoma? au ndio kufata lami moja kwa moja?

Mi najuaga mnafata mabasi kwa nyuma sasa naona itakua haina maana kama utafata bus kwa nyuma,bora upande bus sasa.

Nauliza hivi kwasababu Baba angu ni msafiri sana wa huko mikoani na unakuta kuna mkoa anaenda hajawahi hata kufika.

Nilishaenda nae kipind flani nikahisi labda huko barabarani kuna vibao,ila ajabu ni kwamba sijawahi ona kibao tofauti na vya SPEED LIMIT

ukimuuuliza amejuaje njia,anakujibu kisiasa "ntakwambia ukiwa mkubwa"

Sasa mi naomba kujua nyie waenda mikoani hizo njia mnazijuaje hadi mnafika kabisa mkoa Husika

Maana kuna sehemu unakuta round about halafu njia ziko kama 4 hivi na hazijaandikwa ila mtu hakosei anaingia right way,mnajuaje?

Na ndio mikoa yote sasa nchi nzima,kweli?
Google map, bando lako tu na network access
 
CONTROLA Salaam Mkuu

Hii ni kwako na kwa wengine wote wenye hulka yakutoa funzo au maonyo au maangalizo juu ya jambo fulani.

Mosi msingi mkuu wa kabla kutoa maoni jipe nafasi ya kujifunza jambo husika io itakupa nafasi ya wewe kuwa na uelewa mpana yani kuwa na taarifa zaidi juu ya jambo lenyewe.

Kutoka kwa uzoefu wangu; kuendesha ‘PRIVATE CAR’ kwenda mikoani sio jinai ata siku moja na haitakuja kuwa jinai. Ilimradi akikisha umefata taratibu salama zote za chombo chako (gari yako). Mfano umefanya service zote kwa akika na kujiridhisha gari yako ipo swaaafi kwa safari. Umemwaga oil zote,umecheki breki zote zipo poa, umecheki life span ya tairi zako ipo poa. Kuanzia hapo washa Gari kwa safari.

Sasa io habari ya kwamba unafata bus kwa nyuma ni jambo dogo sana linaloonesha kiasi usivyo na baadhi ya taarifa kichwani mwako.

Safari yako ya mkoani isimamiwe na mambo mawili makuu mkuu CONTROLA . Mosi, zingatia vibao vyote vya barabarani (barabara husika) na mbili kabla ujaanza safari jifunze matumizi sahihi ya ‘GOOGLE MAP’ dunia sasa ni kijiji au kiganjani kwako since ‘ANDRO na iOS’ zipo utawalani. Kabla ya safari utaiona barabara yooote kwa simu yako. Hivyo basi pembeni ya uskani wako bandika simu yako yenye kukupa muongozo wa mtililiko wote wa barabara yako.

Hakika na kwambia utafurahia safari yako kuliko Wakati mwingine wowote.

Shukrani sana na uwe na muda mwema.
 
Mkuu kwanza kila junction haikosi vibao vya kukuelekeza Pia saivi tuna coverage ya internet maeneo mengi au unakuwa na offline map we nikuchapa tu gia mimi siulizi mtu yoyote popote, Map inanielekeza tu
 
Ukitoka dar kusafiri kupitia morogoro road.
unatoka ulikotoka mpaka ubungo unanyoosha unapita mlandizi mpaka chalinze, hapo kuna kibao kikubwa kinaelekeza ukiingia kulia Arusha /Moshi/Tanga/ mpaka mombasa.
ukinyoosba manake unaelekea morogoro ukifika msavu utakua kibao/bango linaelekeza ukuzunguka round about unaelekea Dodoma/manyoni/singida/ shinyanga na kuendelea. Ukiinyoosha kutokea morogoro utaelekezwa kwamba unaelekea iringa/Makambako/ na kuelendea.
Nataka nikuambie kila kwenye makutano vipo vibao/mabango yanaelekeza unakokwenda na kilometa zake ili mafuta yasije yakakuishia njiani.
Nawapongeza sana TANROADS kwa kazi nzuri wanayofanya.
 
Automatic ukiwa mkubwa utajua tu, kama vile ambavyo umejua sehemu ya kuingiza dushe lako bila kufundishwa na baba ako.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom