Jiwe Linaloishi
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 3,736
- 2,137
Utendaji wa JK ni wa namna ambayo unatakiwa uwe na kumbukumbu nzuri ili uweze kuufanyia tathmini.Pamoja na udhaifu wake JK anapendelea kuacha mfumo ufanye kazi yake.Hii inaweza ikatafsiriwa ya kuwa hataki lawama lakini kwa upande mwingine ndo utawala wa sheria unaotakiwa katika dunia ya leo,naomba nitoe mifano.Kwanza tuangalie mgomo wa madaktari ambapo mahakama iliamuru MAT wasitishe mgomo lakini viongozi wa MAt wakakaidi,wakzima mpaka simu na mgomo ukatokea lakini leo hii Rais wao ana kesi Mahakamani akishtakiwa kwa kukaidi amri halali ya mahakama na sio JK. La karibuni,hili la kina Ponda na wenzie angeweza kuwatia hata kizuizini kwa uchochezi lakini sasa wanakabiliana na kesi ambayo hawatamlaumu Raisi na ikiwa watashinda au kushindwa itakuwa ni uamuzi wa mahakama. Tujadiliane.
Nakubalia na wewe kwenye utaratibu wa kimahakama lakini mbona serikali hiyo hiyo haitaki kuheshimu hizo taratibu za mahakama hasa pale imapokuwa imeshindwa??