Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Baadhi ya viongozi wakuu wa CDM (wengi wajumbe wa Kamati Kuu) wanagombea Ubunge sehemu mbalimbali nchini. Baadhi ya hawa ndio wamekuwa waimbaji wakubwa wa sifa za Lowassa kama mgombea wao na wameamua kuweka heshima na hatima yao na ushindi wa Lowassa. Hili limenifanya nijiuliza maswali yafuatayo hasa kama wakianguka - kama wakishinda sidhani kama itakuwa shida mambo mengine. Ngoma itakuwa kwenye kama wakishindwa.
Lowassa Akishinda: Kama Lowassa akishinda (kinadharia tu japo haitotokea) na viongozi hawa wa CDM wakakataliwa majimboni mwao, Lowassa awakumbuka nafasi mbalimbali au aheshimu maamuzi ya watu na kuwaacha wajifikirie wenyewe? Au afanye kama marais wa CCM ambao mtu hata akikataliwa na wananchi anapewa nafasi nyingine ambazo zinaitwa za "ulaji"?
Lowassa akishindwa: Na wao wakashindwa, waendelee kuongoza chama hasa kama Lowassa ataamua baada ya kushinda kujiuzulu siasa au hata kuamua kurudi CCM (hata kimya kimya)?
Maswali haya ni muhimu kwa sababu zipo dalili za baadhi ya viongozi maarufu kujikuta wanakataliwa na wao majimboni na tusije kushangaa baadhi ya majina maarufu hayarudi Bungeni hasa kwa sababu wapo wanachama ambao kutokana na hili la Lowassa na dubwasha la UKAWA wataona kuwa viongozi wao wamewaingiza mjini na kukivuruga chama bila sababu ya msingi wakati ushindi ulikuwa uko njiani.