SWALI LA UGOMVI: Tatizo kubwa la familia za Watanzania ni ngono? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SWALI LA UGOMVI: Tatizo kubwa la familia za Watanzania ni ngono?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 5, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu nimekiona (labda na wengine wamekiona pia) ukiangalia sana mijadala inayoendelea kuhusu suala la mahusiano na mapenzi hapa mingi inahusiana na aspects mbalimbali za kungonoka. Nani kapewa nini, nani kanyimwa, nani anataka nani hajui jinsi ya kupata, vipi ilivurugika, vipi mtu anatamania n.k Kiasi kwamba unaweza kuhitimisha kuwa labda tuna matatizo makubwa zaidi katika eneo hili la ngono kuliko eneo jingine lolote la mahusiano. Je yawezekana ni kweli? Au ni kwamba watu wanatafuta kila sababu ya kungonoka zaidi na zaidi na kwa namna tofauti zaidi na zaidi?

  Je vipi suala la malezi ya watoto? Je tunatafuta msaada zaidi wa mashauriano kuhusu malezi ya watoto kama tunavyotafuta kujua juu ya mambo ya kupata ngono zaidi na tamu zaidi? Tunatafuta zaidi namna ya kufurahia ngono kuliko kufurahia matokeo ya ngono hizo?

  Au ni kweli kamba kwenye suala la malezi tuko pouwa zaidi na hatuhitaji msaada ila kwenye eneo la ngono ndio tunahitaji kushauriana zaidi?
   
 2. m

  mwanamabadiliko JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 340
  Trophy Points: 80
  Ni kweli kaka, ngono imekuwa tatizo kubwa, kiasi kwamba nimeamua kuwa singo, kila mwanamke nikikutana nae anadai simridhishi, kisa ni my Premature ejacul. Nawapa pesa,care, . Wanawake ni kama mbwa
   
 3. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakumbuka wakati Lowassa akiwa pm,alikwenda zanzibar kwenye mkutano,akawauliza tatizo ni nini hasa mbona ngona imekithiri sana?walimjibu tatizo ni Pweza,nafikiri watanzania wana neema ya chakula na vinywaji vya kurutubisha zile nanihii za zinaa,kizazi chetu kitapita na labda wajao wanaweza kubadilisha,anyway Mkuu mada ni nzuri na itapata wachangiaji wengi,sisi wazee tutakaa pembeni kusoma comment zao
   
 4. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  ngono ni tamu kuliko vitu vyote hapa duniani.
   
 5. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ni kwel familia nyingi za ktz zimejengwa kwa misingi ya ngono thats why matatizo hayaishi tungeweza kuchanel energy 2zitumiazo kwenye kutafuta ngono kwenye aspects nyingine za kifamily kama malez tungekuwa mbali sana
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,343
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha! MM unapouliza maswali ya changamoto, weka rangi katika alama ya kuuliza.
  Baada ya muda utasikia, MM amesema 'watu wangonoke'

  Siku za nyuma kulikuwa na mada nzuri, kuna tatizo katika safu na wana safu. Labda ndio wakati au umri n.k
  Nakuhakikishia matatizo yapo mengi kuliko ngono, sijui kwanini hayasemwi!!
  Anyway, MMU wapo njiani, nilisimama kusalimia tu
   
 7. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  ngoja nisikujibu!
  lakini hapana nahis ntakuwa sijitendei haki!
  WEWE NDIYE MBWA!tena koko i see!kutia ushindwe mwenyewe unakuja kutukana wanawake humu?wa wapi wewe?
   
 8. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  dah!umenikwachu wanasema watoto wa siku hizi!
  yani umeona mbali sana i see!kimisngi hata mimi ni mtuhumiwa katika hili,hivyo nashkuru kwa kunishtua Mzee Mwanakijiji
  nafkiri kasi hii ya kuchangia maswala ya ngono na mahusiano tungeipeleka kwenye kutimiza wajibu wetu kama wazazi pengine halia ingebadilika!lakini kipi kinaweza kututoa hapa tuanze na moja?hali si nzuri
  mapenzi yanachukua akili zetu kuliko maelezo,mapenzi yanatenda watu,mapenzi yanawapa watu amani
  lakini je hivi ni kweli ndilo pekee litupasalo kulijadili kila wakati?ahsante mkuu kwa kunirudisha kwenye mstari kwa kweli!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Mzee Mwanakijiji umetukumbusha kitu muhimu sana katika jamii ambacho wana MMU tumekuwa hatukiongelei mara kwa mara na hata ikitokea thread ya namna hii kuanzishwa, basi haipati mchango wala support ya kutosha.
  Nafikiri thread nyingi zinazungumzia ngono na mapenzi zaidi kuliko matatizo mengine ya kimahusiano ya kijamii kwa sababu ya unyeti wa suala lenyewe ya kwamba:

  Kwanza, mapenzi ndiyo hutuleta ndoa na baadaye watoto na familia kwa ujumla. Kukosa mapenzi ya kueleweka kunaweza kukunyima watoto au kukupa watoto wasio na malezi sahihi na hivyo kuwafanya wengi waipiganie part hii kuondoka na adha ya kuja kupata watoto kuishi na mama/baba wa kambo. Kwa kifupi, kinga ni bora kuliko tiba.

  Pili, changamoto nyingi sana za kimaisha, ukiacha za uchumi na magonjwa zinazofuata zinaweza kuwa ni za mahusiano. Utafiti huu usio rasmi umefikia hatua ya kuwatisha hata wale ambao hawajaoa/kuolewa kuanza kuogopa kuingia kwenye ndoa na badala yake kuangalia na kujadili matatizo ya wanandoa ya marafiki au ndg zao badala ya mahusiano yao binafsi ya baadaye. Angalia thread nyingi utasikia rafiki yangu alipata tatizo hili na mpenzi wake, au ndg yangu alikumbwa na hili au jirani yangu alifanyiwa hivi nk

  Tatu, suala la malezi kinadharia linatibika kirahisi zaidi either kwa wahusika kukubaliana au kufundishwa namna ya kulea watoto au sheria kuwalazimisha wazazi kutunza watoto wao na pengine hata mafundisho ya dini huwezi kusaidia kwa kiasi ktk malezi tofauti na mapenzi ambayo majeraha yake ni magumu sana kutibika kirahisi hususani mmoja wapo anapokuwa alipenda kwa dhati. Na hata yakitibika, makovu yanayobaki huwa ni magumu kufutika.

  Mkuu MM, sababu nilizozitaja hapo juu ni hisia zangu tu juu ya thread za mapenzi kuwa nyingi hapa MMU lakini hazifuti au ku-off set changamoto uliyotuletea.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Inapotokea kuwa wengi wa wahusika humu wapo katika safari ya kutafuta hao watoto wa kulea na mambo hayaendi sawa unafikiri tutazungumzia matokeo yaani watoto na huku njia bora ya kuwapata inatushinda?
  Wanawake hujitowa kwa wanaume kwa tamaa kuwa watajenga familia ya baadae huku wengi wa wanaume wanatafuta mchezo tu na inapotokea mwanamme anapopenda msichana akitegemea familia mwanamke anahadaiwa na mwengine na hadithi inakuwa ile ile ya kulalamika na kulipana visasi.
  Nafikiri tunahitaji jukwaa la Malezi peke yake na huko tena sidhani kuwa kutakuwa na hiyo nongonongo!
   
 11. c

  ckcacana Member

  #11
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mada na wachangiaji vyote viko poa kichizi.
   
Loading...