Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,736
- 40,858
Imebidi niuliize swali hili kwani inaonekana inawezekana tunapozungumzia suala la hali ya chakula nchini tunatumia maneno ambayo yana maana yanapotumiwa sawasawa. Kwa mfano baa la njaa (famine) siyo sawasawa na upungufu wa chakula (food shortage); maneno yote mawili yana maana ya kiufundi na hayatumiwi kama mbadala wa jingine.
Kwa wale ambao mnapita mitaani, masokoni n.k je mnashuhudia ukosefu wa chakula kiasi kwamba watu hawana chakula chochote na wanakaribia kufa njaa au mnashuhudia bei imepanda ya vyakula kwa sababu watu wanahofia chakula kitapungua msimu ujao sababu ya uchelewaji wa mvua mwaka huu?
Na je, mvua kuchelewa ni sawasawa na mvua kutokunyesha kabisa? kwa mfano, Watu walipanda mazao lakini mvua zikachelewa; ikabidi wapande tena mvua zilipoanza je hofu itakuwa ile ile sawa na wale ambao kwa mfano, Mvua hainyeshi kabisa msimu huu?
Kwa mfano, hadi sasa mvua isingenyesha kabisa hadi mwezi Juni hali ingekuwa sawasawa na mvua kunyesha hata kwa kuchelewa?
Isije kuwa kwa sababu za kisiasa na labda hofu ya kawaida ya kibinadamu tukajikuta tunatumia maneno ambayo baadaye yakaonekana hayana msigni kweli kweli. Tanzania ni kweli kuna njaa sasa hivi?
Hivi leo, Watanzania wanaofikiria au kuamini kuwa kuna njaa kubwa na wakataka serikali iingilie kati - kama wanavyofanya - watakuwa tayari kujipanga fulani na kupewa kadi za maduka ya kaya kama tulivyofanyiwa sisi miaka ile ya mwanzo ya themanini na kuokoa wananchi kutokana na ukame ulioleta upungufu mkubwa wa chakula?
Leo, wakiambiwa kama sehemu ya serikali ya JPM kukabiliana na upungufu wa chakula wakaleta unga wa Yanga tutakuwa tayari au tutalilia unga mweupe? Leo, ili kuhakikisha maskini na matajiri wote wananafasi sawa ya kupata chakula watu wakapangiwa kiasi (ration) ya vitu wanavyoweza kununua kuanzia sabuni, sukari, chumvi au unga n.k watakuwa tayari kukabiliana na hali hiyo au watasema "kila mtu ajitegemee, serikali isiwapangie watu kiasi cha kununua; mwenye uwezo aache kununua anachotaka asiye na uwezo na lwake?"
Ni kweli tunataka serikali iingilie kati sasa hivi?