Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Swali la Ugomvi: Miaka hii tisa wametuhubiria sana "mafanikio" yao, wametuonesha vyuo, barabara, mahospitali n.k ambavyo wamevifanya na wanajivunia. Ghafla kila mmoja anayetaka kugombea anasema "mabadiliko"; oo "ntabadilisha x,y". Najiuliza mbona hawasimamii 'maendeleo' yao wenyewe kila mmoja ni kama anayaruka?
Mara kadhaa tumewasikia wakitamba Bungeni "Serikali sikivu ya CCM imefanya a, b, c, na d" na tena kwa kejeli wengine walidai "hawa wapenzi hawayaoni?". Sasa leo, watangaza nia wetu ambao wengi ni mawaziri, manaibu au wabunge wote wanajaribu kutuaminisha kuwa nchi inaelekea kubaya kiasi kwamba inahitaji "mabadiliko". Kulikoni wenzetu? Yale mafanikio yamepeperuka au yalikuwa yakuzuga au sasa na nyie mmeamua kudandia treni la "mabadiliko"?
Obama alipotangaza "Change" alikuwa anamaanisha mabadiliko hasa kutoka chama na utawala wa Rais George Bush. Alikuwa analipeleka Taifa lake upande mwingine - kwa uzuri au kwa ubaya. Wananchi walioamuamini na kumpigia kura walifanya hivyo kwa sababu waliamini katika "mabadiliko". Sasa hawa wenzetu, chama chao, serikali yao na asilimia 99 wamewahi kutumikia serikali hiyo hiyo kwa nyadhifa mbalimbali; sasa iweje leo watuambie na kutuimbia "mabadiliko" na baadhi yetu kama tuliolishwa limbwata la kisiasa tunashabikia kweli kutakuwa na "mabadiliko".
Unaweza vipi kubadilisha kitu ambacho hakijabadilika isipokuwa kukibadilisha bila kukibadilisha; kama kubadilisha duara?
Picha hii haiko sawa. Nini tatizo?