Swali la ugomvi: kina Warioba wametumia kiasi gani kuja na hii rasimu ?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Hivi kweli hii rasimu ya katiba mpya inaendana na thamani ya fedha (value for money ) iliyotumika na tume ya Warioba? Mliomsikiliza jana alisema ni kiasi gani tume imetumia hadi sasa? Je rasimu hii isingeandikwa na jopo la wataalamu wachache kabla ya kufanya igizo la kukuaanya maoni?
 
Je zanzibar watakubali hili?

SURA YA NANE
VYOMBO VYA DOLA VYA TANGANYIKA,NA ZANZIBAR
SEHEMU YA KWANZA
SERIKALI YA TANGANYIKA NA YA ZANZIBAR

101.(1) Kutakuwa na Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar ambazo zitakuwa na mamlaka katika Tanganyika na Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Shirikisho kwa mujibu wa Katiba hii;
(2) Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar zitaundwa na kutatekeleza madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii na Katiba ya Tanganyika na Zanzibar;
(3) Kiongozi Mkuu wa wa Serikali ya Tanganyika na pia Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Zanzibar ataitwa Gavana wa Tanganyika na Gavana wa Zanzibar;
 
katiba ya Tanaganyika hiko wapi?????
(4) Kutakuwa na kiapo rasmi cha Gavana wa Tanganyika na cha Gavana wa Zanzibar kitakachosimamiwa na Jaji Mkuu wa Tanganyika na Jaji Mkuu wa Zanzibar ambapo viongozi wote wawili wataapa kuitii, kuilinda na kuitetea Katiba hii, kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania, na kiapo kingine chochote kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar.
76
102. (1) Magavana wa Tanganyika na Zanzibar watachaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar;
 
HEBU ONA HII IMEKAAJE.JE KUTAKUWA NA TUME YA UCHAGUZI YA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

SEHEMU YA PILI
MABARAZA YA WAWAKILISHI
103. (1) Kutakuwa na mabaraza mawili ya wawakilishi, moja la Tanganyika na jingine la Zanzibar ambayo yatakuwa na mamlaka ya kutunga sheria kuhusu mambo yasiyo ya Shirikisho, kujadili, kusimamia na kudhibiti shughuli za Serikali za Tanganyika na Zanzibar;
(2) Mabaraza ya wawakilishi yatakuwa na wajumbe wanaolingana na idadi ya majimbo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume za Uchaguzi za Tanganyika na Zanzibar;
 
Wamedesa ile mbaya. Haya yote waliyoleta yalikuwa obvious. Tume ya uchaguzi haimo kwenye katiba?
 
Kumbuka kwenye bajeti hii
Walihoji lakini maneno mepesi
kama wanajitolea

Hapo ni funika kombe Mwanaharamu
apite kwanza.
 
Hivi kweli hii rasimu ya katiba mpya inaendana na thamani ya fedha (value for money ) iliyotumika na tume ya Warioba? Mliomsikiliza jana alisema ni kiasi gani tume imetumia hadi sasa? Je rasimu hii isingeandikwa na jopo la wataalamu wachache kabla ya kufanya igizo la kukuaanya maoni?

Je, Katiba ya Tanganyika itaandikwa lini ama tutatumia hiyo hiyo?
maana tunashangilia kuwepo kwa serikali 3 ilihali ZNZ wana katiba yao, Tanganyika mh!!
 
7) Kamati ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya Ibara hii, itakuwa na
wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa
Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Bara;
(c) Jaji Mkuu wa Zanzibar; na
(d) wajumbe wengine sita watakaoteuliwa na Spika
 
sasa ni wazi kuwa hii katiba haitaweza kutumika katika uchaguzi ujao au labda yale ya kumwongezea muda mhisimiwa dhaifu kwa miaka miwili yawe ya kweli(tutaliaje).hapa kwanza tunatakiwa tuanze safari mpya ya kutengeneza katiba ya Tanganyika na kurekebisha mambo pande zote kabla ya kuanza kutumia hii.tumerudi nyuma kwa miaka 50.
 
Hatuna rasimu ya katiba tuna kasima ya katiba!! wamekula tumeliwa!! haina utofauti na iliyopo! Kilio cha wananchi juu ya katiba ya maana hakipo tena ukiunganisha na mabaraza ya ccm katiba!!
Rais mteule wa kila kitu!!
Rais mwajiri wa utumishi!
rais mwajiri wa JAji mkuu!! eti kutoka tume ya utumishi!
Rais anakinga ya kutoshitakiwa ingawaje pia hawakutoa sababu gani imepelekea kufanya hivyo!
RAis mchagua mwenyekiti wa Tume ya rais ya uchaguzi!
Rais ashauriwe kuhusu kuteua IGP na wengineo! ana weza akakataa watamfanyaje??!!

WAMEKULA TUMELIWA!!!!
TUSUBIRI MIAKA 50 TENA!
WARIOBA HANA MAANA KAMA ALIVYOFANYA KWENYE TUME YA MKAPA YA RUSHWA!!
 
Unafikiri kweli inetokana na wananchi?

Imetokana na Tume ya katiba! Mfano: suala la Rais kuondolewa kinga ya kutoshitakiwa! wananchi walipendekeza kwa wingi kuwa rais ashitakiwe atokapo madarakani! Tume imependekeza rais akiwa bado madarakani ashitakiwe na Bunge na Je, AKIWA AMESTAAFU URAIS IWEJE???
 
Sifa za
Mawaziri
na Naibu
Mawaziri
94.-(1) Mtu atateuliwa kuwa Waziri au Naibu Waziri wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano ikiwa:
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa
Sheria za nchi;na
(b) angalau ana shahada ya kwanza ya Chuo Kikuu
kinachotambulika kwa mujibu wa Sheria za nchi.
‐ 39 ‐
(2) Watu wafuatao hawatakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa
Mawaziri au Naibu Mawaziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano:
(a) Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Wabunge wa
Bunge la Tanzania Bara, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar au madiwani kutoka Washirika waMuungano;
(b) mtu aliyewahi kutiwa hatiani kwa makosa ya ubadhirifu wa
mali za umma, ama katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
Serikali ya Tanzania Bara au Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
 
Nimewasoma wote, imeletwa ili tuikosoe na kuongeza/kuuliza ambayo hatuyaelewi!
Swali, je watakubali mapendekezo mapya??? Je, wametoa muda gani wa kuipitia na hatimaye kutoa rasmi?
Je, itakuwa tayari by 2014?
 
Back
Top Bottom