Swali la ugomvi: kina Warioba wametumia kiasi gani kuja na hii rasimu ?

Hivi kweli hii rasimu ya katiba mpya inaendana na thamani ya fedha (value for money ) iliyotumika na tume ya Warioba? Mliomsikiliza jana alisema ni kiasi gani tume imetumia hadi sasa? Je rasimu hii isingeandikwa na jopo la wataalamu wachache kabla ya kufanya igizo la kukuaanya maoni?

unajidhalilisha mkuu, kaa huko ulaya ponda maisha ya huku tuachie wenyewe, kama maisha yamekushinda tukutumie nauli urudi nyumbani
 
Uteuzi wa viongozi wa taasisi za serikali (Iwe mawaziri, majaji, wakuu wa vyombo vya usalama,n.k) ufanywe kwa kutangaza nafasi na watu wapeleke maombi yao. Maombi yachujwe kwa kuzingatia vigezo vitakavyowekwa. Wachache watakaopita katika huo mchujo wafanyiwe usaili (Interview) na tume ya uajiri. Baada ya interview, tume itachuja hadi majina matatu yatakayopelekwa kwa Raisi kwa kuteuliwa. Raisi nae atapeleka hilo jina moja atakaloliteua bungeni kwa kuthibitishwa. Utawala bora unaanzia kwenye uteuzi wa watendaji kwa mfumo wa uwazi na shirikishi. Hapa mtu akiboronga hakuna wa kumlaumu yeyote. Tujifunze mfano wa Kenya ambapo hata interview ya viongozi wazito, mawaziri, majaji, wakuu wa vyombo vya usalama unavyofanyika kwa uwazi na kuwezesha wananchi wote kuushuhudia kupitia luninga. Bravo Kenya!!!!
 
Lakini watu 250,000 kati ya millioni 50 waliotoa maoni si ni kundi dogo? Unasemaje kuhusu hilo? barafu

ndo tabia ya Watanzania..wakipewa nafasi hawajumuiki..wanabakia kulalama nyuma ya key board!hakukuwa na masharti na bado hawakutokea..kungekuwa na masharti je?
 
Last edited by a moderator:
Je zanzibar watakubali hili?

SURA YA NANE
VYOMBO VYA DOLA VYA TANGANYIKA,NA ZANZIBAR
SEHEMU YA KWANZA
SERIKALI YA TANGANYIKA NA YA ZANZIBAR

101.(1) Kutakuwa na Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar ambazo zitakuwa na mamlaka katika Tanganyika na Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Shirikisho kwa mujibu wa Katiba hii;
(2) Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar zitaundwa na kutatekeleza madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii na Katiba ya Tanganyika na Zanzibar;
(3) Kiongozi Mkuu wa wa Serikali ya Tanganyika na pia Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Zanzibar ataitwa Gavana wa Tanganyika na Gavana wa Zanzibar;

Kwanini GAVANA na sio WAZIRI MKUU,

Wanataka kupokonya madaraka ya Tanganyika na zanzibar ?
 
Hivi kweli hii rasimu ya katiba mpya inaendana na thamani ya fedha (value for money ) iliyotumika na tume ya Warioba? Mliomsikiliza jana alisema ni kiasi gani tume imetumia hadi sasa? Je rasimu hii isingeandikwa na jopo la wataalamu wachache kabla ya kufanya igizo la kukuaanya maoni?
Haikuwa lazima kwa kundi lote hilo la watu kuzunguka nchi nzima. Kila nikisoma draft najiuliza what is the catch.
 
Binafsi nnafikiri wametumia utaratibu wa ushirikishwaji wananchi, serikali ya ccm huwa haiangalii swala la gharama, maana nchi ina hela nyingi za kuchezea, ndo maana unaweza hata kuona Rais wa nchi akisafiri kila wiki bila kujali gharama na faida za safari yake kwa nchi yetu.
 
Inaonekana watu wamekubali mapendekezo ya Katiba jinsi yalivyo kiasi kwamba hawataki kuhoji kabisa.. haya nitawasaidia kuichambua in Shaa Allah.
 
7) Kamati ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya Ibara hii, itakuwa na
wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa
Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Bara;
(c) Jaji Mkuu wa Zanzibar; na
(d) wajumbe wengine sita watakaoteuliwa na Spika

Naomba kujua huyu Mkuu wa Tanzania Bara ni wa nchi tofauti na Tanganyika??
 
MMM sina majibu ya maswali yako, hivyo hata na mimi ningependa kupata majibu ktk hilo.

Asubuhi ya leo kijana Nape alikuja hapa jamvini akikejeli eti wako wapi tuliokuwa tunaipinga Tume ya Katiba. He's, of coz, off the mark as usual.

Well, kwa CCM wengi na baadhi ya watu wa itikadi nyingine za kisiasa "Katiba Mpya" ni zawadi ya mtawala kwao. WRONG.Ndio maana huwa wanasema ooh ".....JK ni Rais wa ajabu maana katoa uhuru wa vyombo vya habari..." na mambo mengine mepesi mepesi. Huo ndio utamaduni wa CCM na marafiki zao... kutokufikiri na kuchambua mambo.

Hii rasimu na muundo mzima ulioko hauwezi kutupa Katiba ambayo Tanzania ya leo na ya kesho inaihitaji.
Kuna dosari na mapungufu na makosa mengi tu (hasa ya kiuandishi) na baadhi ya makosa ya kimsingi ktk rasimu husika. Hebu niulize mfano mdogo tu: ukisoma ibara ya 70 (1) (e) utaona maneno haya "Mjumbe mmoja anayewakilisha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa"
Sasa Ktk rasimu yote ya Jaji Warioba, pendekezo kuu ni kuwa iundwe Tume Huru ya Uchaguzi ili ichukue kazi ambazo kwa sasa zinafanywa na Msajili wa Vyama vya Siasa + na kazi/mamlaka ya Tume ya sasa ya uchaguzi. Sasa watueleze huyo mjumbe wa hiyo Ofisi ya Msajili atapatikanaje wakati huo? (kwani ofisi na mamlaka hiyo zimekwishafutwa kimantiki na kisheria) Na je maudhui ya mkanganyo ni yapi?
 
naona wamekopi sheria mbalimbali zilizopo na kuongeza kurasa za katiba mfano haki za mahabusu wamecopy kwenye cpa, haki za mfanyakazi wamecoppy sheria ya kazi aina za raia wamecopy kwenye immigration act n.k
 
Unafikiri kweli inetokana na wananchi?

Mkuu na mimi niongezee kidogo, kama ulimsikiliza vizuri mwenyekiti alikuwa ansema "mapendekezo ya tume", je niya tume au ya wananchi? maana mimi nilidhani kazi ya tume ni kusummarize wanachosema wananchi wlalio wengi na sio tume kuwaamulia wananchi nini kinafaa na nini hakifai. Hii process kuna vitu sijavielewa vizuri hata kidogo.

Kama mawazo ni ya wajumbe wa tume basi ingekuwa bora wakae tu wenyewe walete draft kama mdau mmoja alivyodokeza.
 
Je zanzibar watakubali hili?

Mkuu,hebu angalia rasimu yako vzr ili usiwachanganye watu
SURA YA NANE​
URATIBU WA MAHUSIANO YA WASHIRIKA WA MUUNGANO

102.(1)Kutakuwa na Tume ya kusimamia na kuratibumahusiano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali za Washirika waMuungano na kusimamia na kuratibu mahusiano baina ya Serikali zaWashirika wa Muungano, ambayo itajulikana kwa kifupi kama "Tumeya Mahusiano na Uratibu wa Serikali".
‐​
42 ‐
(2) Tume ya Mahusiano na Uratibu wa Serikali itaundwa nawajumbe wafuatao:(a) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambayeatakuwa Mwenyekiti;(b) Rais wa Tanzania Bara;(c) Rais wa Zanzibar;(d) Mawaziri Wakaazi;(e) Waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje wa Serikali ya​
Jamhuri ya Muungano
~Seen today~
 
watz ni tatizo hakuna jema? wangejitokeza watu milioni moja angeibuka mtu na kusema hakukuwa na haja ya kufanya hivyo.
kuhusu gharama kila kitu kina gharama yake
 
Inaonekana watu wamekubali mapendekezo ya Katiba jinsi yalivyo kiasi kwamba hawataki kuhoji kabisa.. haya nitawasaidia kuichambua in Shaa Allah.

As usual asilimia fulani iko kwenye msiba wa magwea, nyingine iko busy na mechi ya stars na Morocco, wengine wako busy kutayarisha sabasaba kiasi kwamba muda wa kutafakari rasimu ya katiba ni mdogo sana.

Natatizwa na utaratibu wa transition , endapo rasimu hii itapita, kutoka serikali mbili kuwa serikali tatu, Hasa ukizingatia kuwa serikali ya Tanganyika aka Tanzania bara ilikwisha ua katiba yake. Kwa maana nyingine inabidi kutafuta jina, wimbo wa taifa, bendera ya nchi , serikali, bunge, mahakama, nakadhalika.
 
sasa ni wazi kuwa hii katiba haitaweza kutumika katika uchaguzi ujao au labda yale ya kumwongezea muda mhisimiwa dhaifu kwa miaka miwili yawe ya kweli(tutaliaje).hapa kwanza tunatakiwa tuanze safari mpya ya kutengeneza katiba ya Tanganyika na kurekebisha mambo pande zote kabla ya kuanza kutumia hii.tumerudi nyuma kwa miaka 50.
Kama tetesi za kuongeza muda ziliyolewa na Lipumba then there is every truth kwani watakuwa wali-confide.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Je, Katiba ya Tanganyika itaandikwa lini ama tutatumia hiyo hiyo?
maana tunashangilia kuwepo kwa serikali 3 ilihali ZNZ wana katiba yao, Tanganyika mh!!

Kwa mantiki hii uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani hapa nchini utakuwa 2017 badala ya 2015. Katiba ya Tanganyika itaanza kuandaliwa kati ya 2015 na 2016. Kikwete kaula, atakaa madarakani kwa zaidi ya miaka 10.
 
Mkuu na mimi niongezee kidogo, kama ulimsikiliza vizuri mwenyekiti alikuwa ansema "mapendekezo ya tume", je niya tume au ya wananchi? maana mimi nilidhani kazi ya tume ni kusummarize wanachosema wananchi wlalio wengi na sio tume kuwaamulia wananchi nini kinafaa na nini hakifai. Hii process kuna vitu sijavielewa vizuri hata kidogo.

Kama mawazo ni ya wajumbe wa tume basi ingekuwa bora wakae tu wenyewe walete draft kama mdau mmoja alivyodokeza.

Inawezekana haya yakawa ya TUME na ya WANANCHI yatakuja badae,
 
Hivi kweli hii rasimu ya katiba mpya inaendana na thamani ya fedha (value for money ) iliyotumika na tume ya Warioba? Mliomsikiliza jana alisema ni kiasi gani tume imetumia hadi sasa? Je rasimu hii isingeandikwa na jopo la wataalamu wachache kabla ya kufanya igizo la kukuaanya maoni?
Yawezekana pia ilikuwa hivyo unavyosema - rasimu ilikuwepo kabla ya kukusanya maoni!
 
Back
Top Bottom