Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Mara nyingi utaona watu wanalisifia sana jeshi letu la Ulinzi hasa baada ya operesheni fulani. Mfano mzuri ni hili la kwenda DRC na kuwachakaza M23; licha ya kupoteza wapiganaji kadhaa jeshi letu bado limesifiwa kwa umahiri katika medani ya mapambano.
Kwa wale tulioshuhudia kwa karibu Vita ya Kagera na harakati za Ukombozi wa Nchi zilizoko Kusini mwa Afrika tunajua ni kwa kiasi gani jeshi letu lilijipatia heshima katika kushiriki mapambano, kutoa mafunzo na kulinda usalama wa nchi yetu. Kiasi kwamba tulijiaminisha kuwa jeshi letu ni mahiri kabisa katika eneo letu hili. Kutokana na ujuzi huo tumekuwa na kiburi cha ufahari wa jeshi letu; ndio maana tunapochokozwa na majirani zetu hatuchelewi kuanza kushadadia vita na mapambano kwa sababu tunaamini kabisa kuwa katika eneo letu hakuna nchi ambayo inaweza ikaingia vitani na sisi ikatupiga; siyo Malawi, siyo Rwanda wala siyo nani.
Siri ya mafanikio haya ya jeshi letu ni nini hasa? Je ni kwa sababu tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika vifaa vya kijeshi? (hili si kweli); je inawezekana ni kwa sababu tuna silaha za kisasa zaidi kuliko wengine? au kwa sababu sisi ni Tanzania kana kwamba kwa kuwa Tanzania basi automatically jeshi letu ni bora zaidi? Au kuna siri kubwa zaidi na ya msingi?
Naomba kupendekeza kwa msomaji kuwa siri ya mafanikio ya jeshi lolote duniani (likiwemo la kwetu) imelala kwanza kabisa katika nidhamu (discipline). Jeshi lisilo na nidhamu haliwezi kushinda vita hata kama lina silaha, wataalamu au mabilioni ya pesa. Vitu vingine ni muhimu sana katika kufanikisha mapambano lakini hakuna kitu muhimu kama kuwa na wapiganaji walio na nidhamu iliyopitiliza; ambao wanatambua majukumu yao barabara na ambao pamoja na makamanda wao wako moyo mmoja kutafuta ushindi. Hakuna brigedi, hakuna kikosi, hakuna company ambayo inaweza kusimama peke yake au kujifanyia mambo yake kwa ajili ya sifa zake yenyewe. Jeshi lote na sehemu yote chini ya majenerali husika ndio linaenda kutafuta ushindi. Jeshini hakuna sifa ya kikosi moja au kapteni mmoja!
Lakini ni hii nidhamu ndio msingi wa ushindi. Baada ya nidhamu hii ni ile hali ya kujitoa kwa lengo lililoko - total commitment to the cause. Mara baada ya lengo kuwekwa bayana -kumtambua adui na kupambana naye - vikosi vyote chini ya makamanda wao na wote hao chini ya kamandi kuu ya vita (Military High Command) vita vinaenda kupiganwa. Hiyo MHC nayo inapata maelekezo yake ya malengo ya kisiasa kutoka kwa viongozi wa kiraia wa nchi (civilian authorities) wakiongozwa na Amiri Jeshi Mkuu. Kutoka hapa ndio suala la vifaa, utaalamu n.k vinapokuja.
Wapo wanaoitwa makamanda katika siasa za Tanzania; na hasa katika chama kikuu cha upinzani CDM. CDM wameaminisha umma wa Watanzania kuwa wao "wapiganaji" wanataka kweli kuiondoa CCM madarakani. Mengi yanasemwa na mengi yanaahidiwa. Tunachoshuhudia sasa hivi na kwa muda kidogo sasa kunafanya tuhoji kama zipo brigedi zilizoasi, kamandi zilizopoteza amri, au kama kuna makomandoo ambao wameenda rogue! Majibizano kufuatia amri ya Kamati Kuu na jinsi ambavyo vikundi mbalimbali - wenyewe wanajiita wapiganaji - vinajitokeza kupingana vyenyewe kwa vyenyewe na hasa tukishuhudia kile ambacho tunaweza kuita MHC ya kisiasa imegawanyika inabidi tubakie na swali ambalo tayari limeshaulizwa na wengine vile vile.
Je, bila nidhamu tunaweza kushinda kweli? Bila kuwa pamoja kwa malengo na harakati adui anaweza kushindwa kweli? Je, kuna uwezekano wapiganaji wakaamua kujipigania vita vyao vyenyewe bila kujumuisha harakati zao na zile za jeshi zima? Je, makamanda wenyewe wanapowekeana bunduki vichwani mwao huku wakitunguana wenyewe kwa wenyewe kama watu wanaotungua tetere kwenye nyaya za umeme kweli kuna matumaini ya kushinda vita? Siyo kwamba tutafika kwenye final stand hatuna mtu wa kurusha risasi ya mwisho? SIyo kwamba tutajaribu kusonga mbele vitani huku kila kamanda anachechemea na wapiganaji wa vikosi mbalimbali wanatoka damu wengine wakiwa wameangamizwa na risasi za wenyewe kwa wenyewe (friendly fire)?
Wazo.
MMM