Swali la ufahamu: TAKUKURU wanahusikaje kuchunguza kauli ya Askofu Gwajima kuhusu chanjo ya Corona?

pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,636
6,261
TAKUKURU wameagizwa na waziri wa Afya (Dorothy) wakamchunguze Askofu Gwajima Kwa kusema chanjo ni feki na ina sumaku.

Swali: hapo TAKUKURU wana kazi gani?
 
Hiyo Task force, Gwajiboy anatakiwa achunguzwe na:
Polisi
TAKUKURU
Tume ya kudhibiti matumizi ya drugs
Mkemia mkuu
Hospitali ya Milembe.

Na mwisho anapelekwa kamati ya CCM kuvuliwa uanachama na ubunge.
 
Wameshindwa kumjibu Gwajima hoja zake wanaanza kumtisha na kutumia mabavu...
Sasa hivi baada ya Magu kufariki ndio wanajifanya wanatambua chanjo...
Hivi hii nchi unafiki utaisha lini?
 
TAKUKURU wameagizwa na waziri wa Afya (Dorothy) wakamchunguze askofu (josefu) gwajima Kwa kusema chanjo ni feki na ina sumaku.

Swali: hapo TAKUKURU wana kazi gani??
Kwanza nikufahamishe kwamba viongozi wetu wanapenda sana kutisha wananchi wao na kujikweza, pili, hasa awamu ya 5 na hii hawajui vizuri mifumo ya utendaji kazi serikalini, taratibu, sheria na kanuni mbalimbali za utumishi wa umma. Wao wanachoangalia ni kupata ujiko na kuiga wenzao.

Kiongozi anayejua wajibu wake na majukumu ya taasisi mbalimbali hawezi kusema TAKUKURU wakamchunguze Gwajima, na hii ni ushahidi kwamba huyo waziri hajui majukumu ya TAKUKURU kabisa.

Kingine ni kwamba hiki chombo, TAKUKURU tokea ameondoka Edward Hosea hakijapata mtu bold na mwenye msimamo, ndiyo maana badala ya wao kubaini na kufanya uchunguzi wao kitaalamu mara nyingi wamekuwa wanaelekezwa na wanasiasa na viongozi wengine cha kufanya.

Kuna clip nimeona muda mfupi uliopita ambapo IGP Simon Sirro amegomea hayo maagizo akisema wayamalize wenyewe huko.
 
Wameagizwa wamkamate kwa sababu amesema kuna viongozi wamehongwa pesa na wenye Corona wakubali na kuhamasisha chanjo.
TAKUKURU wameagizwa na waziri wa Afya (Dorothy) wakamchunguze askofu (josefu) gwajima Kwa kusema chanjo ni feki na ina sumaku.

Swali: hapo TAKUKURU wana kazi gani??
 
Back
Top Bottom