Swali la ufahamu: katika hifadhi huwa kumetengwa eneo la makaburi ya wanyama wanaokufa?

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,438
14,916
Binafsi sijawahi kutembelea hifadhi za wanyama katika mbuga zetu.

Lakini kuna swali linanisumbua,nimesikia kuna kaburi la mnyama linatakiwa lionyeshwe,nawauliza wazoefu wa masuala ya mbuga za wanyama kama kuna utaratibu wa kutenga eneo la makaburi hifadhini kwa ajili ya wanyama waliokufa kama binadamu tunavyotengewa maeneo,mfano makaburi ya kinondoni,na anapozikwa huandikwa RIP fulani

Athante
 
Binafsi sijawahi kutembelea hifadhi za wanyama katika mbuga zetu.

Lakini kuna swali linanisumbua,nimesikia kuna kaburi la mnyama linatakiwa lionyeshwe,nawauliza wazoefu wa masuala ya mbuga za wanyama kama kuna utaratibu wa kutenga eneo la makaburi hifadhini kwa ajili ya wanyama waliokufa

Athante
Hawazikwi officially bali hufukiwa na madawa hasa kama walikufa kwa magonjwa ya kuambukiza...vile vile huchomwa moto na wengine kama joni wetu huwa chakula cha wazee wa mizoga
 
Hawa jamaa yaani ni vituko ili mradi tujue wanafanya kazi, ila ile miili ya watu 7 wala hawataki kujua DNA yao ili ya john wameitolea macho
 
Mizoga ya wanyamapori huwa uchomwa moto pale lnapoonekana amekufa kwa ugonjwa fulani ili usisambae.
 
Hakuna... wanatupwa, pembe ndo huchukuliwa kwasababu ni bidhaa kuntu...!
 
Kaburi la faru! Afanaleki! Kuna jambo linasukumwa ili lisahaulike na maisha yaleyale yaendelee. Hivi nalo hili ni Kati ya Yale ya ujenzi wa viwanda?
Njooni ni mbinu jenzi bwana, hizi za kaburi hazituondolei kero na changamoto zinazotukabili Kama za ajira na maji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom