VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Naulizia ile combination ya jana ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU). Combination ya jana, imejitokeza jana na kutema mkwara mzito kwa wezi na mafisadi. Mkwara wa hadi kufilisi mali za wezi na mafisadi.
Kama ilivyo ada na mtindo wa Serikali ya Rais Magufuli, kila anayezungumza na wananchi kupitia waandishi wa habari hutema mkwara heavy. Na wa jana pia nao uko hivyohivyo. DPP Biswalo Maganga ni mtu mwenye nguvu kubwa kikatiba kuhusu mashtaka. Anaweza kuanzisha,kuendeleza,kufuta,kuondoa,kurejesha,kuunganisha na kadhalika kesi yoyote ya jinai.
DPP akishirikiana na Polisi na TAKUKURU aweza kufanya makubwa kimahakama bila ya kuzungumza na waandishi wa habari. Kujitokeza kwa wakuu wa jana na kusema waliyoyasema ndiyo Mahakama ya Mafisadi ya Rais Magufuli? Au nao wamejitokeza ili ijulikane kuwa wapo? Kama sheria na mahakama zilizopo zaruhusu yote yaliyosemwa jana, kuna haja gani ya mahakama ya mafisadi mpya?
Ufike muda wa vitendo. Maneno yanatisha lakini yametosha. Maneno huonesha mzaha na baadaye kuwa karaha. Ifike wakati, HAPA KAZI TU iwe kivitendo. Wezi na mafisadi wakamatwe na kushtakiwa. Silent operations are more sound than noisy conversations!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Pemba)