singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
kwa tunaofuatilia siasa za nchi hii, na tunajua maana ya siasa ni nini na ni wapi chadema iliharibikiwa baada ya kubadili gia angani kwa kumpokea lowaasa na kumfanya kuwa mgombea wao wa urais katika uchaguzi mkuu wa 2015, vile vile ilipo sasa na inakoelekea.
Kwa msomi yeyote makini na mahiri katika fani ya sayansi ya siasa, anatambua vyema kwamba hakuna kipindi chochote katika historia ya nchi hii, ambacho ni kigumu kufanya siasa zenye uelekeo za ushawishi wa umma (to win mass) kama katika kipindi hichi cha Rais Dk. Magufuli
Siasa kwa mwanasiasa yeyote yule duniani, ni uwezo wake wa kushawishi umma ili watu wamkubali, umwamini, umheshimu na uwe na imani naye. Kinyume na hapo, mtu huyo hawezi kuwa mwanasiasa.
sasa basi baada ya kukosea kwa Mbowe na chadema katika uchaguzi mkuu uliopita tumeona yanayoendelea bungeni kwa chama hicho na mbinu zile zile za awamu ya nne za kutoka bungeni kwa visingizio mbalimbali hii ina maanisha nini? Wananchi wa kawaida tunafaika nini na vituko vya upinzani bungeni vikiwa na baraka za kiongozi wa kambi upinzani (KBU)
Swali langu kubwa kwa figisufigisu zinazofanywa na upinzani bungeni nini mashiko yake kwa wananchi kwa ujumla wake?
Je kwa kulitumia bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma, Mwenyekiti wa chama cha demokrasoia na maendeleo chadema anaweza kuutua mzigo wa mkubwa wa mzimu wa Edward Lowassa unaomwelemea, na kurejesha heshima ya chama chiko ya kisiasa, hivyo kufufua iamani kwa umma wa watanzania kwakwe na chadema.
nawasilisha