Swali la Tundu Lissu linakosa mjibuji?

Contribution ya profesionals kwenye mambo ya msingi ya nchi yetu inatia mashaka sana.Wengi wanafanya kazi kwa kutegemea huruma ya wanasiasa ndio maana wamepumzisha akili zao kabisa kwenye masuala yanayohusu nchi.
 
Swali hilo ni sawa na kuuliza kwamba kwa nini WAGANGA wa KIENYEJI hawaukemei UCHAWI?
Pili, Mawakili wengi wako kimya kwa sababu wanafaidika na mfumo uliopo kwa kazi yao ya uwakili ambapo wanawatoza pesa nyingi wateja wao na hakuna KODI wanayolipa serikalini.
 
Akiisha kuchangia kwasehemu kubwa katika mada hiyo Lissu alisema" Ni swali ninalojiuliza sana, mara nyingi, hata sasa ninajiuliza ni kwanini Baraza la Mawakili limekuwa kimya hadi sasa juu ya tuhuma za ufisadi? Masuala ya EPA, Richmond, Kagoda yanatajwa wako kimya.Hawajatoa tamko wala kuchukua hatua

Yeye vile vile ni wakili, je alililiwakilisha kwenye baraza hilo ombi lake?. Nini maamuzi ya baraza hilo la mawakili?
 
Unataka waseme nini wakati mawakili wenyewe ndio wahusika. Maregesi Law chambers, Mkono Advocate, IMMA. Na hizi kumbuka ni moja ya kampuni zenye nguvu sana katika field hiyo.

Safi LISSU! Tunataka watoe msimamo if possible wawasimamishe uanachama wanaohusika kuihujumu nchi

Ingekuwa masuala ya maslahi yao wangeshakuja juu kweli na kelele nyingi. Hapa wameguswa
 
Contribution ya profesionals kwenye mambo ya msingi ya nchi yetu inatia mashaka sana.Wengi wanafanya kazi kwa kutegemea huruma ya wanasiasa ndio maana wamepumzisha akili zao kabisa kwenye masuala yanayohusu nchi.

Lakini chanzo mkuu ni kutokana na kwamba mwanzoni wasomi/professionals walijaribu kuwa wanatoa ushauri lakini baadaye ikaonekana kuwa wanawatilia kauzibe wanasiasa/wezi. Ndo baada ya hapo wasomi nao wakaona watumie ule usemi kuwa "if you can not fight them then join them". Fikiria mwandosya alipokuwa wizara ya nishati na madini, sikumbuki vizuri lakini alitoa ushauri nadhani kupinga IPTL lakini wanasiasa wakampinga na akajiuzuru, leo vipi si aliamua kuwajoin!

Kwa hiyo ni kwamba even advocates, nao wengi wamekata tamaa ndo maana wamekuwa wala rushwa wakubwa. Nenda pale jengo la sido DSM, kuna advocate anaitwa Ndanzi, nadhani ni kinara wa issues za kupindisha sheria lakini ni tajiri kupindukia, na wa namna hii wako wengi.
 
Mambo ya "Maslow Hierarchy of Needs" as detailed in the seminar paper "A Theory of Human Motivation". Wanasheria wetu wengi njaa na waoga.

You are spot on this. Novemba 2008 wakati kamata kamata ya watuhumiwa wa EPA ilipopamba moto kuna rafiki yangu ndugu yake aliwekwa ndani, manasheria walikuwa wanapigana vikumbo ofisini kwake kila mmoja kumshawishi achakuliwe kama mwanasheria wa mtuhumiwa! Kuna mwandishi mmoja huwa anawatania wanasheria rafiki zake kuwa ni "Scavengers of disaster". Wataongeaje wakati midomo yao imejaa "Chakula". Sio adabu ya kiafrika kuongea na chakula mdomoni.
 
Last edited:
Jibu ni rahisi sana, wanansheria wanaunganishwa sio kwa ridhaa yao wenyewe kama kundi la wanarsheria mawakili, bali kwa lazima kupitia sheia uliyotungwa na bunge wakati wa ukoloni. Sheria hiyo ilikuwa na nia ya kubana mawakili kwani serikali ya kikoloni iliona kuwa vuguvugu la uhru wakati huo lilikuwa linaanzia kwa wanasheria hivyo sheia hiyo iliyotungwa ili kuzuia wanasheria kuwa manaharakarti katika kudai uhuru.

Kama kawaida baada ya uhuru serikali ilisahau kubadili sheria za namna hiyo ambazo zipo mpaka leo. Sio hii tu pamoja na kuja katiba inayotambua haki za binadamu bado mawashewria wananshindwa kelewa kuwa nanayo haki ya kujumuika bila kulazimishwa na hivyo basi kufanya malengo ya sheria hiyo kuwa kwa manufaa ya masters waliobadilika ngozi kutoka wazungu kuwa waswahili wenzetu.

kutokana nahiyo basi msitegemee sana wanasheria wa tanzania watakuwa maacivists kama nchi nyingine. Vile vili discplinary body ya manasheria ni Jaji, Jaji yoyote anaweza kusimamisha wakili wakati wowote. Utaona basi mawakakili wa Tanzania wako very passive. Angalia Kenya, Pakistan, Uganda etc mawakili wanafanya wonders sio hapa kwetu.

Kila siku naimba tubadili sheria zetu, vidole vinasagikana kupata na kupata sugu kwa ajili ya kutype views na comments and nothing happens and nothing will happen kama sheria ni hizi tulizonazo.
 
Back
Top Bottom