Swali la Tundu Lissu linakosa mjibuji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali la Tundu Lissu linakosa mjibuji?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mnyamahodzo, Aug 31, 2009.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mjibuji=>mtoa jibu.

  Ni miezi mitatu sasa tangu mwanasheria? Wakili Tundu Lissu alipouliza swali la msingi kama televisheni ya ITV.

  Ilikuwa ni tarehe 30/05/2009 katika kipindi cha Kipima Joto, kinachoendeshwa na Alfred Masako, mada ikiwa VITA DHIDI YA UFISADI JE, WANACHI WANAHUSISHWA KWA UKAMILIFU? (kama patakuwa na dosari katika kichwa cha mada basi ni ndogo, lakini ndiyo maana ya kimuktadha ya mada iliyojadiliwa) miongoni mwa washiriki wa kipindi hicho ni Tundu Lissu na Ananilea Nkya.

  Akiisha kuchangia kwasehemu kubwa katika mada hiyo Lissu alisema" Ni swali ninalojiuliza sana, mara nyingi, hata sasa ninajiuliza ni kwanini Baraza la Mawakili limekuwa kimya hadi sasa juu ya tuhuma za ufisadi? Masuala ya EPA, Richmond, Kagoda yanatajwa wako kimya.Hawajatoa tamko wala kuchukua hatua ...Kenya na sehemu nyingine duniani ni forum hiyo ya mawakili ndiyo iliyoibia mambo makubwa na kuponya wizi wa mali za umma...... Ukimya huu wa baraza la Mawakili dhidi ya ufisadi hadi sasa unasababishwa na nini?"

  Swali ninalojiuliza hivi kwanini swali hilo alilouliza Lissu linakosa mtu wa kulijibu katika baraza hilo?
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mambo ya "Maslow Hierarchy of Needs" as detailed in the seminar paper "A Theory of Human Motivation". Wanasheria wetu wengi njaa na waoga.
   
 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Waliwahi kusema ndani ya Baraza la Wawakilishi kwamba, "matatizo ya ufisadi yako bara tu, haywahusu watu wa Zanzibar", lakini kuna matukio makubwa yanayohusu ufisadi ndani ya SMZ na ndani ya vyama vikuu vya siasa visiwani Zanzibar. Yanajulikana na wana JF watasaidia kuchangia humu. Hii ni changamoto kwa CUF ambao ndio wanaotakiwa kuibua mijadala kuhusiana na matatizo ya maadili huko Zanzibar. "Haki sawa kwa wote" lazima iwekwe kwa vitendo na mijadala ianze kuhusiana na ukwepaji kodi unaofanywa na vigogo wa Zanzibar, ukusanyaji mapato ya watalii wanaoingia Zanzibar kwa makundi!! Makampuni ya mafuta? na kodi nyinginezo.
   
 4. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,722
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Mkuu Halisi
  Ni wawakilishi au mawakili? Ebu jaribu kuangalia vizuri alichoandika mtoa mada.
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu njaa wanaogopa kuwakoma usoni kwa vile wanawalea na wanagongana kwenye kumbi za starehe inakuwa ngumu...fadhira mazee.
   
 6. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu, siyo Baraza la wawakilishi ni Baraza la mawakili(hawa ni wanasheria na si wanasiasa labda kama wanaamua kuingia huko).

  Kwenye nyekundu, ni kuongezea kuwa kuyashughulikia masuala haya hadi kukata mzizi wa fitina na watu kuishi kwa furaha hakutegemei chama chochote cha siasa ikiwa wanasheria watalala au kuwa kimya kama mbwa-koko (sivyo walivyo kwasasa, walakini wakinyamaza mwongo mzima twaweza fikiri hivyo).

  Wanazijua vizuri sheria gani za kusimamia kuwashitaki wahusika(watu binafsi) na makampuni yao. Tulio maamuma tunasubiri jitihada yao. Wenye njaa wakichoka, naogopa kuwa watachukua mawe, mikuki na silaha yoyote ya karibu kujilipizia kisasidhidi ya hao wezi halisi(mafisadi) na mali zao au jamaa zao. Sina uhakika kama itakuwa ni njia sahihi kurejesha mali walizoibiwa.
   
 7. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nimeteleza naomba radhi nadhani swaumu imepanda
   
 8. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nashukuru kwa kunizindua!! ama kwa yale uliyoweka msisitizo. Tuko pamoja.
   
 9. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ni aibu kubwa kwa wanasheria hawa kujitamba kuwa wao wanapesa na wanakula jasho la kazi waliyosomea kumbe WANALELEWA, Duh!! Kwahiyo nikimwona kidume katika fani hii na kiongozi wa forum hiyo nijue yeye (na familia ) analelewa na kidume fisadi mwingine? Mmhh!!

  Je! Kuna uwezekano mkubwa viongozi wa forum hiyo kuwa walilambishwa rojo ya tende ndiyo maana wanatafuta kila namna ya kulipa fadhila ikiwa ni pamoja na kuwa mabubu?

  Mkuu nijuvye zaidi kinaga-ubaga.

  Ni maswali, maswali maswali tu.
   
 10. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mawakili na wawakilishi mtu anaweza kusema ni hao hao tu, na hili linaweza kuwa msingi wa kuchanganya huku.Kimsingi wote wanachukua dhamana za kuwawakilisha wengine katika vyombo vya kutunga na kutetea sheria, kwa hiyo hii outrage kuwa extended kwenye baraza la wawakilishi ni fair kabisa.inawezekana originally outrage ilikuwa kwa wanasheria, but the bigger picture involves the entire civil society, ambayo inajumuisha si mawakili, wawakilishi wabunge mahakimu na majaji tu, bali pia watumishi wa serikali, wasanii, professionals etc.

  Kama walivyoshindwa mawakili kukemea hili, wawkilishi wameshindwa. Pengine wawakilishi wanaweza kusemwa kwamba wameshindwa vibaya zaidi kwa sababu wao wapo katika nafasi ya kuchaguliwa na wananchi.
   
 11. S

  Simoni Member

  #11
  Aug 31, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jibu lake ni kuwa utamaduni wa nchi yetu na ambao kwa kweli unaonyesha hata national character yetu ni kuwa sisi ni taifa ambalo ni mafisadi tolerant. Kwa nini kwa sababu watu wengi wamekata tamaa na hao mawakili hawana ubavu wa kupiga kelele kwa sababu hawana moral authority. Katika viongozi tuliokuwa nao nchi hii ambao walikuwa na moral authority ni Nyerere na Kawawa. Akina Slaa, Mwakyembe, Lembeli? Si lolote isipokuwa ni political rhetorics. Hakuna kitu hapo. Ndiyo maana hata wito wa maaskofu na kina Pengo et al hakuna atakaewafuata.
   
 12. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Wakuu wa JF wakati tunaendelea kulijadili hili naomba msaada huu ili tuoanishe ukimya wa forum hiyo na uongozi walionao. Naomba msaada wa majina ya viongozi wakuu;Mwenyekiti(Raisi),Makamu wake,Katibu na Mtunza hazina.

  Tabia za viongozi huwa zina-determine ufikiaji wa malengo ya jamii husika.
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Amini amini nakuambieni kwamba hawa mawakili wetu wanaponzwa na njaa. hebu fikiria mtu kasotea uwakili kwa miaka zaidi ya kumi na akipewa ananong'onezwa kwamba amepata kwa fadhila unadhani atajiweka kitanzi shingoni endapo aliyempa fadhila atafisadika??

  Inahitaji ujasiri wa kizalendo. sana sana utakuta wanawafanyia kazi mafisadi kwa mlango wa nyuma. angalia jinsi nyaraka za makapuni yaliyochota EPA yalivyopaliliwa na busara za mawakili....

  Siwatuhumu ila ndo inavyoonekana kwani wapo kimya wanasubiri kupangiwa kesi mahakama kuu wapata ulaji wao...
   
 14. Sungi

  Sungi Senior Member

  #14
  Aug 31, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna maswala mengi ya kuangalia kitaalamu katika prosecution. Haya makosa yanakuwa alleged in ya jinai, na kwa hiyo yanatakiwa kuendeshwa na serikali kwa kupitia Director of Public Prosecutions (DPP). Kama ni ya madai (civil) kuna maswala ya kutazama, kama "locus standi" yaani kama wanaofungua shauri wana haki kisheria ya kuyafungua - "standing". Haya "madai" yanaweza kufunguliwa kama "public interest litigation" ambayo inampa mtu yeyote "locus standi".
  Mimi sikuangalia huo mjadala kwenye television, lakini sijui ndugu yangu Lissu alikuwa anamaanisha nini kwa "baraza ya mawakili" nadhani ni Tanganyika law society kwa bara.
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Jamani mimi nimeshuhudia mkoani tanga wakili wa utetezi, mawakili wa serikali, hakimu wakijiburudisha kwa bata na mnvinyo baada ya kesi kumalizika na serikali kushindwa. Sasa sikujua walikuwa wanapongezana kwa serikali kushindwa au?
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwa kifupi hakuna sekta iliyo gubikwa na rushwa kama ya sheria. Mawakili wengi wanakula rushwa na serikali inajua hilo, kumbuka wakati wanafunzi wa uhandisi wamefanya vurugu pale UDSM mawakili karibu wote waligoma kushughulikia kesi ya wale vijana.

  Ukichunguza utagundua mawakili wengi wanajua kuwa hata serikali injua wanakula rushwa kwa hiyo hawawezi kupia kelele yoyote kuhusu ufisadi. Kumbuka tu issue ya malegesi, haya Masha mwenyewe rushwa tupu na anatuhumiwa kampuni yake ya uwakili kwa kudhulumu mirathi ya mama wa Kamanga ferry n.k.
   
 17. M

  Magezi JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Fikiria Dk. ringo tenga alivyokuwa wakati wa NCCR-Mageuzi, kumbe ilikuwa ni njaa. Amehusika sana ktk kushughulikia pesa za EPA na nadhani na yeye anatakiwa kuchunguzwa. Alitamba kweli kama wakili mahili lakini leo yuko mifukoni mwa mafisadi na hafurukuti, leo umwambie akemee ufisadi wakati yeye mwenyewe ni fisadi na 1.

  Hii nchi ni kula kwa nafasi yako, lakini siku vijana wa kaboya wakicharuka nchi itagawanyika vipande.
   
  Last edited: Sep 1, 2009
 18. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kwa kushirikishwa kunatafsiriwa vipi? Kama kuna mtanzania leo atasema hajashirikishwa sijui anataka apewe nini au afanyiwe nini ili ajione kuwa ameshirikishwa. Wakuu tukipewa information ni lazima tuangalie tunatumia hizo information vipi, it is up to us to decide how to deal with them.

  Siku Slaa, Lipumba, Mrema, Mbowe etc waliposimama Mnazi mmoja na kutuambia kuwa mafisadi ni hawa, walisema wameamua kuwapekelea wananchi suala hilo. Wananchi ni pamoja na wanasiasa, waandishi wa habari, bloggers mawakili, wanasoka, waumini wa dini mbalimbali, wafanyabiashara na wengine wengi.

  Naona kama Lissu angekuwa na genuine question lingekuwa wao kama wanasheria wamefanya nini? Tumeona waandishi wa habari walivyofanya, tumeona wanasiasa walivyofanya, tumeona watu wa dini walivyofanya, bloggers as well, lakini hao mawakili tunaona wameplay negative role ya kuwatetea mafisadi mahakamani (ingawa ni kazi yao kisheria), sasa i wonder what Tundu Lissu wants.
   
 19. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Siku nilipoiona signature yake kwenye Mwanahalisi jinsi alivyowatambua "WEZI WAKUU WA MALI YA TANZANIA" nilichoka.
  Alikuwa anatamba nje na ndani ya vijiwe vya starehe kuwa ni mtu makini.
   
 20. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mawakili wananafasi ya kusimama na kusema badala ya wananchi(washitaki au washitakiwa). Katika maswala haya ya UFISADI-mbegu ya UHUJUMU UCHUMI, akizungumza mwanasheria mmoja-mmoja huenda isiwe na impact kubwa. lakini wakizungumza Baraza kwa tamko lililotolewa na viongozi wao impact yake itakuwa kubwa zaidi. Nafikiri hicho ndicho Lissu anachotaka wao kama watu wa sheria watoe tamko lao wakiongozwa na viongozi wao.
  Kama ni vinginevyo, kwakuwa naye ni msomaji wa JF, huenda akatujibu vizuri zaidi.
   
Loading...