Swali la Tafakuri: Kwanini CCM hawagongani kabla ya chaguzi ndogo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali la Tafakuri: Kwanini CCM hawagongani kabla ya chaguzi ndogo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 27, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nililiona hili wakati wa kampeni ya Igunga ambapo Rostam Aziz mmojawapo wa wanasiasa na wafanyabiashara wanaotajwa katika madai ya ufisadi alipoachia jimbo. Rostam aligongana na wana CCM kadha wa kadha na mgongano ulikuwa wazi katika hotuba yake ya kuwaaga watu wa Igunga. Ilitarajiwa basi Rostam angeshambuliwa sana na wanaCCM wenzake na hasa maadui wake wa kisiasa. Haikuwa hivyo; kampeni nzima ya Igunga kwa upande wa CCM ilikuwa imetulia na mtu asingeweza kuhisi tofauti yoyote ya msingi ndani ya CCM. Mgongano uliokuwa umedumu kwa muda mrefu ulizimika ghafla; hata hoja za kujivua gamba hazikusikika kwa namna ya kuwagawanya wana CCM isipokuwa kwa namna ya kuwaleta pamoja kuleta ushindi.

  Tunaliona hili tena Arumeru Mashariki ambapo mkwe wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Bw. Lowassa anagombea katika kile ambacho kinaonekana kuwa nguvu "kubwa" ya Lowassa. Japo kulikuwa na maneno wakati wa kuelekea kura za maoni mara baada ya Sumari kupitishwa jitihada kubwa imefanyika ya kuhakikisha kuwa wale walioumizwa na wenye kuhisi kuonewa wanatulia kimya na kuonesha umoja wakati huu hadi ushindi. Na kweli kabisa tumewaona wakipanda majukwaani wote wakionesha umoja na Siyoi. Hatuwasikii kina Sitta, Mwakyembe au wana CCM wengine maarufu wakitumia muda huu kushambuliana.

  Kwa mpinzani yeyote wa Lowassa ndani ya CCM angeweza kutumia nafasi hii kuhakikisha kuwa Lowassa hapati anachokitaka na ihvyo kumpunguzia nguvu. Inawezekana kuna watu ambao wanafanya kisirisiri sana juhudi za kuvuruga CCM lakini kwa kila kipimo CCM imepatana sana na imeungana zaidi katika kutaka ushindi. Tofauti zao wameweka pembeni na wanaangalia Jumapili ijayo na watazifufua tofauti hizo baada ya uchaguzi huo. Ni wazi kabisa kuwa endapo CCM watashindwa tutashuhudia mgongano mkubwa, lawama na manung'uniko ya CCM lakini hatutasikia vitu hivyo sasa.

  Kimsingi CCM wameonesha kuelewa uzito wa kinachogombaniwa Arumeru Mashariki. Lakini tunaweza kujiuliza hawagombani kwa sababu hawana demokrasia? hawalaumiani hadharnai kwa sababu hawataki uhuru wa maoni? hatuwasikii viongozi maarufu vijana wa CCM wakitoka wazi kukikosoa chama chao kiasi cha kuonekana kukidhoofisha - japo wawez akuwa na sababu. Kwanini?

  Hili linarudisha swali kwa CDM na viongozi wake; kwanini wakati wa kuelekea hii kampeni ndio tunaweza kuona mashambulizi ya ndani na hata migongano ya wazi badala ya kuonesha umoja na uthabiti wa kunuia kushinda. NImesoma tangu juzi baadhi ya viongozi wa CDM wakijibishana kwenye mtandao huu huku kila mmoja akifikiri anafanya hisani kumtetea "mtu wake" wakati kwa kufanya hivyo wanasahau kuzungumzia CCM na sera zake na udhaifu wake! Nimesoma maandishi ya wengi ambao wanachambuana yanayotokea ndani ya CDM badala ya kuchambua yanayoendela ndani ya nchi kwa sababu ya kushindwa kwa sera za CCM.

  Ninabakia kujiuliza hawa viongozi wa CDM hawana uwezo wa kuona yale ambao wenzao wa CCM wanayaona? Kwamba, mnapokuwa vitani jukumu lenu ni kushinda vita kwanza halafu tofauti zenu za nani alale wapi, ale nini au afunge ndoa na nani na lini zinakuja baada ya ushindi. Think about it. Je, siku hizi chache zilizobakia tutaona ukimya ndani ya CDM kuonesha kuwa wana focus ya ushindi au watatumia muda ziadi kwa wengine kuja na kauli na maelezo zaidi ya kuwahamisha watu kutoka ushindi? Je, tutaendelea kushuhudia vijana maarufu na viongozi maarufu wa CDM wakitumia muda kuzungumzia mambo mengine yote isipokuwa haja ya kuishinda CCM Aprili Mosi?

  Hivi kweli CDM wakishindwa tunaweza kweli kuilaumu CCM na serikali yake kwamba imecheva vibaya. Itakuwaje kama tutaweza kuonesha kuwa aliyepiga ngwala ni mchezaji wa timu ile ile na aliyemsukuma golikipa hadi goli likafungwa ni beki wa timu ile ile?

  Naweka nukta nasubiri Aprili Mosi. Ili ama tunawapongeza kwa kushinda au kutaka uongozi mzima uwajibike kwa kushindwa; siyo mtu mmoja wa kulaumiwa bali WOTE. Hili liwe wazi mapema.
   
 2. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  CCM ugomvi ni kawaida kwa sababu kila mwanachama ana uhuru wa kutoa maoni yake popote pale, na maoni ya mwanachama siyo official statement ya chama. Sisi tunaelewa hilo.
  Kwa upande wa CDM, uhuru wa kutoa maoni haupo, kiongozi yeyote akiwa kinyume na Mwenyekiti au Katibu, basi kunakuwa na purukushani nguo kuchanika.
  Kwa mfano, Sitta kasema anaweza kugombea urais, sawa!
  Lowassa karudia kuhusu ukosefu wa ajira kwa vijana, sawa!
  Nape kamjibu Lowassa kiaina, sawa!
  Uchaguzi wa NEC kutohusisha wabunge, sawa!
  Rais/mwenyekiti kutobariki ongezeko la posho, sawa!!

  Kwa upande wa CHADEMA, Zito kamwambia mwandishi kuwa nikipata ridhaa ya Chama changu nitagombea urais.... you know the rest!
  CHADEMA hawaonyeshi demokrasia ya ukweli ndani na nje ya chama chao, mfano hata hapa JF, ambayo ni ya CDM utaona matusi yatavyofuata.
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,889
  Trophy Points: 280
  Mgongano wowote ni pale ambapo pande mbili zinapovutana kuhusu jambo fulani.
  Kama ni hili la Zitto na urais mimi binafsi sijawahi kuona wala kusikia popote Slaa au Mbowe wakisema kuwa wanautaka urais siku zijazo.
  Sasa mgongano unaouzungumzia ni upi???
  Viongozi waliovutana huku JF hawana majina????
   
 4. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Chadema ni mficha maradhi...
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Sasa kweli na wewe unaamini JF ni ya CDM? duh! Alichosema Sitta wala hakiwatishi watu kihivyo wala majibizano ya Lowassa na Nape hayahusiani hasa na kudhoofisha CCM. Kama unakumbuka baada ya kura za maoni kulikuwa na wito wa wazi kabisa wa wanaCCM kuwa pamoja na kumuunga mkono Siyoi. Husikii wale walioenguliwa - hata kama wana manunguniko - wakijitenga na kampeni au kufanya mambo ambayo yangemdhoofisha sana mgombea wao. Ni kwanini umoja huu katika kutafuta ushindi wakati watu wanatofauti za msingi sana na hata za kibinafsi?
   
 6. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Kobello naona hujamwelewa Mwanakijiji vizuri, swali ni kwanini sasa hivi?? Why now? Hayo unayosema kuhusu demokrasi ndani ya chama may be debatable but why now?

  Kama ni Slaa kukaa na Josephine hajaanza baada ya kifo cha Sumari! Kama ni pesa za Sabodo hazikuahidiwa baada ya kifo cha Sumari. Na huyu Zitto alipokuwa akitetea hoja ya umri wa kugombea urais kushushwa, alisema hiyo haitakuwa kwa ajili yake, hana mpango wa kugombea... But why is he bringing the party in disrepute right now? Angalia magazeti ya mwananchi siku mbili hizi, it's all Zitto Zitto Zitto....

  The point is kuna mambo yanaweza na muda mwingine yanapaswa kusubiri, hatuangui kilio kwenye harusi kwa sababu kuna mbuzi mmoja kapotea bandani, maliza harusi ukamtafute. Ndio maana watu wanaanza kuhisiwa vibaya kwa mambo kama haya.
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,889
  Trophy Points: 280
  Ina maana hapo kwenye red ulitaka Zito apewe ridhaa na chama gani kama sio chama chake.
  Demokrasia ya CCM ndo ile ile iliyomuua Kolimba?
  Demokrasia ya CCM ndo ile ya hujuma dhidi ya Sitta kuwa spika?
  Demokrasia ya CCM ndo ile inayomuumiza mwakyembe kwa sumu?
  Demokrasia ya CCM ndo ile ya kumpinga kwa nguvu na matusi Lowasa kuhusu bomu la ajira linalokaribia kulipuka?

  CCM wanajitekenya wenyewe na kucheka wenyewe.
   
 8. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,889
  Trophy Points: 280

  Hapo Arumeru CCM wanajinadi kwa kusema kuwa ni chama kilichozalisha ajira nyingi kwa vijana, at the same time Lowasa anasema tatizo la ajira ni bomu linalotegemewa kulipuka punde.
  Kwa kutumia akili ndogo tu ya darasa la nne utagundua kuwa kuna mgongano wa hoja ambao unanafasi kubwa ya kupunguza kura za CCM arumeru.
  Analysis ya kusema eti CDM wanamgongano kipindi cha uchaguzi mdogo na CCM hawana inahitaji uchambuzi wa sera ambazo zinagongana na sio kukariri.
   
 9. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  MM uliyoyasema lakini naweza kusema kwamba CDM kinakuwa siku hadi siku iendayo kwa mungu na kikiwa kwenye process hiyo kunakuwa na changamoto, mimi ninavyoona kunatatizo la uwajibikaji wa pamoja wa viongozi na hii inatokana na makundi yaliopo ambayo wasipo lifanyia kazi na kuwekea mkakati nadhani mbeleni hali itakuwa mbaya sana na huenda ikwa kama ccm tunayoikosoa kwa kuwapo kwa makundi.

  Uwepo wa vijana wengi ni azina ndani ya chama lakini mara nyingi vijana wanakuwa na matarajio makubwa na wanataka yafanyike kwa haraka hali hivyokupelekea wakati mwingine kukosa uvumilivu inapofika wakati wa uchaguzi unakuta joto linapanda zaidi na ndiyo haya yanayojitokeza.

  Jambo lingine ni ndani ya chama kuwa na mamluki au wapita njia ambao wakopale chadema kwa mapenzi bali kwa sababu za ubinafsi wakuisikilizia upepo wa chadema ukiwa mzuri wanajifanya wanamapenzi na chama lakini hali ikiwa tofauti wanaanza fitna.

  Chakufanya ni nini,

  Chama kiwe nataratibu ya uwajikaji wa pamoja, kuwa na kitengo cha kiitelejensia za kufuatilia waliopo ndani ya chama cha kuatilia nyenendo za waliopo ndani za chama kuwahoji na kuwa mfumo wa ukosoaji wa chama.
   
 10. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kabello, siamini kama kweli CDM hakuna demokrasia. Kiukweliingawa CDM inavijana wanasiasa wengi na walio makini ila bado hawajapata uzoefuwa kubaini yatokanayo kwa wanayoyaongea/yafanya kwa wakati gani na nafasi zaokatika jamii. Tunajua wanamaanisha wanayoyasema, tunajua wanauwezo mzuri na niazao, na ni kweli wengi wanamvuto si ndani ya chama tu bali pia wanakubalika najamii. Lakini pamoja na yote haya, ni vizuri pia wakatumia taratibu za kichamakwani ndicho kinachowabeba. Ikitokea kukawa kuna watu zaidi ya mmoja wanatakawadhifa fulani na kutangaza hadharani, basi ni wazi kunauwezekano wa kuwagawawanachama ikiwa wote wanakubalika. Ndiyo maana ni vizuri kutumia vikao vyachama na washauri wao kuweka mambo yao vizuri ili waweze kuweka mshikamanokatika chama na kujijengea imani kwa jamii yote. Ikiwa ndani ya chamahayakufanyika kidemokrasia, basi wanachama na jamii tunahaki ya kuelewa nakuweza kuhukumu kwa njia yoyote inayofaa.
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mwanakijiji, ni vigumu sana kwa 'CCM" hivi sasa kugombana kwa sababu watagom,bania nini wakati hawa waili ndio wenye chama? wanachokitaka wao, ndicho kinachokua. Ugomvi unaweza kuibuka iwapo tu watatokea watakaowapinga ndani ya 'CCM'. Lakini kwa bahatyi mbaya, hao hawajatokea bado
   
 12. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hapa panaitaji mjadala mpana sana vinginevyo tunavyokwenda uko mbele ya safari CDM itadondokea pua humu humu!Kwa kuwa lisemwalo lipo kama alipo laja.
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Una ushahidi na hili?
   
 14. P

  Paul S.S Verified User

  #14
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  What should I say more?
  nice shot mkuu
   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Mamluki hawakosekani kila mahali, mtadhani mko pamoja kumbe mko page tofauti kabisa.

  'si kila wasemao Bwana Bwana wataona ufalme'

  Everyone has a price, the problem is to know what it is, labda kuna mtu keshafika bei mahali fulani.
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Nilidhani jf ni platform ya watu wote kutoa mawazo yao sababu ni 'user generated content' website.
  Hebu nieleweshe nisipoteze nguvu na akili mapema.

   
 17. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 618
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  UKOMAVU. kwenye maisha kunakukomaa kiakili na kukomaa kimwili. CCM wananjia nyingi sana za kuwakomaza watu wao kisiasa. CDM mtu anatoka kijiweni na mahaba ya chama anapewa ukatibu wa wilaya. Ofisi ya Taifa imejaza wapenzi wa chama lakini ambao hawajakomaa kisiasa.
  NJAA. Lengo la maisha ni kila kiumbe kuhakikisha kinaishi. CDM imejaza waganga njaa na ma-opportunists. Wengi bado wako hatua ya awali ya kutafuta mkate wa kila siku. Ni rahisi kwa wao kupandikizwa na CCM lakini ni ngumu kwa CDM kupandikiza mtu ndani ya CCM.
  WAHAMIAJI. Mimi si mfuatiliaji sana wa siasa za nje lakini ukiacha nchi chache ambazo zilipractise multiparty democracy mara baada ya kujikomboa, nchi nyingi tafsiri ya upinzani ni watu waliojiengua kutoka chama tawala. Mfano wa karibu ni wa kenya ambako wapinzani karibu wote tunajua kwamba walikuwa ni wanachama wa KANU. Labda CDM inahitaji kuvuna wazoefu kutoka CCM(isahau mwiba wa SHIBUDA) waje wachanganye na wazoefu waliowakuta ili kujenga chama imara chenye umoja.
  UMOJA. CDM bado inapambana kujitanua. CCM imekuwa huu ni mwaka wa 35.lakini ukijumlisha na wakati wa TANU hapa tunaongelea miaka 58. inamaana CCM imekuwa na miaka 58 ya kujikosoa na kujirekebisha. CDM haiwezi subiri mda huu wote. CCM ilijijenga kwenye umoja huku ikibomoa na kujenga bila upinzani. LEO CDM inabidi kubomoa na kujenga huku ikiwa inaandaliwa anguko! CCM wana chuo chao cha kusomeshea wanasiasa wao. CDM utajifunza mtaani kadiri mambo yanavyoenda. Inachukua mda mrefu sana kujenga umoja na mda huo utazidi kadiri mapambano yanavyozidi. CDM BADO INAJENGWA KUFIKIA UMOJA WA KITAIFA ARUMERU MASHARIKI SIO KIPIMO BADO CHA UONGOZI KUJIHUDHURU. TUWAPE MDA!
   
 18. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 618
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Unajua mojawapo ya maendeleo ya nchi ni kupractise ukweli. tukikataa ukweli haitutofautishi na mafisadi. Uongo pia ni ukweli. JF imetekwa na mashabiki wa CDM zaidi. Ukiwa na mawazotofauti lazima utaitwa gamba. Wengi humu ndani hawaamini kwamba KUNA WATU TUNAICHUKIA CCM KULIKO TUNAVYOIPENDA CDM. sasa ukija na wazo mbadala ni matusi na kashfa. Infact this is the bad part of CHADEMA PSYCHOS!

   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,600
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Mpaka mtei hajamuelewa zito..bahati mbaya au makusudi?? these people suck
   
 20. N

  Ntuya Senior Member

  #20
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CHaDEMA kitadumu katika mazingira yoyote, haya yote tunayoyaona ni changamoto ambazo kwa vichwa vilivyopo CDM yatapata ufumbuzi maridhawa bila tatizo. So everyone calm down, everything gonna be alright, cha msingi tutafakari ufumbuzi wa changamoto hizi.
   
Loading...