Ha ha ha! Duh!Yaani badala ya kuuliza kwa mfano ni lini Serikali itafanya tafiti kuthibitisha huo upupu alioambiwa salon wakati yupo kwenye "drayaa" japo bado ni swali la kipuuzi, anauliza kabisa ni lini zitapigwa marufuku kuingizwa Nchini. Hii kiwango cha ujuha ni cha juu mno. Aibu yetu.
Mbunge wa kuteuliwa Mama Salma Kikwete katika kipindi cha maswali na majibu ameuliza kuwa, Kwa kuwa matumizi ya headphone za simu sinasababisha ukiziwi,je ni lini serikali itapiga marufuku uingizwaji wa headphone nchini?
Naibu Waziri amejibu hakuna utafiti wa kisayansi unaoonyesha headphone zinaleta ukiziwi
My Take
Maswali haya huandaliwa miezi kadhaa na kutafutiwa majibu. Inashangaza mbunge kutumia rasilimali za nchi kuandaa maswali kama haya. Nashauri unapokuwa huna swali omba nafasi yako itumiwe na kina Tundu Lissu, Hussein Bashe, Mnyika wasaidie nchi isonge
Tatizo ni mfumo ulomruhusu kuja bungeni.Msimlaumu maana inawezekana ndo mwisho wa kufikiri kwakwe
Sasa hilo ndio lilipaswa kuwa swali. Tatizo ali-conclude as if kwamba kuna utafiti ulishafanyika.pengine yupo sahihi lakini hajaliuliza vizuri, Headphone zile za Monster, Beats, AKG na brand zinazoaminika duniani zinaweza zikawa hazileti ukiziwi, je hii mikopo yetu tunayoitoa china imethibitishwa kuwa haidhuru afya yetu? mamlaka husika wanazikagua?
mke wa mstaafu.huku ccm tuna utaratibu wa kulipana fadhila ukishaondoka madarakani.Bado sijaelewa alipewa ubunge kwa kutumia vigezo vipi. Shame
mwingine huyu hapaBavicha bhana mbona hamshangai walio wai pendekeza kuzuiwa kuingizwa piki piki kuthibiti ajali...
Na mzee wa chato akashindiliaHuyu ndiye aliyepeleka hoja za kufukuzwa kwa watoto wa kike waliopata mimba shuleni...!! Poor u
Sent using Jamii Forums mobile app
Wakiwezeshwa wanaweza! As simple as that bila kuzingatia vigezo na masharti MUHIMU ya kuwezeshwa huko.