Swali la lazima kwa Wana-CCM: Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge si mafisadi (magamba)?

Walisemwa sana. Kwasasa wananchi wananong'ona chinichini kuwahusu. Urafiki na Serikali iliyopo madarakani unaimarika siku hadi siku. Kila mahala wanapokuwepo na kila maneno wanayoyasema, wanaisifu Serikali kadiri ya uwezo wao. Serikali hii ni ile ile iliyoingia ikijipambanua kuwa iko kwenye vita dhidi ya mafisadi. Rais huyu ni yule yule anayeuchukia ufisadi chamani na Serikalini.

Rostam, Lowassa na Chenge wako ndani ya CCM muda huu. Wako ndani ya chama 'kinachochukia' wizi na ufisadi. Wapo ndani ya chama kinachounda Serikali iliyo kwenye vita dhidi ya ufisadi na wizi chamani na Serikalini. Rostam, Lowassa na Chenge walipachikwa jina la 'Mapacha Watatu' chamani wakati ule wa Rafiki yangu Wilson Mukama.

Kutokana na mtiririko na historia yao chamani, Rostam, Lowassa na Chenge ni mafisadi au si mafisadi? Makada wa CCM tunapaswa kulijibu swali hili bila aibu wala woga. Nguvu waliyonayo chamani isifanye tumuache Rais na Mwenyekiti wetu ajongeane na 'mafisadi' hawa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Sombetini, Arusha)
jUZI MBUNGE MSTAAFU WA IGUNGA ALITAMKA MANENO KUNTU SANA...AMERUDI KWA SABABU MAZINGIRA YA KUFANYA BIASHARA YAMEBORESHWA! HAMKUMWELEWA...MAZINGIRA YALE ALIYOKUWA ANAFANYIA BIASHARA ZAKE SASA YAMERUDI TENA MNAJIULIZA NINI!
 
Kwa sasa ukiwagusa hao watu unaweza kujikuta unafukuzwa uana chama wako
Walisemwa sana. Kwasasa wananchi wananong'ona chinichini kuwahusu. Urafiki na Serikali iliyopo madarakani unaimarika siku hadi siku. Kila mahala wanapokuwepo na kila maneno wanayoyasema, wanaisifu Serikali kadiri ya uwezo wao. Serikali hii ni ile ile iliyoingia ikijipambanua kuwa iko kwenye vita dhidi ya mafisadi. Rais huyu ni yule yule anayeuchukia ufisadi chamani na Serikalini.

Rostam, Lowassa na Chenge wako ndani ya CCM muda huu. Wako ndani ya chama 'kinachochukia' wizi na ufisadi. Wapo ndani ya chama kinachounda Serikali iliyo kwenye vita dhidi ya ufisadi na wizi chamani na Serikalini. Rostam, Lowassa na Chenge walipachikwa jina la 'Mapacha Watatu' chamani wakati ule wa Rafiki yangu Wilson Mukama.

Kutokana na mtiririko na historia yao chamani, Rostam, Lowassa na Chenge ni mafisadi au si mafisadi? Makada wa CCM tunapaswa kulijibu swali hili bila aibu wala woga. Nguvu waliyonayo chamani isifanye tumuache Rais na Mwenyekiti wetu ajongeane na 'mafisadi' hawa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Sombetini, Arusha)
 
Wapo ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI.
itoshe tu kuiogopa sana ccm maana wanakumbatia mafisadi
[QUOTE="...Kutokana na mtiririko na historia yao chamani, Rostam, Lowassa na Chenge ni mafisadi au si mafisadi?"

IJAPOKUWA MIMI SIYO KADA WA CCM (NA SINA MPANGO WA KUWA KADA WA CCM) NINASHAWISHIKA KUKUJIBU, NA JIBU LANGU NI HILI "ROSTAM, LOWASSA NA CHENGE SIO TUU MAFISADI, BALI NI MAFISADI PAPA"
 
Wakati hayo ya muungano wa "VIGOGO PAPA" yakitokea,na yule DAKTARI SILAHA yupo huko huko au unaweza kusema yuponao yeye akiwa kama MJUMBE wa nchi ughaibuni.
 
Tukitoka huko tumuulize mpiga TUMBA maarufu vigezo alivyo tumia kumrudisha Lowasa ndani ya ccm
Tumuulize dj mbowe alipompa Lowassa kugombea urais kwa tiketi ya chadema alikua fisadi au si fisadi , naomba majibu.
 
Ehe! Walilaumiwa halafu wakafanya maamuzi yao kwa mazingatio yapi? Fisadi au si fisadi?
Kuhusu Lowasa, alisema mwenyewe kwamba alifanywa kuwa mbuzi wa kafara, kulinda mafisadi wa CCM. Na ndio maana maskandali mengi tu yaliendelea kufumuka long time baada ya Lowasa kujiuzulu. Lowasa alisema wazi hata kwenye kikao kwamba alijiuzulu ili kumlinda Rais. na hata Mwakyembe alisema kuna mambo wameyagundua na wameamua kuyaacha yalivyo. hayo ni historia inajulikana.

Sasa shida ni kwamba CCM mliendelea kusema kwamba Lowasa ni FISADI. sasa kama hiyo ndiyo imani yenu, inakuwaje mmewapokea hao mafisadi wote?????
 
Mwalimu aliondoka na CCM yake maskini, hili lilikopo ni kundi la wanyang'anyi
 
Kuhusu Lowasa, alisema mwenyewe kwamba alifanywa kuwa mbuzi wa kafara, kulinda mafisadi wa CCM. Na ndio maana maskandali mengi tu yaliendelea kufumuka long time baada ya Lowasa kujiuzulu. Lowasa alisema wazi hata kwenye kikao kwamba alijiuzulu ili kumlinda Rais. na hata Mwakyembe alisema kuna mambo wameyagundua na wameamua kuyaacha yalivyo. hayo ni historia inajulikana.

Sasa shida ni kwamba CCM mliendelea kusema kwamba Lowasa ni FISADI. sasa kama hiyo ndiyo imani yenu, inakuwaje mmewapokea hao mafisadi wote?????
Mkuu mindi usipate shida saana kujieleza , swali ni jepesi tu, na jibu lake halina mzunguruko kama wa msamvu ,je ni fisadi , gamba au fisadi papa.
 
Back
Top Bottom