Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,735
- 40,858
Kuna baadhi ya watu wameshtushwa, wengine wameshangazwa, wengine wako katika hali ya kuzidi kumshangaa Magufuli na wengine wakiamini amefanya kile ambacho hawakukitarajia. Binafsi najiuliza, hivi inawezekana wapo kati yetu ambao ni kweli wana kumbukumbu ndogo hivi? NI jambo gani ambalo limefanyika la kuwafanya watu waachwe makanwa yao wazi kwa mshangao?
Mbona Magufuli alisema kabisa kitakachotokea na wengine tulijua kitatokea na tuliombea kitokee? Mtu alishawaambia tena hadharani kabisa kuwa wasaliti ni wabaya kuliko wachawi; na aliwasema wazi mbele ya Kikwete? Hivi walidhani anawatania, au hajamaanisha au ndio walikuwa wanaombea na kufunga kama watu wanaoombea kila mwaka na kufunga kuwa mvua ikinyesha yasitokee mafuriko Jangwani?
Binafsi kilichonishangaza ni jinsi watu walivyoliwa timing? Ni kwamba watu walijisahau kabisa? Kilichotokea nitakitolea maoni vizuri tu lakini mtu mzima anasoma alama za nyakati. Kwanini wanasiasa wengine tena wakongwe kama kina Sofia Simba, Madabida na wengine hawakuzisoma alama za nyakati.
Wapo waliosema "ulipo tupo" lakini mwenzao alipoondoka hawakumfuata. Sasa si wamelazimishwa wawepo? au walitaka wawepo kama hawapo wakati wapo? Binafsi sidhani kama kuna miongoni mwa waliofukuzwa uanachama ambaye anaweza kusikitika kuwa kaonewa. Sijui. Na wale wengine waliobakia... well.. shoka limewekwa kwenye shinani...