Swali la kufikirisha: Rais Magufuli, lifikirie hili kwa makini: unawawekaje watu ndani mwaka 1 hadi miaka 3, na kesi bado inachunguzwa!!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,315
24,178
Najua Dr Magufuli ni muumini mzuri tu wa dini.

Biblia ina kanuni(sheria )kumi za Musa, wengi tunazishindwa hasa ile sheria ya sita!!!

Lakin katika sheria zote kuna sheria kuu mbili.

1. Mpende Mungu wako kwa uwezo wako wote na akili zako zote

2. Mpende jirani yako kama nafsi yako

Sheria ya kwanza katika hizi mbili haina utata, ingawaje kuna wanao amini katika ushirikina. Roho Mtakatifu anawafuatilia.

Hili la pili ndo gumu. Mtendee mtu(jirani yako) kama utakavyojitendea nafsi yako.

Sasa nauliza, hivi mtuhumiwa wa wizi, ufisadi,uhujumu si haya ni makosa dhahiri?
Na adhabu zake ziko wazi.

Tumeona kesi ya mtu mmoja dhidi ya Waziri mwandamizi, akituhumiwa kutaka kumhonga.
Kesi ikatupiliwa mbali kwa vile ilikuwa ya hisia na hakuna ushahidi wa kutoshelezea.

Kuna watu kadhaa wamewekwa ndani(Remand Prison), wengine kwa miaka inaelekea mitatu.

Tunatenda haki gani kama hakuna ushahidi, bali hisia?

Nina uhakika watu hawa wanapiga magoti kila usiku wakienda kulala, kumwomba Mungu aziguse nafsi zilizowaweka huko Rumande.

Tuelewane hapa, mimi siwatetei mafisadi, wezi au wahujumu.

The best political move ni kutaifisha mali ambazo wahusika ambazo wamezipata kwa matendo yao yenye kutilia mashaka.

Kuwaweka watu ndani kwa hisia, kukomesha, kulipiza kisasi au kwa kuonea tu, hakika ni dhambi juu ya uso wa dunia na mbingu.

Tulifikirie kwa makini hili tunapomaliza mwaka 2018.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Naunga mkono Hoja
Hili la watu kukaa mahabusu muda mrefu bila Kesi kutamletea a bad karma na nilizungumzia hapa

Magufuli is Getting Better and Better, He is Changing for The Better!. Hongera Sana!. - JamiiForums
Nimesema

Wanabodi
Nimemuona akihutubia kwa humility na genuinity, hivyo mnaweza kushangaa akasimamia kuhakikisha ofisi ya DPP inatenda haki kweli na haki ikaonekana inatendeka, hivyo wote wanaoozea kwenye mahabusu za nchi hii wengine kwa zaidi ya miaka 7 kama wakili Medium Mwale, na wale wanaozea Keko, Ukonga, Segerea na mahabusu nyingine kama kina Harry Kitilya, Sioi Sumari, Shose Sinare, Isaack Kasanga, Gonzaga, James Rugemalila, Jamal Malinzi, Dr Ringo Tenga, wale Ma Sheikh wa Uamsho na wengine wengi, wanatendewa haki, na haki kuonekana inatendeka!. Kuna watu wanaoshitakiwa kwa makosa ambayo ukikutwa na hatia adhabu yake ni kifungo cha mwaka mmoja jela, lakini mtu yuko mahabusu mwaka wa 7 sasa na kesi haijaanza kusikilizwa!, huu ni uchunguzi gani ambao haukamiliki, na hii ni haki ya aina gani inayocheleweshwa?!.

Huwezi jua, kufikia 2025, President Magufuli might end up being the best president, this country had ever had, na sisi Watanzania katika umoja wetu, tukamlilia aendelee na kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza katiba ibadilishwe, kipengele cha ukomo kiondolewe!.

Hongera sana rais wetu Magufuli, you are changing for the better!.
Big up!.

Viva Magufuli!.
Viva Tanzania!,
Mungu mbariki Magufuli, Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
Rejea
Rais Magufuli Akifanya Mazuri, Apongezwe: Hotuba Yake Kuzima Mwenge, Ni One of The Best! - JamiiForums
Tusilalamike Tuu, Kulaumu na Kulaani Kila Kitu, Kwenye Mazuri Tupongeze, Rais Magufuli is Changing For The Better!. - JamiiForums
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . - JamiiForums
Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?!. - JamiiForums
P
 
Naunga mkono hoja,

Pia tuzingatie juu ya matabaka yaliowazi baina yetu Raia/Viongozi hivi sasa nchini. Ni jambo ambalo lipo wazi kabisa, na linafanyika bila pazia (Matabaka; Walio bora, na wasio bora. Wanaokosea, na wasiokosea. Wenye sauti, na wasio na sauti. Wenye vyeo, na wasio na vyeo).

Kuna baadhi ya watu/viongozi wanafanya makosa ila yanafumbiwa macho, ilhali makosa ambayo hata raia asiekua na elimu ya Form 2 anabakia kushangaa, ila makosa hayo hua yanafumbiwa macho na wakubwa kwasababu zao binfsi.

Wakati kuna watu wengine wakifanya hayo hayo makosa, basi atawekwa ndani kwa masiku/miezi/mwaka kama sio kufukuzwa kazi kama mnyama (mbele ya hadhara, bila stara yoyote wala kupata nafasi ya kujitetea, kama sheria inavyotaka). Bila kuzingatia huyo mtu ana familia, ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi wenzake wanaomtegemea kama sio kumpenda kwa dhati.

Tunasikia vilio vya baadhi ya familia za wenzetu (Tanzania) vikitikisa ardhi, milima, mabonde na mito. Vilio hivi vikitaka kupatiwa MAJIBU TU, ya ndugu zao waliopotea, kutekwa, kuuliwa au kufungwa (Ben Saanane, Azory Gwanda, Ma Sheikh wa Uamsho, Watu wasiokulikana kuhusu issue ya Mo Dewj na Tundu Lissu, na huyu kijana mwenzetu Frank Kapange, alietimiza siku 206 akiwa mochwari kisa ndugu kutaka mwili wake kufanyiwa uchunguzi wa daktari).

Mwili wa Frank Kapange watimiza siku 206 mochwari. - JamiiForums

Matabaka haya hayana mwisho mwema, historia haidanganyi. Tumeshuhudia nchi nyingi zikifanya uvunjifu wa haki ya binaadamu (Mauwaji, Ubakaji, Kufungwa kwa viongozi kisa maswala ya siasa) kwaajili ya VISASI vya kisiasa.

Mfano wa visasi vilivyoitingisha dunia,

● Master Sergeant SAMUEL DOE aliefanya mapinduzi ya kijeshi (Nchini Liberia) mnamo tarehe 12th April 1980 kwa kumuondoa Rais William R Tolbert.

MS Samuel Doe nae alikuja kuondolewa madarakani na Prince Johnson (Aliewahi kua mgombea mwenza na Charles Taylor) kwa KUKATWA MASIKIO, KUVULIWA NGUO ZOTE na kisha KUULIWA huku akioneshwa katika Television.

● Rais wa 29 wa U.S.A (29th President) Warren G. Harding. Alikua akicheza GOLF mnamo tarehe 26th July ila hakuweza kucheza zaidi ya kupiga mipira 6 tu (Kwa mchoko aliokua nao), kisha alifanya mhadhara na kutoa speech huku akijivutavuta (alitereza kwa kauli kwa kuiita ALASKA - NEBRASKA) kupelekea akataka kuanguka kwenye podium.

Alipofikishwa hopsitali, madaktari walisema alikula chakula kilichoharibika. Na mnamo tarehe 2th August 1923, rais huyo mwenye umri wa miaka 57 alifariki dunia ghafla katika hoteli ya Palace Hotel (SF).

Madaktari walisema sababu ya kifo chake kilikua ni STROKE (Declared a stroke as the cause of Death).

Na kwa maombi ya mke wake, Bibi Florence Harding, aliomba afanyiwe mume wake UZINDUKWAJI (Embalmed) mwili wake haraka ili usiharibike. Baada ya saa moja maiti ilichomwa sindano ya uzindukwaji bila kufanya upelelezi wa maabara kwa kina (Kuchoma ile sindano ili kuua ushahidi alilishwa sumu na MKEWE katika chakula alichokula). Na baada ya muda kupita Bi Florence alisikika akiongea na rafiki yake Bi Evalyn McLean kwa kusema "Sasa hili limeisha, naanza kuamini ilikua kwa madhumuni mema".

*** Haya ni baadhi (Yapo mengi sana) ya matukio ya kisasi/kisiasa yaliosababishwa na mizizi ya chuki/uonevu/uakandamizwaji/tamaa na kadhalika.

Wito wangu,

Turudi na tujitafakari, tupokee ushauri na tutende haki kwa kila mtu. Tanzania miaka mitano iliopita tulitukuka na kusifika ndio nchi inayoongoza kwa AMANI DUNIANI. Hii sifa, hakika ilikua ni HESHIMA KUBWA sana kwa Tanzania (Ndoto yangu, natamani sifa hii tuipate milele daima).

Uadilifu/Haki/Upendo ni miongoni mwa NGUZO za kila imani ya dini, na ndio chemu-chemu ya amani. Kukosekana hizi nguzo za dini husababisha uvunjifu wa amani.

Matabaka/Jeuri/Chuki/Kiburi sio sifa ya mwanaadamu wala maamrisho ya mungu.

KUMBUSHO;

Biblia.

* "(John 5:17 ESV) Matendo maovu (dhuluma) ni dhambi, lakini kuna dhambi zisizopelekea kifo".

* "(John 3:4 ESV) Kila mtu anafanya dhambi ndio anaefanya uvunjifu wa sheria, dhambi ni kuvunja sheria".

* "(Matthew 7:1-2 ESV) Usihukumu, vile wewe usingependa kuhukumiwa. Kwa hukumu uitoayo mdomoni ndivyo utakavyo hukumiwa, na kipimo utakachotumia kutoa adhabu ndiyo kipimo kitakachotumika kwako".

Qur'an.

* "[Az-Zumar, 22] Kwahiyo, wahusieni hao wenye mioyo (moyo) iliomigumu (wasio na huruma)".

* "[An-Nur, 22] Wape msamaha na uwasamehe".

* "[Al-Ma'idah, 13] Wasamehe, na uwatafutie sababu za kuwatetea makosa yao waliotenda. Hakika, Allah anapenda watenda mema".

* "Dhuluma haizidishi kitu chochote isipikua; Hasara, Kudhalilika, Kuangamia".

Nawasilisha kwa nia njema,
Ruhusa kunitolea povu nlipotereza.
 
Shida ni tabia tulio jijengea wanadamu jinsi ya kumuadhibu mtu wako wakaribu anae kuhusu na jinsi ya kumuadhibu mtu ambae sio wa karibu yako asie kuhusu shida sio yye shida tabia tulio zoea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono Hoja
Hili la watu kukaa mahabusu muda mrefu bila Kesi kutamletea a bad karma na nilizungumzia hapa

Magufuli is Getting Better and Better, He is Changing for The Better!. Hongera Sana!. - JamiiForums

P
Ninkweli mkuu Pasko.

Wakati mwingine tupitie Biblia Takatifu inasemaje juu ya mambo haya.

Mfalme Solomon aliomba sana apewe hekima katika utawala wake, asije mkosea Mungu.
Mfalme Solomon(Suleyman) anatushirikisha:


Zaburi 37:8
"Ukomeshe hasira, uache ghadhabu.
Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya."

Zaburi 37:28
"Kwa kuwa BWANA hupenda haki, wala hawaachi watauwa wake.
Wao hulindwa milele, Bali mzao wa wasio haki ataharibiwa."

Na katika kitabu cha Mithali, mfalme Solomon anatoa somo,

Mithali 8:15
"Kwa msaada wangu wafalme humiliki,
Na wakuu wanahukumu haki."

Tuyazingatie maandiko.
 
Wanasema mruka kihunzi lazima ajishauri na nyonga yake. Yeye atampenda jirani lakini nyonga zake zinaweza zisitake kuruka vihunzi. Nakinyume chake ni kweli.

Visasi vilianza kabla hajapata; ni ndoto kama ajenda yake ya visasi na chuki havijatimia. Fisi ndani ya bucha lazima amalize mifupa ndipo aondoke. Natumaini wenye bucha watashtuka na kulinda bucha zao.
 
Magufuli ni matokeo tu, tatizo la msingi lipo katika katiba yetu. Ukijaribu kuangalia muundo wa katiba yetu inatoa nafasi ya tabia binafsi za kiongozi kuwa ndio sheria za nchi. Hiki kitendo cha rais kutoshtakiwa akiwa au ametoka madarakani. Kifungu hiki kitalitesa taifa hili mpaka litakalofanyika marekebisho. Jaribu kuangalia nchi zote zenye maendeleo na demokrasia ya kweli kama kuna kifungu cha kutomshitaki rais akiwa au ametoka madarakani.

Kifungu hiki kinachompa rais kuwa Mungu, ndio kimezaa sheria yenye nguvu kuliko katiba na sheria iitwayo amri toka juu. Hii amri toka juu iliyo na nguvu ya ajabu kuliko katiba na sheria, ndio msingi wa mihimili ya nchi na taasisi za kimamlaka kuwa dhaifu kwenye utekelezaji wa sheria. Hapa ndio mahali nilipoona udhaifu wa Nyerere kwani katiba hii ilitungwa wakati wake, kwa ushawishi wake, au waliokuwa wakijipendekeza kwake. Na alikiri hilo kwa kusema katiba hiyo ingeweza kumgeuza dictator na haswa kifungu hiki ndio kilikuwa msingi wa kukiri kwake udhaifu wa hii katiba. Sioni Magufuli akikubali katiba ibadilishwe na kifungu hicho kutolewa kama marais wengine wa ccm waliopita na wala sioni kwa rais yoyote atakayepatikana kwa mfumo huu unaoruhusu wizi wa kura.
 
Najua Dr Magufuli ni muumini mzuri tu wa dini.

Biblia ina kanuni(sharia )kumi za Musa, wengi tunazishindwa hasa ile sharia ya sita!!!

Lakin katika sharia zote kuna sharia kuu mbili.

1. Mpende Mungu wako kwa uwezo wako wote na akili zako zote

2. Mpende jirani yako kama nafsi yako

Sheria ya kwanza katika hizi mbili haina utata, ingawaje kuna wanao amini katika ushirikina. Roho Mtakatifu anawafuatilia.

Hili la pili ndo gumu. Mtendee mtu kama utakavyojitendea nafsi yako.

Sasa nauliza, hivi mtuhumiwa wa wizi, ufisadi,uhujumu si haya ni makosa dhahiri?
Na adhabu zake ziko wazi.

Tumeona kesi ya mtu mmoja dhidi ya Waziri mwandamizi, akituhumiwa kutaka kumhonga.
Kesi ikatupiliwa mbali kwa vile ilikuwa ya hisia na hakuna ushahidi.

Kuna watu kadhaa wamewekwa ndani(Remand Prison), wengine kwa miaka inaelekea mitatu.

Tunatenda haki gani kama hakuna ushahidi, bali hisisa.

Nina uhakika watu wahawa wanapiga magoti kila usiku wakienda kulala, kumwomba Mungu aziguse nafsi zilizowaweka huko Rumande.

Tuelewane hapa, mimi siwatetei mafisadi, wezi au wahujumu.

The best political move ni kutaifisha mali ambazo wahusika wamezipata kwa matendo yao.

Kwaweka watu ndani kwa hisia, kukomesha, kulipiza kisasi au kwa kuonea tu, hakika ni dhambi juu ya uso wa dunia na mbingu.

Tulifikirie kwa makini hili tunapomaliza mwaka 2018.
Nadhani ni mahakama ndio inaamuru hao watu waende mahabusu huku kesi zikiendelea.

Nimewakumbuka le bilioneaaz mbebez wa stanbic aliyekuwa Ana shop Dubai shose.
Sioi Solomon sumari, Harry Kitilya, Dr Tenga, bilioneaaz muhuni shamte na wengineo. Mungu awape unafuu na kadhia za lupango



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais wa awamu ya nne alishwahi sema...

laiti mngejua nguvu na mamlaka niliyokua nayo kikatiba hata msingekua mnashinikiza hayo mnayotaka nifanye... hizo zinaitwa busara...

Awamu hii ni mwendo wa kutambuana who is who...


Cc: mahondaw
 
Najua Dr Magufuli ni muumini mzuri tu wa dini.

Biblia ina kanuni(sharia )kumi za Musa, wengi tunazishindwa hasa ile sharia ya sita!!!

Lakin katika sharia zote kuna sharia kuu mbili.

1. Mpende Mungu wako kwa uwezo wako wote na akili zako zote

2. Mpende jirani yako kama nafsi yako

Sheria ya kwanza katika hizi mbili haina utata, ingawaje kuna wanao amini katika ushirikina. Roho Mtakatifu anawafuatilia.

Hili la pili ndo gumu. Mtendee mtu kama utakavyojitendea nafsi yako.

Sasa nauliza, hivi mtuhumiwa wa wizi, ufisadi,uhujumu si haya ni makosa dhahiri?
Na adhabu zake ziko wazi.

Tumeona kesi ya mtu mmoja dhidi ya Waziri mwandamizi, akituhumiwa kutaka kumhonga.
Kesi ikatupiliwa mbali kwa vile ilikuwa ya hisia na hakuna ushahidi.

Kuna watu kadhaa wamewekwa ndani(Remand Prison), wengine kwa miaka inaelekea mitatu.

Tunatenda haki gani kama hakuna ushahidi, bali hisisa.

Nina uhakika watu wahawa wanapiga magoti kila usiku wakienda kulala, kumwomba Mungu aziguse nafsi zilizowaweka huko Rumande.

Tuelewane hapa, mimi siwatetei mafisadi, wezi au wahujumu.

The best political move ni kutaifisha mali ambazo wahusika wamezipata kwa matendo yao.

Kwaweka watu ndani kwa hisia, kukomesha, kulipiza kisasi au kwa kuonea tu, hakika ni dhambi juu ya uso wa dunia na mbingu.

Tulifikirie kwa makini hili tunapomaliza mwaka 2018.

Hivi ni yeye ndo anawaweka ndani?
 
Back
Top Bottom