Swali la kizushi: Makao makuu ya DPP yako wapi na kwanini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali la kizushi: Makao makuu ya DPP yako wapi na kwanini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 2, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Serikali ya JK jana imejisifia kwa kuwezesha TAKUKURU na CAG. Sote tunajua idara hizo mbili ambazo ni vinara katika kupigana na ufisadi sasa zina ofizi zao za kisasa - makao makuu na hata za mikoa/kanda. Lakini hakuna ofisi yenye matokeo ya moja kwa moja katika vita dhidi ya ufisadi kama ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP). Huyu ndiye mtu wa mwisho nchini anayeamua nani anashtakiwa kwa kosa gani na adhabu gani itafutwe. Baada ya majigambo yote yaliyotolewa jana nimebakia na hili swali - kwa kweli nimelirudia tu kwani nilishaliuliza mara kadhaa sasa. Nina maswali haya matano ya ugomvi:

  a. Makao Mkuu ya DPP yako wapi na kwanini?
  b. Ni ofisi ngapi za DPP mikoani ni mpya na zinazomilikiwa na idara kama ilivyo kwa TAKUKURU na CAG?
  c. Je kati ya DPP, CAG na TAKUKURU ni yupi anawatumishi wengi na bajeti kubwa ya utendaji na kwanini?
  d. Ni kwanini msisitizo uko kwenye uchunguzi sana kuliko kuleta mashtaka?
  e. Kwanini wabunge (wa CCM na UPinzani) wanamtegemea sana CAG na TAKUKURU kwenye hili la vita lakini hawaonekani kupigania uwezeshaji wa DPP?


  Mwenye kuweza kujuza atujuze.
   
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  1. Ofisi za DPP makao makuu ziko Sukari House.

  2. Kwa ufahamu wangu DPP hana ofisi yoyote ile mikoani ila anatumia
  ofisi za/na wanasheria wa serikali (State Attorneys) kufanya kazi zake

  3. Takukuru ndiyo yenye wafanyakazi wengi na bajeti kubwa maana wako mpaka wilayani.

  4. Tuhuma zinazothibitika na kufikishwa mahakamani ni chache sana labda 5%.

  5. Nakubaliana na wewe kuna haja ya Ofisi za DPP kuboreshwa!
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ohoo,nami ckua nalifahamu hilo
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Asante sana; kwanini iko Sukari House? Kwanini hajajengewa ofisi yake kama CAG na TAKUKURU?
   
 5. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mkuu, soma jibu langu kamili kwa hoja zako za awali halafu tujadiliane
  maana natumia cmu na nilikuwa nikiedit na kujibu maswali yako mengine
  kwa awamu
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Si lazima ofisi zote za serikali ziwe na majengo yao. Hata huko uliko Mwanakijiji kuna ofisi nyingi tu za serikali ambazo hukodi kutoka real estate, na huhamahama. Ukitaka nikutolee mfano nitafanya ikibidi. Mfano huko Marekani Taasisi ya Social Security ambayo ni taasisi kubwa ya kiserikali yenye kuchota pesa nyingi za wafanyakazi kwa ajili ya mafao ya uzeeni majengo mengi hutumia ya kupanga, ingawa kuna baadhi ya ofisi zina majengo yao.

  Serikali katika nchi zilizoendelea hutumia njia ya kukodi baadhi ya majengo ambayo humilikiwa na makampuni/mashirika ya umma ili kuokoa hasara ambazo zinaweza kupatikana kama zitakosa wapangaji.

  Kama Makao Makuu ya DPP ni Sukari Haouse, binafsi sioni tatizo, kwani jengo hilo lilijengwa na pesa za wakulima na walipa kodi.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wanatumia ofisi zao hapo Sukari House Bure kwa vile zimejengwa na fedha za umma au wanapanga?
   
 8. K

  Keil JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Swali la nyongeza:

  Zama zile Mama Nagu akiwa Waziri wa Sheria na Katiba, alisema Wizara yake ilikuwa kwenye mchakato wa kuliondolea Jeshi la Polisi kazi Uendesha Mashitaka, na kwamba waendesha mashitaka wote wangekuwa chini ya DPP moja kwa moja na kwamba wangekuwa na ofisi zao mikoani. Kwa mwenye ufahamu, any progress kwenye hili?
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama wanatumia bure hilo ndilo swali la muhimu kuuliza, kadiri ya uelewa wangu wanapaswa kulipa pango.
   
 10. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Wanapanga. Kama ukisoma edited version ya jibu langu la awali utaona DPP hana manpower ya kutosha na mikoani anawakilishwa na ofisi za wanasheria wa serikali. hivi sasa ndio kuna mipango ya DPP kuongezewa manpower.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  May 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi CIA au NSA wana majengo yao? yes! kwanini? kutokana na uzito na umuhimu wa kazi yao. CAG na TAKUKURU wanamtegemea kwa asilimia 100 DPP kuweza kukamilisha kazi zao sasa kwanini wao wanajengewa maofisi kila kona ya nchi isipokuwa DPP? Jaribu kujibu hayo maswali mengine pia (ya raslimali na wabunge)
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  May 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa kadiri ninavyokumbuka mwaka 2008 walipitisha sheria iliyofanya ofisi ya DPP kuwa idara maalum wenyewe wanaita National Prosecution Services. Na kuanzia wakati huo wamekuwa kwenye transition ya kuhamisha uendeshaji mashtaka kutoka polisi kwenda kwenye idara hii. Hata hivyo bado kuna maeneo mengine nchini ambayo bado kesi zinaendeshwa na polisi sijui ilitakiwa iwe hadi lini kabla hawajafikia full compliance.
   
 13. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ndio. kuna massive recruitment ya wanasheria unafanyika ili DPP aweze kuendesha kesi za jinai moja kwa moja kuliko hivi sasa ambapo anawakilishwa na waendesha mashtaka wa Polisi na Takukuru kwenye mahakama za wilaya na state attorneys mahakama kuu.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  May 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Unaweza kukubaliana na mimi kuwa priority za law enforcement zimegeuzwa? TAKUKURU inakuwaje na waendesha mashtaka wengi kuliko watu wa DPP? Unaweza kusema ofisi ya DPP ina vitendea kazi vya kutosha kuweza kuhakikisha kesi nyingi inazotakiwa kufanyia maamuzi zinashughulikiwa kwa haraka?
   
 15. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mkuu rejea post yangu ya awali. nimei edit na kujibu maswali yako yote. tujadiliane from there.
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Serikali ni kubwa na pana sana. Kama kila Wizara, Taasisi, Idara kuwe na majengo yao inawezekana ila inaweza kugharibu pesa nyingi kwa sababu baadhi ya taasisi nyeti hazina kawaida ya kujiendesha kwa uwazi na pengine kujisajiri kama kampuni binafsi, hali inayosababisha kuhamahama kadiri ya mahitaji au sababu nyingine wanazojua wao.

  Ingawa ofisi hiyo ya Mkurugunzi wa mashtaka nchini si nyeti sana kama baadhi ya idara nyeti za serikali, lakini ukubwa wa ofisi hiyo kwa sasa ni jina zaidi na dhana yenyewe ya uwajibikaji wakati idadi ya watumishi ni ndogo. Hilo linaweza sababisha serikali kutotilia muhimu kuwa na jengo lao. Lakini kadiri mahitaji yanavyokuwa na ofisi hiyo inavyozidi kupanua wigo huko siku za usoni inawezekana hilo likafanyika.
   
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  May 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  As of now kesi zote za umma zinashughulikiwa na kupelekwa mahakamani na dpp. Polisi wakishakusanya ushahidi wanampa dpp ndo anaamua kama anapeleka mahakamani ama la. Ni kweli dpp anahitaji manpower. Lakini hata huko mahakamani kukoje?
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  May 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kokolikoo, unaweza kukubaliana na maelezo ya Candid Scope hapa kwamba DPP siyo ofisi nyeti kihivyo ukilinganisha na TAKUKURU au CAG kwa jinsi nilivyomuelewa na ndio maana haijawezeshwa kama zinavyowezeshwa ofisi hizi nyingine?
   
 19. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #19
  May 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Of course nakubaliana na wewe. kwa taarifa yako Takukuru imeanza kupanuka kwa kasi mwaka 1999 baada ya utekelezaji wa mapendekezo ya tume ya warioba kuanza kuwa implemented.
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  May 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kila kitu kinakwenda kwa wakati wake. Hata hao CAG walikuwa hawana ofisi katika awamu zote zilizopita ni Kikwete ndiye aliyeliona kuwa hilo ni tatizo na akaamuru wawe na ofisi zao "independently".
   
Loading...