Swali la Kizushi: Kwanini CCM haiwakemei wabunge wake wanaoondoka na "vyao"?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Baada ya kusikia habari za Nyamagana, Mbeya Mjini na sasa Iringa Mjini; na kuja kugundua kuwa viongozi wa umma wanaweza kufanyia matengenezo ofisi za umma na kuzipamba kwa gharama zao na muda wao ukiisha ni halali kwao kuondoa na "vilivyo vyao" na nikizingatia kuwa hadi hivi sasa hakuna kiongozi yeyote wa juu wa CCM aidha aliyetoa mwongozo wa nini kifanyike au kukemea ninachukulia kuwa yanayoendelea aidha yamepata kibali au yamebarikiwa (nadhani ni kitu kile kile) na uongozi huo.

Kama ni hivyo, wazo moja baya limenijia ambalo nimejaribu kulikataa sana maana yake. Swali lenyewe ndiyo hilo limekaa kizushi zushi. Sijui nauliza nini lakini nadhani nauliza kitu.
 
ukiona hata mkuu wa nchi kanyamaza, basi ujue na yeye ana 'vitasa na mapazia' yake Ikulu.
 
haya siyo ya kuyaacha yapite hiv hiv, ni lazima viongozi wa nchi walikaripie hili, bila hivyo ndo utakuwa mtindo kila baada ya UCHAGUZI
 
Si mnaona urais sasa ni mradi wa familia ya kikwete badala ya taasisi?..............ni ajabu na kweli kuwa lazima chadema wakichukua ikulu 2015 kikwete ataondoa kila kitu pale patakatifu
 
Ofisi ya mbunge ni ofisi ya serikali iliyo chini ya DAS. Masha aliponunua samani kwa ajili ya ofisi ya mbunge, samani zile zilipaswa kujumuishwa kwenye inventory ya samani za ofisi ile ikionyeshwa kuwa ilikuwa ni donation toka kwa mbunge Masha. Hii ya Masha na wenzake inakupa picha ya utendaji wa serikali yetu legelege.
 
Hata kama alitoa pesa zake mwenyewe kuweka vitu vyake, basi akitoa vyake aturudishie vile alivyovikuta, And dont tell me kwamba vimechakaa mimi kigoda alichokuwa nacho bibi hata kabla sijazaliwa mpaka leo kipo
 
nadhani hapana budi MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI awe anakagua matumizi ya kila ofisi ya mbunge kwani nao huwa wanapewa fungu toka mfuko mkuu wa serikali na ukaguzi huo uwe unafanyika kabla hawajagombea kutetea kiti chao yaani iwe precondition kwa mbunge anayemaliza mda wake lazima akaguliwe ndo aruhusiwe kugombea tena
 
Hata kama pesa ya kununua hizo samani ni yaserikali, baadhi ya viongozi husika wakimaliza muda wao huchukua hizo samani kupelekwa makwao na kubadili na kukuu.

Lakini mkuu una ujua kwamba huo ukarabati wa ikulu haufiki kwenye nyuma zile za wafanyakazi ambazo zipo upande wa kaskazini mashariki?
 
Natoka nje ya mada
Je ni kweli mawaziri, makatibu wakuu na presdential appoitnment wote wako entitled kupata vitu vipya kama sofa,magari, etc no matter wanavyokuta vimetumika kwa muda gani?
 
Back
Top Bottom