Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,189
- 39,954
Kama miaka 10 iliyopita hivi nilipata safari ya kikazi kwenda huko mbali kwa muda wa miezi sita. Kwa sababu ndoa yangu ilikuwa bado ni changa, nikaona nimtafutie majukumu mazito mama watoto wangu ili nitakapokuwa huko nje, asiweze kushawishika na mabaharia wa mjini.
Nikampa kazi ya kwenda kusimamia ujenzi wa nyumba ya kufikia huko kijijini; siku ilipofika ya kuondoka, niliondoka na yeye akaenda kijijini kwa ajili ya kutekeleza majukumu niliyomuachia. Nikiwa huko ugenini, nilikuwa nafanya mawasiliano ili kujua kinachoendelea nyumbani, pamoja na kazini.
Baada ya kumaliza kilichonipeleka huko ugenini, nilirudi nyumbani na familia ilinipokea vizuri; ingawa nilikuwa na kama wiki mbili hivi za kupumzika kabla ya kuripoti kazini. Kwa muda ule niliutumia kuwa karibu na familia, pamoja na kupunguza uchovu wote niliotoka nao safari.
Ndipo mama watoto, akanishawishi twende kijijini ukaone kazi uliyoniachia; nami nikamkubalia nikamwambia twende na familia angalau tukaone alichokifanya. Kwa ujumla alifanya kazi nzuri, nami nikamwambia inabidi tuizindue kwa kulala humo angalau kwa siku tatu.
Kesho yake jioni majira ya saa 11 jioni, niliamua kujilaza kwenye veranda hapo nje ili kupata upepo wa nje, pamoja na kunyoosha mgongo vizuri. Baada ya kama nusu saa hivi, nilihisi kitu kimenipiga shingoni, najaribu kugeuza shingo hivi, inakataa na kuwa ngumu huku inauma, nainua mkono wa kushoto unakata, mguu wa kushoto unakataa, kichwa kinagoma; daa nililia kama mtoto mdogo ,ndipo watu wakaja kwa ajili ya kunipa msaada. Wakajaribu kunikanda na aina fulani ya majani, nafuu haikupatikana; ikabidi wanipeleke hospitali ya wilaya, baada ya dokta kunicheki haoni tatizo, zaidi ya kunipa dawa za kutuliza maumivu.
Ndipo baba mmoja akawa na wazo, hebu mpelekeni kwenye tiba ya asili; Kule na wenyewe wakafanya yao, wakasema kama ningecheleweshwa kuna uwezekano nisingemaliza wiki. Ila wakasema changamoto ni huko kazini, na hata ukirudi huko watakushangaa kwa kusalimika. Kesho yake ilipofika maumivu hakuna na nikawa niko powa,tukalipia gharama, na tiba nyingine nikaondoka nazo kwa ajili ya kutumia.
Safari ya kurudi kazini ilipowadia, nilipanda basi na kwenda huko mkoani; tunakaribia kufika huko mkoani, basi nililokuwemo likapoteza uelekeo na kuingia kichakani na kupinduka; bahati nzuri lililala kiubavu na hakuna mtu aliyefariki zaidi ya majeraha tu; mi niliumia vidole vya mikononi kwa sababu nilikuwa napiga ngumi ili nipasue kioo. Ndipo tukapata usafiri mwingine na kuondoka.
Nilipofika kazini, kila mmoja ananitazama; umefikaje fikaje huku; mi nikawa nawauliza kwa nini mnaniuliza hivyo? Wakawa wanacheka tu, basi tukaendelea na maisha ya mzigoni, ila kuna wengine waliomba kuhama kutokana na sababu zao wanazozijua. Ilinibidi nisiwe nasafiri safiri kwa muda mpaka ile kumbukumbu ya ajali itakapoisha. Na nilifanikisha hilo.
Swali la kizushi; Kwa nini umtendee mwenzako mabaya?
NB: Ishi na wenzako kwa akili, 'co-workers are not your friends'