Swali la KIZUSHI: Kwa nini hakuna cheti kwa Divisheni Ziro?

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Nini sababu ya mtu aliyepata divisheni ziro kutopewa cheti cha kidato cha nne au cha sita? Si ni matokeo aliyoyapata baada ya kushiriki mitihani? Kitamsaidiaje, hiyo si ni yeye mwenyewe atajua? Gharama za cheti - si alilipia mitihani sawa na wenziwe? Ziro si ni moja tu ya matokeo ya mitihani? Kwani ziro inaweza kutolewa kwa mtu asiyefanya mtihani?
 
Ukipewa cheti maana yake umepata kitu,na sefuri maana yake NOTHING.

Kwa hyo ukipata zero maaana yake umepata nothing.
 
unaelewa nini maana ya ZERO au sifuri kwa kiswahili??

Kama ulikuwa hujui ni kwamba SIFURI ni kitu ama namba ambayo haina thamani ikiwa peke yake. Kwa kifupi tu ni kwamba mtu aliyepata Sifuri maana yake hakuna chochote cha thamani alichokifanya na hastahili reward yoyote
 
Si ndio unipatie cheti kinachoonesha nilifanya mtihani nikapata sefuri?

Asinipe reward yoyote, zaidi ya cheti kinachoonesha matokeo yangu ya ziro. Shida iko wapi?
 
Sijawahi kusikia division zero au disco inahitajika sehemu yeyote ile mpaka kuwe na mahitaji ya cheti kuthibitisha hilo.
Nataka nikiweke kwenye fremu nikining'inize sebuleni. Kwa nini unizuilie cheti changu kwa vile tu unadhani hakuna mtu mwingine atakihitaji?
 
Ukinunua machungwa 5 halafu njiani ukayapoteza kwa uzembe wako unarudi kwa muuza machungwa akupe machungwa sifuri ili ukifika nyumbani uwaambie nimenunua machungwa sifuri.

Au dhana ya sifuri/ziro hukujifunza ukiwa vidudu mkuu?
 
Mfano wako ni non sequitur.

Nimefanya mtihani, nimepata D moja na F6. au nimepata F saba. Ukanipatia cheti kama ulivyowapatia waliopata A saba, nikikipoteza na kuja kudai cheti kingine, ndio mfano unaousema.

Mada kwenye OP ni kwamba nimetoa hela kamili kununua machungwa. Lakini unasema hutaki kuniuzia machungwa, na hela hunirejeshei.

Divisheni Ziro ya kidato cha nne ni kubwa kuliko darasa la saba. Divisheni ziro ya kidato cha sita ni kubwa kuliko kidato cha nne. Mpaka sasa sijapata jibu lizingatialo mantiki ya swali la awali: nadhani kila aliyefanya mtihani anastahili kupewa cheti kinachoonyesha matokeo aliyoyapata, iwe au isiwe divisheni ziro, cheti tupewe. Si ni ndio?
 
Mfano wangu ni so paratable.

Umefanya huo mtihani under which circumstances?? Umepewa guidelines umezikiuka halafu unataka huruma.

Kwanza sijui unalazimisha kitu ili hali hata umekubali kwamba kupata D moja ni ziro.

Mkuu unadai upewe ziro
 
Si ndio unipatie cheti kinachoonesha nilifanya mtihani nikapata sefuri?

Asinipe reward yoyote, zaidi ya cheti kinachoonesha matokeo yangu ya ziro. Shida iko wapi?
Kwa hoja za namna hii kweli unasadifu zero kichwani.

Nimeshakwambia ukipata sifuri ni sawa sawa na hamna chochote ulichokifanya. Sasa hicho cheti kitatoka wapi wakati hamna ulichokifanya??
 
Kwa hoja za namna hii kweli unasadifu zero kichwani.

Nimeshakwambia ukipata sifuri ni sawa sawa na hamna ulichokifanya.Sasa hicho cheti kitatoka wapi wakati hamna ulichokifanya??

Walijuaje kama ninastahili ziro ikiwa sikufanya mtihani? Cheti kitatoka kulekule vinakotoka vya waliopata divisheni wani.
 
Naona umeanzisha uzi kwaajili ya ubishi na siyo uelewa. Anyway kama umekuja kutafuta wingi wa comment ngoja waje wajinga wenzio muendelee na ujinga wenu. Asante
 
Mfano wangu ni so paratable.

Umefanya huo mtihani under which circumstances?? Umepewa guidelines umezikiuka halafu unataka huruma.

Kwanza sijui unalazimisha kitu ili hali hata umekubali kwamba kupata D moja ni ziro.

Mkuu unadai upewe ziro

Wanaokiuka guidelines hufutiwa matokeo. Yangu hayajafutwa. Nimepata tu FFFDFFF. Nataka tu cheti kinachoonesha matokeo hayo ya FFFDFFF na hiyo divisheni ziro. Waiboldi wakipenda, lakini wanipe cheti. Juu ya nini wao kukatalia cheti changu cha divisheni ziro?
 
Naona umeanzisha uzi kwaajili ya ubishi na siyo uelewa. Anyway kama umekuja kutafuta wingi wa comment ngoja waje wajinga wenzio muendelee na ujinga wenu. Asante

Nimeuliza ili mkuu unitoe ujinga. Sasa mbona hutoi sababu yoyote ya kwa nini mtu aliyefanya mtihani anyimwe cheti kinachoonesha matokeo ya mtihani wake, kwa vile tu matokeo hayo ni ya FFFDFFF?
 
Ukipewa cheti maana yake umepata kitu,na sefuri maana yake NOTHING.

Kwa hyo ukipata zero maaana yake umepata nothing.

Je mtu aliye pata division 0 anaweza kuwa na elimu ndogo kama ya darasa la saba? Au atafanana na darasa la saba! Kielimu?
Kwangu Mimi Miata minne ya kusoma sec. na kitoka na. Sifur hakuwezi linganishwa na mtu aliye ishia la saba
 
Exactly my point.

Na tukichukulia hoja zilizotolewa to their logical conclusion: mwenye divisheni ziro hapati cheti. Mwenye divisheni wani anapata cheti kimoja. Mwenye divisheni 2 anapata vyeti viwili. Divisheni 3 vyeti vitatu na divisheni 4 vyeti vinne :p😁😀
 
Nataka nikiweke kwenye fremu nikining'inize sebuleni. Kwa nini unizuilie cheti changu kwa vile tu unadhani hakuna mtu mwingine atakihitaji?
Nafikiri waweza kuchukua yale matokeo yako na kuyatengenezea kitu mfano wa cheti na kufanya hilo jambo unalotaka kufanya.
 
Unayo hoja....lakini sasa bandugu hicho cheti cha ZERO unakipeleka wapi? Unakitundika ukutani kama ukumbusho wa Kristo?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom